Je Wamakonde wanaogopa kufa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Wamakonde wanaogopa kufa?

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Zinduna, May 30, 2012.

 1. Zinduna

  Zinduna JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 2,384
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Hebu tuangalie imani zao wakati wa maziko, pale wanapokuwa wameondokewa na mpendwa wao. Kwa kawaida wakati wa Maziko Wamakonde huwa na maombi tofauti na yale yanayofuatwa na madhehebu mengine. Badala ya Sheikh au Kasisi kusoma dua, Wamakonde wana desturi ya kuieleza maiti maombi na maonyo ili marehemu huyo asije patwa na madhara wala asiandamwe na mikasa katika safari yake huko aendako, na pia ndugu wanaobaki nyuma wasikabiliwe na mabalaa na mikosi ya aina yoyote. Wenyewe wanaamini kwamba mabalaa huongozana, yaani likitokea moja hufuata la pili, la tatu na kadhalika. Kwa mujibu wa simulizi zao, kuna madai kwamba pale mambo hayo ya mila yanapopuuzwa vifo mfululizo hutokea katika familia husika.

  Mkuu wa mazishi Huieleza maiti wakati wa maziko:

  "Ndugu umeacha jembe, mshale, shoka, nyumba na kazi kwa hiyari yako mwenyewe, hakuna aliyekulazimisha kufunga safari hii, ile wewe mwenyewe umeazimia. Umetuacha sisi huku nyuma kwa hiyari yako mwenyewe, Hivi, ufikapo kwenye ukomo wa safari yako, ukaeleze yanayokuhusu wewe binafsi. Wakikuuliza ‘Wako wanadamu wengine waliobaki?' ukawajibu, ‘hapana.' Ujitahidi kuwathibitishia kwamba ni wewe tu peke yako, hakuna mtu mwingine aliyebaki."

  Kwa maneno hayo, inadhihirisha wazi kabisa kwamba waliobaki nyuma wanaogopa kufa. Ingawa wanajua kuwa kufa kupo, ila kama kunaweza kukwepeka basi ombi lao lisikilizwe!

  Hata hivyo inadaiwa kwamba mila hii bado inafuatwa na Wamakonde wa Msumbiji, tofauti na Wamakonde wa Tanzania ambao mila kwa kiasi kikubwa zimeathiriwa muingiliano wa makabila na dini hizi za mapokeo.
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Aiseee. . .
  Nimependa maagizo na angalizo lao. Umejipeleka mwenyewe, uongelee mambo yako mwenyewe.

  Nwy nlitaka kukuuliza hivi we Zinduna show yako ndo imefulia ama?
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Inafurahisha ubongo!
  Kawaida, kuachana na mpendwa wako na kwenda kumzika ni ngumu sana, ndio maana huwa kuna taratibu mbalimbali zinafanywa na jamii mbalimbali, hii ikiwa ni kuvuta muda tu na kutafuta pozi la kumtelekeza marehemu kaburini.
   
 4. Zinduna

  Zinduna JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 2,384
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Yaani Maiti inaambiwa iache kiherehere, izungumze mambo yake yenyewe!
  Lizzy Zinduna Talk Show ni kila JUMAMOSI saa nne asubuhi, na show inadumu kwa wiki nzima.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #5
  May 30, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Heheheheh. . .ni noma.

  Ahhhh mie nshaboreka. Embu nipe maswali utakayoniuliza kwanza nikariri majibu, sitaki kuaibika.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. Zinduna

  Zinduna JF-Expert Member

  #6
  May 30, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 2,384
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Lizzy Hayo hayo ya Bishanga, yageuze kichwa chini miguu juu!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #7
  May 31, 2012
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 934
  Trophy Points: 280
  Lets get to serious matters, Zinduna wewe ni mwanaantrhopolojia?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Kipaji Halisi

  Kipaji Halisi JF-Expert Member

  #8
  May 31, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 2,263
  Likes Received: 204
  Trophy Points: 160

  ...hahahahahaha..wamakonde wa Dar au Mtwara...ama kule Msumbiji. Zinduna..ila unanikumbusha enzi hizo nakaa maeneo ya Migombani....nilkua naenda msasani au Mikocheni A..kuangalia Ngoma zao..Thanx Zindu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...