habari zimezagaa kwenye mitandao ya simu na kule Dodoma kuwa aliyepiga kura za hapana ni Lowassa na Bashe ambao walikuwa mstari wa mbele kutaka kiti na Urais vitenganishwe japokuwa hili ni gumu kuthibitika (siri yao wao wenyewe), ili wapate mwenyekiti wa kambi yao na baada ya mpango huu kukwama waliamua kumuaibisha JK kama ilivyo ada yao kwa kuanzisha harakati za kutaka apigiwe kura za Hapana apate aibu ya mwaka, japokuwa pia walidhibitiwa kwa kuanzisha utaratibu wa kupiga kura kwa mikoa na hapo ndipo
Kama demokrasia ya kweli ingechukua mkondo wake ndani ya uchaguzi wa ccm ,m/kiti wa kitaifa wa chama hicho asingepata kura alizopata.Kusema m/kiti alishinda kwa kishindo kwa mazingira ya uchaguzi ulivyofanyika ccm imeongeza udhaifu.Hakukuwa na haja ya kumbeba mtu eti kuwaaibisha maadui wa chama.Chama kilichokomaa kinakuwa tayari kumwondoa kiongozi ye yote aliye dhaifu.CCM acheni demokrasia ichukue mkondo wake! Mnahubiri demokrasia halafu ninyi wenyewe mnafanyiana udikteta. Kuna haja gani ya kupiga kura kama mnaowachagua mmeshawapanga na mnawajua? Mnapanga kuwajua wanaowakataa ndani ya chama ... ndo kujenga chama huko? Kama ni hivyo basi vikao vyenu vingi ni vya kupoteza muda na fedha ambayo ingetumika kutatua matatizo ya wananchi.
Lini mtapiga kura za kuwavua uanachama magamba na pia kukubali kuacha kutumia polisi kuteka, kutesa na kuua raia wasiokuwa na hatia eti ili kuzuia mabadiliko na mawazo mbadala.
Hivi zile siku 90 za Nape kuwavua wezi wenzake magamba ziliishia wapi????
Nape hakuungwa mkono na Mukama,Sasa subiri kiama cha EL mbele ya Kinana.Chezea JK wewe.Hivi zile siku 90 za Nape kuwavua wezi wenzake magamba ziliishia wapi????
Kinana-Arusha!Nape hakuungwa mkono na Mukama,Sasa subiri kiama cha EL mbele ya Kinana.Chezea JK wewe.
Wadau wa jf siku moja kabla ya mkutano mkuu Dodoma, mh Lowassa aliwaita wajumbe wote wa mkoa waArusha nyumbani kwake Dodoma ili kushiriki chakula cha jioni.
Baada ya hapo aliwaomba wajumbe wa mkoa wa Arusha woote kumpigia Jakaya kura za ndiyo. Hii ni kutokana na habari zilizozagaa kuwa lowassa anapiga kampeni ya kura za hapana kwa jakaya. Wajumbe walisimama kuchangia mmoja mmoja huku wakilaani hao wanaovumisha kuwa mkoa wa Arusha umejipanga kupiga kura za hapana kwa jk, walimuhakikishia mh Lowassa kuwa hilo halipo na kura zote za ndiyo ni kwa jk.
Mjumbe mmoja alitoa ushauri kuwa ili mkoa wa Arusha usije ukachafuliwa ni vyema kila mkoa ukapiga kura kwenye sanduku lake. Katika hafla hiyo alikuwepo katibu wa ccm mkoa wa Arusha Marry Chatanda. Na matokeo yake mkoa wa Arusha haukuwa na kura za maruhani.