Je, wajua nani aliyebuni kura za m/kiti wa CCM ktk mkutano mkuu Dodoma zipigwe kimkoa?

Kama demokrasia ya kweli ingechukua mkondo wake ndani ya uchaguzi wa ccm ,m/kiti wa kitaifa wa chama hicho asingepata kura alizopata.Kusema m/kiti alishinda kwa kishindo kwa mazingira ya uchaguzi ulivyofanyika ccm imeongeza udhaifu.Hakukuwa na haja ya kumbeba mtu eti kuwaaibisha maadui wa chama.Chama kilichokomaa kinakuwa tayari kumwondoa kiongozi ye yote aliye dhaifu.

CDM mbona hamtaki Mbowe apingwe kwenye uenyekiti? katika demokrasia ndogo hii ni hali ya kawaida ili kuleta stability na msukumo wa dira endelevu kwa muda unaokubalika kuliko kubadilisha sura za juu kila miaka 5. Mbona Bush 2004, na Obama 2012 walipita bila kupingwa ndani ya vyama vyao, unataka kusema kulikua hamna wa kuwapinga ndani au kila mtu alikubaliana na kazi waliyofanya? ukilaumu CCM na udhaifu wake angalia na vyama vingine au mifumo mingine inafanyaje kazi na ukimaliza hapo linganisha na mazingira yake kikazi ndiyo useme unachosema. itafika wakati ikitokea el nino mtasema ni udhaifu wa CCM na serikali yake.....wanaolalamika na kubeza bila kujiangalia wao ni watu dhaifu kupindukia
 
Sasa kulikuwa na haja gani ya kufanya uchaguzi wakati ilikuwa ni lazima kura iwe ya ndio?

uchaguzi ni muhimu kumpa mtu fresh mandate ya kuendelea kuongoza, kwa mbali mithili ya kurenew wedding vows baada ya miaka 10, 15 hivi ili kurefresh zaidi ndoa. nafikiri na CDM 2013 Mbowe atapitwa bila kupingwa lakini atapigiwa kura
 
hio inajulikana kwa wana ccm kwa kuwa na maamuzi ya kinafiki hata ktk mambo ya msingi, mnajitapa kashinda kwa kishindo kumbe mnapiga kura za kupanga
Wadau wa jf siku moja
kabla ya mkutano mkuu Dodoma, mh Lowassa aliwaita wajumbe wote wa mkoa
waArusha nyumbani kwake Dodoma ili kushiriki chakula cha jioni.

Baada ya hapo aliwaomba wajumbe wa mkoa wa Arusha woote kumpigia Jakaya
kura za ndiyo. Hii ni kutokana na habari zilizozagaa kuwa lowassa
anapiga kampeni ya kura za hapana kwa jakaya. Wajumbe walisimama
kuchangia mmoja mmoja huku wakilaani hao wanaovumisha kuwa mkoa wa
Arusha umejipanga kupiga kura za hapana kwa jk, walimuhakikishia mh
Lowassa kuwa hilo halipo na kura zote za ndiyo ni kwa jk.

Mjumbe mmoja alitoa ushauri kuwa ili mkoa wa Arusha usije ukachafuliwa
ni vyema kila mkoa ukapiga kura kwenye sanduku lake. Katika hafla hiyo
alikuwepo katibu wa ccm mkoa wa Arusha Marry Chatanda. Na matokeo yake
mkoa wa Arusha haukuwa na kura za maruhani.
 
Nape hakuungwa mkono na Mukama,Sasa subiri kiama cha EL mbele ya Kinana.Chezea JK wewe.

Lowassa ni rafiki mkubwa kupindukia wa Kinana hapo EL kalamba dume.

Baadhi ya biashara zao wameingia ubia chezea EL weee.

Kinana kuwa katibu Mkuu Urais kwa EL njia nyeupe.
 
Mhhhh!!! Siasa....???? kweli si kuwa ni kazi tu, bali ukiichezea inakuchomoa roho. sie wengine yetu macho. Ona wanavyohangaika ili tu kila mtu alinde kitumbua chake.
 
Wadau wa jf siku moja kabla ya mkutano mkuu Dodoma, mh Lowassa aliwaita wajumbe wote wa mkoa waArusha nyumbani kwake Dodoma ili kushiriki chakula cha jioni.

Baada ya hapo aliwaomba wajumbe wa mkoa wa Arusha woote kumpigia Jakaya kura za ndiyo. Hii ni kutokana na habari zilizozagaa kuwa lowassa anapiga kampeni ya kura za hapana kwa jakaya. Wajumbe walisimama kuchangia mmoja mmoja huku wakilaani hao wanaovumisha kuwa mkoa wa Arusha umejipanga kupiga kura za hapana kwa jk, walimuhakikishia mh Lowassa kuwa hilo halipo na kura zote za ndiyo ni kwa jk.

Mjumbe mmoja alitoa ushauri kuwa ili mkoa wa Arusha usije ukachafuliwa ni vyema kila mkoa ukapiga kura kwenye sanduku lake. Katika hafla hiyo alikuwepo katibu wa ccm mkoa wa Arusha Marry Chatanda. Na matokeo yake mkoa wa Arusha haukuwa na kura za maruhani.[/

Acha uongo wewe,EL hawezi shawishi JK apigiwe kura ya ndiyo,usimsafishe Laigwanani kupitia JF wewe,wasalimie MONDULI.
 
Wadau wa jf siku moja kabla ya mkutano mkuu Dodoma, mh Lowassa aliwaita wajumbe wote wa mkoa waArusha nyumbani kwake Dodoma ili kushiriki chakula cha jioni.

Baada ya hapo aliwaomba wajumbe wa mkoa wa Arusha woote kumpigia Jakaya kura za ndiyo. Hii ni kutokana na habari zilizozagaa kuwa lowassa anapiga kampeni ya kura za hapana kwa jakaya. Wajumbe walisimama kuchangia mmoja mmoja huku wakilaani hao wanaovumisha kuwa mkoa wa Arusha umejipanga kupiga kura za hapana kwa jk, walimuhakikishia mh Lowassa kuwa hilo halipo na kura zote za ndiyo ni kwa jk.

Mjumbe mmoja alitoa ushauri kuwa ili mkoa wa Arusha usije ukachafuliwa ni vyema kila mkoa ukapiga kura kwenye sanduku lake. Katika hafla hiyo alikuwepo katibu wa ccm mkoa wa Arusha Marry Chatanda. Na matokeo yake mkoa wa Arusha haukuwa na kura za maruhani.
Huko ni kujidanganya na kujipumbaza mwenyewe! Utake usitake hata ukiuosha vipi weusi wa mkaa ni asili yake! Mkishitukiwa kubalini yaishe badala ya kujishebedua kwa kudhani wengine ni mapunguani.
 
Back
Top Bottom