Je, wajua nani aliyebuni kura za m/kiti wa CCM ktk mkutano mkuu Dodoma zipigwe kimkoa?

Sanare S

Member
Dec 31, 2011
42
7
Wadau wa jf siku moja kabla ya mkutano mkuu Dodoma, mh Lowassa aliwaita wajumbe wote wa mkoa waArusha nyumbani kwake Dodoma ili kushiriki chakula cha jioni.

Baada ya hapo aliwaomba wajumbe wa mkoa wa Arusha woote kumpigia Jakaya kura za ndiyo. Hii ni kutokana na habari zilizozagaa kuwa lowassa anapiga kampeni ya kura za hapana kwa jakaya. Wajumbe walisimama kuchangia mmoja mmoja huku wakilaani hao wanaovumisha kuwa mkoa wa Arusha umejipanga kupiga kura za hapana kwa jk, walimuhakikishia mh Lowassa kuwa hilo halipo na kura zote za ndiyo ni kwa jk.

Mjumbe mmoja alitoa ushauri kuwa ili mkoa wa Arusha usije ukachafuliwa ni vyema kila mkoa ukapiga kura kwenye sanduku lake. Katika hafla hiyo alikuwepo katibu wa ccm mkoa wa Arusha Marry Chatanda. Na matokeo yake mkoa wa Arusha haukuwa na kura za maruhani.
 
Lini mtapiga kura za kuwavua uanachama magamba na pia kukubali kuacha kutumia polisi kuteka, kutesa na kuua raia wasiokuwa na hatia eti ili kuzuia mabadiliko na mawazo mbadala.
 
Inawezekana mleza uzi unamaanisha icho ulichoeleza lkn pia inawezekana una nia ya kumsafisha Edo asionekane alikuwa na nia mbaya kwa JK maana unafahamu kina Nape wanapita sana huku. Vyovyote iwavyo kiukweli aliyetoa wazo la kupiga kura kwa mikoa nampongeza sana maana alimaliza kabisa uwezekano wa watu kumkataa JK sababu ingekuwa rahisi sana kuwagundua waliofanya hivyo.
 
Habari zimezagaa kwenye mitandao ya simu na kule Dodoma kuwa aliyepiga kura za hapana ni Lowassa na Bashe ambao walikuwa mstari wa mbele kutaka kiti na Urais vitenganishwe japokuwa hili ni gumu kuthibitika (siri yao wao wenyewe), ili wapate mwenyekiti wa kambi yao na baada ya mpango huu kukwama waliamua kumuaibisha JK kama ilivyo ada yao kwa kuanzisha harakati za kutaka apigiwe kura za Hapana apate aibu ya mwaka, japokuwa pia walidhibitiwa kwa kuanzisha utaratibu wa kupiga kura kwa mikoa na hapo ndipo
 
habari zimezagaa kwenye mitandao ya simu na kule Dodoma kuwa aliyepiga kura za hapana ni Lowassa na Bashe ambao walikuwa mstari wa mbele kutaka kiti na Urais vitenganishwe japokuwa hili ni gumu kuthibitika (siri yao wao wenyewe), ili wapate mwenyekiti wa kambi yao na baada ya mpango huu kukwama waliamua kumuaibisha JK kama ilivyo ada yao kwa kuanzisha harakati za kutaka apigiwe kura za Hapana apate aibu ya mwaka, japokuwa pia walidhibitiwa kwa kuanzisha utaratibu wa kupiga kura kwa mikoa na hapo ndipo

Team Membe
 
CCM acheni demokrasia ichukue mkondo wake! Mnahubiri demokrasia halafu ninyi wenyewe mnafanyiana udikteta. Kuna haja gani ya kupiga kura kama mnaowachagua mmeshawapanga na mnawajua? Mnapanga kuwajua wanaowakataa ndani ya chama ... ndo kujenga chama huko? Kama ni hivyo basi vikao vyenu vingi ni vya kupoteza muda na fedha ambayo ingetumika kutatua matatizo ya wananchi.
 
Kama demokrasia ya kweli ingechukua mkondo wake ndani ya uchaguzi wa ccm ,m/kiti wa kitaifa wa chama hicho asingepata kura alizopata.Kusema m/kiti alishinda kwa kishindo kwa mazingira ya uchaguzi ulivyofanyika ccm imeongeza udhaifu.Hakukuwa na haja ya kumbeba mtu eti kuwaaibisha maadui wa chama.Chama kilichokomaa kinakuwa tayari kumwondoa kiongozi ye yote aliye dhaifu.
 
Hicho chama kimejaa visa na mikasa tu. Kwani kuna ubaya gani mkimpigia kura za hapana mwenyekiti!!! Kama hatakiwi si hatakiwi tu!!! Ndiyo maana huwa nasema siku zote kwamba ndani ya chama cha magamba hakuna hata chembe ya demokrasia. Ni usanii mtupu tena usanii uliokubuhu.
 
Lini mtapiga kura za kuwavua uanachama magamba na pia kukubali kuacha kutumia polisi kuteka, kutesa na kuua raia wasiokuwa na hatia eti ili kuzuia mabadiliko na mawazo mbadala.

Ni bora ulitoka ktk media na kuvaa gwanda. Hujui kujibu hoja
 
Mimi nawashauri CCM ili kuzuia kura hizo 2 za HAPANA next time wafanye uchaguzi wa MLOLONGO kama kule Kenya enzi za MTUKUFU Daniel Arap Moi.

Uchaguzi wa MLOLONGO ni mpiga kura kusimama nyuma ya mgombea anayempenda. That means kumchagua Mwenyekiti wa CCM wajumbe wa Mkutano mkuu watatakiwa kusimama aidha nyuma ya PICHA ya JK au Nyuma ya picha ya KIVURI.

You know who will win the landslide votes!

Dmocracy in CCM is a foreign word!
 
Wadau wa jf siku moja kabla ya mkutano mkuu Dodoma, mh Lowassa aliwaita wajumbe wote wa mkoa waArusha nyumbani kwake Dodoma ili kushiriki chakula cha jioni.

Baada ya hapo aliwaomba wajumbe wa mkoa wa Arusha woote kumpigia Jakaya kura za ndiyo. Hii ni kutokana na habari zilizozagaa kuwa lowassa anapiga kampeni ya kura za hapana kwa jakaya. Wajumbe walisimama kuchangia mmoja mmoja huku wakilaani hao wanaovumisha kuwa mkoa wa Arusha umejipanga kupiga kura za hapana kwa jk, walimuhakikishia mh Lowassa kuwa hilo halipo na kura zote za ndiyo ni kwa jk.

Mjumbe mmoja alitoa ushauri kuwa ili mkoa wa Arusha usije ukachafuliwa ni vyema kila mkoa ukapiga kura kwenye sanduku lake. Katika hafla hiyo alikuwepo katibu wa ccm mkoa wa Arusha Marry Chatanda. Na matokeo yake mkoa wa Arusha haukuwa na kura za maruhani.

Acha propaganda aliyestoa ushauri kura zipigwe kimkoa ni Mkapa wala si mtu mwingine yeyote hata Kikwete kakiri hilo na Lowassa alisusia kukaa maeneo yaliyohifadhiwa mawaziri wakuu wa zamani yeye akasema atakaa eneo la watu wa mkoa wa Arusha kwa kujua kwamba wajumbe wa Arusha watakaa mbele kwa kufuata herufi lakini Mkapa kwa kumkomoa Lowassa na kiburi chake walipanga herufi za mwanzo kuanzia nyuma kuja mbele kwa maana nyingine mikoa ya Rukwa na Mwanza ndio ikawa mbele na Arusha na Dar ikawa nyuma hapo ndipo Lowassa alipigwa bao la kisigino na kuonekana kujikunyata kipole kama anaonewa
 
kwa taarifa ni kuwa baada ya kundi la Lowassa kupiga kampeni za kumkataa mwenyekiti na uvumi kuenea, Kikwete alikaa na Mkapa wakajadili na Mkapa akapendekeza kura zipigwe kwa mkoa ili wajue ni mkoa upi unaomkataa mwenyekiti baadae habari zikamfikia Lowassa ikabidi aitishe dinner na kuwaomba wajumbe wabadili msimamo kwani wangeumbuka. si kweli Lowassa ndii aliyebuni bali ni technics za Mkapa ndio ziliokoa jahazi
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom