Je, wajua haya yaendeleayo Korea kaskazini?

britanicca

Platinum Member
Joined
May 20, 2015
Posts
18,165
Reaction score
47,867
Kama nilivyoeleza awali, siku zangu ndani ya Korea ya kaskazini hazikuwa nyingi ni sita tu ila ndani ya kipindi hicho kifupi nimejionea mengi,

1. Wajua kuna watu wana miaka mpaka 30 hawajuji YouTube wala internet? Wapo wapo tu? Maana zinakatazwa,

2. Wajua ukigundualika unataka kwenda nje ya Korea kaskazini unapigwa risasi?

3. Asilimia 80 ya watu walioama north Korea wametoroka kupitia, bahari wakati wa usiku, pia milima ya mashariki kuingia nchi jirani,

4. Korea kaskazini imezungushiwa na ukuta wa umeme kwa maeneo karibu ya mpaka yote kuzuia wakorea kutoroka nchi yao,

5. Kumiliki smartphone Korea kaskazini ni kosa kubwa mno, unafanya uamasishaji wa vurugu kupitia mtandao, asilimia kubwa ya simu zinazoruhusiwa ni zile Siemens za zamani(mayai) Motorola ndogo na Philips,

6. Je wajua kwamba kwenda Korea kaskazini mpaka upite hapa urusi, au upite China kuna airlines moja tu ni KORYO

7. Kwa mwezi wanakufa takribani wakorea 100 kwa kunyongwa au kipigwa risasi hadharani,

8. Hauruhusiwi mkusanyiko wa watu wanaozidi kumi, usio rasmi, labda Ile shule au kanisa,

9. Wakorea wanaishi maisha mabaya mno ya kuomba omba na ni maskini wakati familia chache tu ndo ziko vizuri,

10. Bank account yako ikizidi kiwango ambacho Serikali imesema mtu anapaswa kuwa nacho,hela nyingine zinapelekwa Serikalini

Maajabu ni mengi kule
 
Porojo tu wewe pambana na hari yako hapa hapo bongo......sisi hatuna uhusiano wowote nao undugu au biashara nao...fanya utafiti wenye manufaa na uchumi wetu.....
 
Kama nilivyoeleza awali, siku zangu ndani ya Korea ya kaskazini hazikuwa nyingi ni sita tu ila ndani ya kipindi hicho kifupi nimejionea mengi,

1. Wajua kuna watu wana miaka mpaka 30 hawajuji YouTube wala internet? Wapo wapo tu? Maana zinakatazwa,

2. Wajua ukigundualika unataka kwenda nje ya Korea kaskazini unapigwa risasi?

3. Asilimia 80 ya watu walioama north Korea wametoroka kupitia, bahari wakati wa usiku, pia milima ya mashariki kuingia nchi jirani,

4. Korea kaskazini imezungushiwa na ukuta wa umeme kwa maeneo karibu ya mpaka yote kuzuia wakorea kutoroka nchi yao,

5. Kumiliki smartphone Korea kaskazini ni kosa kubwa mno, unafanya uamasishaji wa vurugu kupitia mtandao, asilimia kubwa ya simu zinazoruhusiwa ni zile Siemens za zamani(mayai) Motorola ndogo na Philips,

6. Je wajua kwamba kwenda Korea kaskazini mpaka upite hapa urusi, au upite China kuna airlines moja tu ni KORYO

7. Kwa mwezi wanakufa takribani wakorea 100 kwa kunyongwa au kipigwa risasi hadharani,

8. Hauruhusiwi mkusanyiko wa watu wanaozidi kumi, usio rasmi, labda Ile shule au kanisa,

9. Wakorea wanaishi maisha mabaya mno ya kuomba omba na ni maskini wakati familia chache tu ndo ziko vizuri,

10. Bank account yako ikizidi kiwango ambacho Serikali imesema mtu anapaswa kuwa nacho,hela nyingine zinapelekwa Serikalini

Maajabu ni mengi kule
Mkuu na wewe hapo kuna chumvi na ukweli umeeleze mkusanyiko labda kanisa lakini elewa North korea hamna makanisa, kingine huyu dogo ataelewa somo tu yaani mdogo mdogo ataachia kila kitu na watu wake watakuwa huru ndio vikwazo vitaondolewa moja kwa moja nawaambieni hili taifa linaenda kubadilika hamtoamini wait and see
 
watu 100 kwa mwezi unajua ukizidisha mara miez 12 utapata ngapi? mara miaka ambayo kim amekaa madarakani? nchi inhekua imesha isha
 
Namba 5,imekaa vibaya. Sasa ukimiliki smartphone unaonekana unachochea kwenye mitandao,je? Ni wakorea Gani watasoma uandikayo kwenye internet ikiwa waliowengi wanamiliki simu za torch.
Nalog off
 
Hizi article imejaa uongo mwingi kuliko ukweli, mtoa mada north korea wana smartphone zao na wanaoperate system zao za simu na kompyuta
Hii ni video toka north korea ikionyesha smartphone iliyitengenezwa humo nchini korea
 
Back
Top Bottom