KWEZISHO
JF-Expert Member
- Jan 29, 2016
- 7,519
- 6,511
Kwenye bandiko hili tulizungumzia Bunge letu kutoa azimio batili.
Kwanza azimio batili hilo lilisema Bunge halifanyi kazi na Ofisi ya CAG.
Tukasema humu Ofisi ya CAG ni Ofisi ambayo ipo kikatiba, Bunge halina mamlaka kuamua kuwa halifanyi kazi na Ofisi ya CAG, Bunge halina uwezo huo, hivyo azimio lile ni batili.
Ndipo Spika ili kulikingia kifua azimio batili hilo, Mhe. Spika, akatoa ufafanuzi wa kuondoa ubatili huo, kuwa Bunge sasa sio halitafanya kazi na Ofisi ya CAG, bali Bunge ni halitafanya kazi na CAG Prof Assad, hivyo halitapokea ripoti ya CAG yenye saini ya Prof Assad, ila ripoti hiyo ikisainiwa na mtu mwingine yoyote, itapokelewa.
Pia tukasema humu, hilo haliwezekani kwa sababu huwezi kumtenganisha CAG Prof Assad na Ofisi ya CAG.
Mwisho wa siku, Ripoti ya CAG yenye saini ya CAG Prof Assad ndio iliyowasilishwa Bungeni na kupokelewa rasmi hivyo kuthibisha rasmi ubatili wa azimio lile.
Leo nimemsikia Mhe. Spika akizungumzia kupokea ripoti ya ukaguzi wa Ofisi ya CAG.
P
Ukimsikiliza kwa makini utagundua kuna jambo analitafuta na majibu anataka yawe kama jinsi anavyotaka yawe.