Je, Wakati umefika wa watanzania kulipia Tv licence kwa kila mmiliki wa television ama computer

Mbase1970

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
6,054
4,601
Nimefuatilia kwa umakini malumbano ya wabunge wetu wa upinzani na wale wa chama tawala kuhusu taarifa ya serikali kuzuia maonyesho ya moja kwa moja (Live Coverage) ya Bunge letu tukufu la mwaka huu.

Ili kwa serikali kuondokana na lawama zisizo kuwa za msingi ama kusaidia kukuza popularity ya baadhi ya wabunge ingekuja na wazo la kuanza kuwatoza wananchi TV Licence.Halafu pia ianzishwe channel pekee mahsusi kwaajili ya vikao vya bunge tu iitwe TBC Parliament ama TBC Bunge. Maana waheshimiwa walikua wakitolea mifano nchi nyingine lakini hawakutaka kuishauri serikali ianzishe kodi.

Ni bora tulipie TV zetu ili mara nyingine tukijilinganisha na nchi zilizoendelea basi tuwe tunafanya kama wao wanavyofanya. TBC Taifa itaendelea na programme zake za kawaida ila TBC Bunge itakua kazi yake moja tu kutuonyesha nini kinatokea bungeni hata kama shanga zitakatwa bungeni tuweze kuziona wenyewe bila kungoja kina Kubenea watueleze kwenye mwanahalisi siku ifuatayo. Kwa kuanzia 5000 kwa mwezi ni tosha.
 
Yani kulipia ving'amuzi hamjaridhika sasa mnataka tulipie tv baada ya hapo redio kisha sofa then vitanda mwisho watoto. Yani sijui mnataka kutupeleka wapi. NOOOOOOOOOOOO
 
Back
Top Bottom