Je, wajua kuwa ulaya ipo mbali yetu kwa miaka zaidi ya 100?

Dec 1, 2018
11
45
Ukatae ukubali lakini ukweli utabaki kuwa Ulaya ipo mbele yetu kwa zaidi ya miaka elfu moja yaani zaidi ya karne.Nasema hivi kwasababu vitu tunavyoviona kama ujanja kwetu kwao vilikuwa vya kipumbavu karne moja iliyopita.

Mwaka 1844 mwandishi wa Norway aitwaye Henrick Ibsen aliandika kitabu kiitwacho AN ENEMY OF THE PEOPLE akimtumia Dr.Stockman kama muhusika mkuu na mtu aliyeitwa adui na watawala na wakapandikiza wananchi hivyo nao wananchi kwa upumbavu wao wakaamini hivyo ilhali Dr.Stockman alikuwa akipambana kwa kila hali aliyokuwa nayo kuwatetea wananchi ikiwa ni pamoja na kujitolea kama kafara bila kujali nafasi aliyokuwa nayo akitumia muda wake mwingi kuwaambia wananchi ukweli ambao kwa watawala ilikuwa ni uadui mkubwa na uhaini.Leo tupo karne ya 21 karne mbili baada ya kuandikwa kwa hichi kitabu lakini huku kwetu yaliyozungumzwa kwenye kitabu ndo yanatokea.

Watu wanaojitoa maisha yao kusema ukweli ambao haupingwi kwa hoja bali kwa bunduki na kuwekwa rumande wanaitwa maadui wa taifa na wananchi wanapandikizwa uongo huo nao bila kutumia macho yao na kama ikishindikana basi pua zao kunusa ukweli nao wanaamini hivyo.

Naweza nikasema kuwa kwa wakati wetu kwa sasa Tundu Lissu namfananisha kama Dr.Stockman maana historia yake tangu kabla ya kuwa mbunge na baada amekuwa ni mtu anayepambana bula woga kuwaambia wananchi ukweli na kuhakikisha haki inatendeka katika taifa.

Namfananisha na Dr.Stockman tena yeye ni zaidi maana Dr. Stockman alipigwa mawe kwa anili ya ukweli lakini yeye akapigwa risasi,Dr.Stockman alifutwa kazi lakini yeye hata kabla ya kufutwa ubunge washafuta mishahara yake wakati yupo wodini akiugulia operesheni ya 23 theatre.

Kila akipata nafasi ya kusema anatoa hoja nzito ambazo zinajibiwa na maneni ya kishenzi kama ombaomba,mzururaji,wakala wa mabeberu na hata kugika kiwango kikubwa cha kumuita haini.Cha kushangaza ni kuwa wananchi hawaoni wala hawapimi hoja ili kujua uongo na ukweli uko wapi ili kusimama upande wa ukweli bali wao wamekuwa washangiliaji tu wa viongizi wa vyama vyao wakijidanganya kuwa huo ndiyo uzalendo.

Ni kweli watazidi kumbeza sana kumtukana na kumyanyasa wanavyoweza maana Dr.Stocjman naye alifanyiwa hivyo lakini wachache wenye mwanga na upeo wa kuona tutasimama naye maana siyo kwamba hata wa huko upande wa pili hawaoni wanaona sana ila uoga umewatawala maana kuna kipindi mwaka 2016 kati ya wabunge ninaowaheshimu kwa utashi wao mkubwa wa kuelewa mambo,Mh.Hussein Bashe alisema kuwa amekuwa akifatilia nyaraka za Tundu Lissu kuhusu upoteaji wa rasilimali za taifa hata kabla hajawa mbunge na akasema kuwa ni nzuri lakini anabezwa kwa kuwa ni mpinzani.

Nimalizie kwa kusema kuwa Ulaya ipo mbele yetu kwa karne zaidi ya moja maana rafiki wa wananchi leo anaitwa adui wa wananchi ila ninukuu neno la mwisho la Dr.Stockman alilosema kuwa *the strongest man in the world is the one who stands alone* kwahiyo Lissu asihofu atajiona yupo mwwnyewe lakini na sisi wapenda haki tupo nae tutasimama naye hadi mwisho na hata wengine wanaoteswa magerezani hadi kunyimwa dhamana tupo nao maana tunatambua kuwa the guilty are afraid na kwa kuwa hawana namna tena ya kuongoza kwa haki watatumia vitisho vyote maana jeshi wanalo lakini sisi tuna haki na daima Mungu yupo na wenye haki hivyo atasimama nasi.Viva Lissu the enemy of the rulers but a friend to the oppressed.
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
45,747
2,000
Nilisoma kitabu jinsi mabadiliko ya Ulaya yalivyotokea. Waliamua kwanza kujenga barabara zote ziwe za lami. Wakulima wote waliweza kupeleka mazao sokoni na magari yalifika mpaka mashambani.

Elimu iliwasaidia kutambua haki zao. Waliweza ku lobby mpaka wakulima kupata ruzuku. Hata kama mwaka ilikuwa mbaya lakini waliweza kuishi.
 

Aiba

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
1,007
2,000
Nilisoma kitabu jinsi mabadiliko ya Ulaya yalivyotokea. Waliamua kwanza kujenga barabara zote ziwe za lami. Wakulima wote waliweza kupeleka mazao sokoni na magari yalifika mpaka mashambani.

Elimu iliwasaidia kutambua haki zao. Waliweza ku lobby mpaka wakulima kupata ruzuku. Hata kama mwaka ilikuwa mbaya lakini waliweza kuishi.
Serekali zetu za kiafrika zingeamua kufata sera za kiuchumi za ulaya za karne ya 19 tungepiga sana hatua kiuchumi kwa mwananchi mmoja mmoja tofauti na saivi wanafata sera za ulaya za karne ya 21wakati wao walishaendelea zaidi yetu kitambo sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
45,747
2,000
Serekali zetu za kiafrika zingeamua kufata sera za kiuchumi za ulaya za karne ya 19 tungepiga sana hatua kiuchumi kwa mwananchi mmoja mmoja tofauti na saivi wanafata sera za ulaya za karne ya 21wakati wao walishaendelea zaidi yetu kitambo sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Pia wananchi walipambana sana kupata haki sawa. Mwanzoni ni matajiri tu ndiyo waliruhusiwa kupiga kura, mwisho masikini waliruhusiwa kupiga kura ila ni wanaume tu. Ni miaka kama 100 iliyopita wanawake waliruhusiwa kupiga kura.
 

Stanley Mitchell II

JF-Expert Member
Jul 2, 2018
712
1,000
Acha masihara wewe. Miaka 100??

America ilifanya declaration ya Uhuru mwaka 1776, Maendeleo yaliyokua America mwaka 1776 sidhani kama Maendeleo yatayopatikana hapa Tanganyika kwa miaka 100 ijayo yatakuta zile levo zao za 1776.

Ukweli unauma.
 

Aiba

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
1,007
2,000
Pia wananchi walipambana sana kupata haki sawa. Mwanzoni ni matajiri tu ndiyo waliruhusiwa kupiga kura, mwisho masikini waliruhusiwa kupiga kura ila ni wanaume tu. Ni miaka kama 100 iliyopita wanawake waliruhusiwa kupiga kura.
Kwa Afrika hasa Tanzani ilo ni tofauti kwanza walidumaza elimu haikuwa kipaumbele kwa taifa kutoa elimu kwa wote saivi wameileta elimu kwa wote isiyo kuwa bora yani wanafanya ili waonekane kwa minajili ya kisiasa tuendako ni pagumu kuliko japo Tanzania kuna fursa nyingi za kazi ila tatizo elimu mbovu

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Aiba

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
1,007
2,000
Acha masihara wewe. Miaka 100??

America ilifanya declaration ya Uhuru mwaka 1776, Maendeleo yaliyokua America mwaka 1776 sidhani kama Maendeleo yatayopatikana hapa Tanganyika kwa miaka 100 ijayo yatakuta zile levo zao za 1776.

Ukweli unauma.
Marekani c ulaya broo angalia kilichoandikwa maendeleo ya hii dunia yameendelezwa kwa kiasi kikubwa na nchi za ulaya na ustaarabu wa hii dunia umetokea sana ulaya kuanzia kiutawala elimu hadi technolojia

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Stanley Mitchell II

JF-Expert Member
Jul 2, 2018
712
1,000
Marekani c ulaya broo angalia kilichoandikwa maendeleo ya hii dunia yameendelezwa kwa kiasi kikubwa na nchi za ulaya na ustaarabu wa hii dunia umetokea sana ulaya kuanzia kiutawala elimu hadi technolojia

Sent using Jamii Forums mobile app
Naona huelewi my point.

Nimechukulia mfano mzuri wa America ya 1776 ambayo ilikua under colonial settlers from Western and Southern Europe, all were Europeans. Sasa kama unashindwa kuelewa obvious fact kama hiyo basi sioni logic ya kua na matumizi na ww.

Unavosema Ulaya....Ulaya gani sasa mana kuna Ulaya Mashariki nayo ni Ulaya....vp maendeleo yao hao?
 

hearly

JF-Expert Member
Jun 19, 2014
38,812
2,000
Mkuu ulaya imetuacha mbali mnoo ni zaidi ya miaka 3000 ... kwa sababu mnamo mwaka 1642, ndio mwaka ambao Galileo aliofariki .... hapo ni baada ya kupatwa na misuko suko mingi ambayo ilikuwa imesababishwa na kanisa katoliki baada ya Galileo kuja na utafiti,uliokuwa unapinga utafiti wa awali wa kanisa katoliki uliokuwa unasema kuwa Jua ndio linalo zunguka Dunia ....

Lakini tangu karne ya 18 ni nadra kwa ulaya kusikia kuwa kuna matukio yenye mfanano na tukio la lissu au la Galileo

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom