Je, Wajua Bunge linaweza kutoa azimio batili? CAG yuko kikatiba. Je, Bunge lina uwezo kutopokea ripoti ya CAG?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
36,441
2,000
Wanabodi,

Hili ni bandiko la swali na alama za kuuliza nimeziweka, maana watu tusije itwa mahali kuhojiwa kuwa tumelidhalilisha Bunge.

Swali lenyewe ni hili,
Jee Wajua Bunge Linaweza Kutoa Azimio Batili?. CAG yuko Kikatiba, Jee Bunge Lina Uwezo Kutofanyakazi na CAG?. au kutopokea Ripoti ya CAG?.

Ukisikia ulevi wa madaraka sasa ndio huu. Hawa wabunge waliopitisha azimio hilo, wanakijua kitu kinachoitwa "The Constitutional mandates of the Controller and Auditor-General"?. Yaani mandate ya CAG iwekwe kwenye katiba yetu halafu waheshimiwa wabunge wetu walioapa kulinda katiba, wazuie jambo lililoelekezwa kikatiba?.
Constitutional Mandates
The Constitutional mandates of the Controller and Auditor-General shall be to- (a) authorize the use of money to be paid out of the Consolidated Fund upon being satisfied that Article 136 of the Constitution has been or shall be complied with; (b) ensure the money authorized to be charged on the Consolidated Fund or the money the use of which is authorized by law, have been spent for purposes connected and incurred in accordance with authorization; and (c) audit and report on the accounts, financial statements and financial management of –
(i) the Government of the United Republic, that is to say, Ministries, Independent Departments, Executive Agencies, Public Authorities and Other Bodies and Donor Funded Projects;
(ii) the local government authorities;
(iii) the Judiciary; and
(iv) the National Assembly.

Huu ulevi wa madaraka utatufikisha wapi?, walidhani nafasi ya CAG ni kama House Boy, House Girl or Shamba Boy, akija bosi mwingine hakupendi, unaambiwa fungasha ondoka.

Jee Waheshimiwa wabunge wetu walipokuwa wanapitisha azimio hilo, hivi wanazijua Powers of Controller and Auditor-General?. Ni kweli Serikali, Bunge na Mahakama, zote zina powers zake na independencis zake, but when it comes to public funds na ukaguzi, all the powera lies with CAG, kusema hufanyi kazi na CAG ni kumzuia CAG asitimize wahibu wake, Bunge linao uwezo huo?.

(1)In the performance of his functions and responsibilities, the Controller and Auditor-General may
(a) call upon any public officer for any explanation and information which the Controller and Auditor-General may require in order to enable him to perform those functions and responsibilities;
(b) summon and examine under oath any person as he may determine in connection with the receipt or expenditure of public monies or the receipt or issue of any public property affected by the provisions of this Act and in connection with any matter necessary for the proper performance of his functions;
(c) authorize any person eligible to be appointed as an auditor as the requirements of the Accountants and Auditors (Registration) Act, to conduct an inquiry, examination or audit on his behalf and that person or officer shall report to him;
(d) without payment of any fee, cause search to be made in and extracts to be taken from any book, document or record in any public office;
(e) seek the professional opinion or advice of the Attorney-General or any other qualified person on matters of a legal nature or of any qualified person on any accounting, auditing or other matter;
(f) accept as correct without further examination, or rely upon a certificate of any other person as hi thinks fit, on the accounts of any other person entrusted with the collection, receipt, custody, control or payment of public monies or public property or with the issue, sale, transfer or delivery of public property;
(g)from time to time acquire the services of any person as provided for under section 16 of this Act.

Hivi wabunge walipopitisha azimio hilo, jee walizingatia Ibara ya 143 ya Katiba inasema nini kuhusu The independence and status of the Office of the Controller and Auditor-General shall be as provided for under Article 143 of the Constitution?.
Tukisema azimio hili ni batili tutakuwa tumelionea Bunge?. Au Ubatili nao ni udhalilishaji?.

Tuliisha zungumza sana kuhusu kuhusu kitu kinachoitwa "The Principle of Separation of Powers, Checks and Balances" tukasema kanuni hii hutumika na mihimili hii mitatu ya dola kwa lengo kila mhimili kuwa a watchdogs wa mihimili mingine isijiinue kupita mamlaka yake.

Jee Azimio hili la Bunge kuamua halitafanya kazi na CAG ni Azimio Batili?, kwa sababu Ofisi ya CAG ipo kwa mujibu wa katiba, na Ripoti ya CAG inawasilishwa Bungeni kwa mujibu wa katiba, Jee Bunge lina uwezo huo wa kuamua kutofanya kazi na CAG, wakati Bunge sio Mamlaka ya nidhamu ya CAG, kama CAG amelikosea Bunge, then Bunge ama limshitaki CAG mahakamani au limshitaki CAG kwa mamlaka yake ya nidhamu, hiyo mamlaka ndio iamue kumchukulia CAG hatua za kinidhamu tena kwa mujibu wa Katiba lakini sio kwa Bunge kutoa Azimio Batili la altimatum kuilazimisha serikali kumuondoa CAG.

Bunge ni tukufu haliwezi kukosea, lakini linaongozwa na watu hivyo watu hawa wanaweza kukosea na ndio maana wakikosea, wanaweza kuondolewa.

Serikali inaongozwa na rais na pale Ikulu ni mahali patakatifu hivyo rais wetu anapaswa kuwa Mtakatifu ambaye hawezi kukosea na ndio maana rais hawezi kushitakiwa, ana kinga ya kutokushitakiwa kutokana na utakatifu huu, lakini rais pia ni binaadamu anaweza kufanya makosa ya kibinaadamu na anaweza asiwe Mtakatifu, ndio maana akikosea anaweza kushitakiwa na Bunge na akikutwa na hatia anaondolewa.

Ofisi ya CAG ni vivyo hivyo, ipo pale kwa mujibu wa katiba na CAG yupo kikatiba, Bunge haliwezi kujiamulia kuwa halifanyi kazi na CAG, bali kwa vile ofisi ya CAG nayo inaongozwa na mtu anayeitwa CAG, mtu huyu anaweza kukosea, akikosea anashitakiwa na akithibitishwa amekosea, anaondolewa.

Rais anapokea ripoti ya CAG kwa mujibu wa katiba, na mara tuu baada ya rais kupokea ripoti hiyo, ripoti hiyo ina change hands za kimamlaka, kutoka kuwa ni Ripoti ya CAG, na kugeuka kuwa ni Ripoti ya Rais kwa jina tuu la Ripoti ya CAG, ila bado inakuwa ni closed document, yaani ni ripoti ya siri.

Rais anatakiwa kuiwasilisha ripoti hiyo Bungeni within 7 days za mwanzo za kikao cha Bunge, baada ya rais kupokea ripoti hiyo na kama rais ataamua kuikalia ripoti hiyo bila kuiwasilisha with the 7 days, siku ya 7 CAG mwenyewe anatakiwa kuiwasilisha ripoti hiyo.

Ripoti hiyo ikiisha wasilishwa tuu Bungeni, mezani kwa Spika, from that moment, Ripoti hiyo inakuwa ni Public document, CAG anakuwa amemaliza kazi yake .

Sasa Bunge lijadili au lisijadili, it's up to Bunge na hapa ndipo kwenye udhaifu wenyewe wa Bunge letu.

Bunge halina mamlaka kukataa ripoti ya CAG bali lina uhuru lisiijadili, na likiikataa kweli, linapaswa kuvunjwa.

Hivyo kama CAG, ana makosa dawa sio kwa Bunge kuamua kutofanya kazi na CAG, kwa kutoa Azimio batili, bali kumshitaki, GAG aondolewe, maisha yaendelee.

Issue ya CAG ni issue nyeti ya kikatiba, nafasi ya CAG ni nafasi nyeti ya kikatiba, hadhi ya CAG kikatiba ni hadhi sawa na Jaji Mkuu, hivyo Bunge haliwezi kupitisha azimio lolote linakwenda kinyume cha katiba,

Kwa kumbukumbu yangu kupitia mafunzo ya sheria ya katiba tulivyofundishwa, Katiba ndio sheria mama, sheria nyingine yoyote inayokwenda kinyume cha katiba ni sheria batili, hivyo azimio lolote lililo kinyume cha katiba ni azimio batili.

Hivyo nahitimisha na lile swali kuu la msingi la bandiko hili
Jee Wajua Bunge Linaweza Kutoa Azimio Batili?. CAG yuko Kikatiba, Jee Bunge Lina Uwezo Kutofanyakazi na CAG?. au kutopokea Ripoti ya CAG?.

Paskali
Update,
Baada ya Ripoti ya CAG yenye sahihi ya CAG, Prof. Mussa Assad, kuwasilishwa Bungeni kwa mujibu wa Katiba. Uzi huu kuulizia kama Azimio lile la Bunge la kutokufanya kazi na CAG ni azimio halali au batili, limepatikana, ni azimio batili ndio maana limepuuzwa. Ufafanuzi wa Spika kuwa Bunge halitapokea Ripoti ya CAG kama imesainiwa na CAG mwenyewe Prof. Assad, ila itapokelewa kama itasainiwa na mtu mwingine pia ni batili, na imepuuzwa, Ripoti ya CAG iliyowasilishwa Bungeni imesainiwa na CAG, Prof. Assad,

Kiukweli kabisa, kuna mabandiko tunaweka humu JF, yanawasaidia sana watawala wetu, japo huwa hawasemi, ila tunapima kwa matokeo. Hivyo ndugu zangu wana jf, huu mjadala nimeufunga rasmi.
Hongera kwa Bunge letu kufuata Katiba.
P.
 

Gambino

JF-Expert Member
Aug 12, 2014
3,497
2,000
Bunge haliwezi kukataa kupokea ripoti ya CAG ila hawatataka ushirikiano nae.

Mara nyingi pale taarifa ya CAG inapopelekwa bungeni, baada ya kusomwa na kujadiliwa na wabunge, hua wataalam wa CAG wanaitwa mara kwa mara kwenda kuwafafanulia wabunge baadhi ya vitu wasivyo vielewa na mambo kama hayo. Hivyo kwa sasa ripoti ikisomwa bunge litatafta watu wengine wa kuja kuwasaidia kufanya nao kazi na sio CAG.

Pure hilarity.
 

Mmawia

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
92,125
2,000
Bunge haliwezi kukataa kupokea ripoti ya CAG ila hawatataka ushirikiano nae.

Mara nyingi pale taarifa ya CAG inapopelekwa bungeni, baada ya kusomwa na kujadiliwa na wabunge, hua wataalam wa CAG wanaitwa mara kwa mara kwenda kuwafafanulia wabunge baadhi ya vitu wasivyo vielewa na mambo kama hayo. Hivyo kwa sasa ripoti ikisomwa bunge litatafta watu wengine wa kuja kuwasaidia kufana nao kazi na sio CAG.

Pure hilarity.
Sasa wanamkomoa nani kama siyo kukaribisha ufisadi zaidi nchini maana taasisi sasa zitafanya zitakavyo bila kumuogopa CAG

In God we trust
 

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
23,743
2,000
Naona Bunge linachukua na nafasi ya mahakama.
Kingine linafanya kazi ya kumfurahisha mtu mmoja.

Hii nchi ukichukiwa na Rais automatiki umechukiwa na Bunge umechukiwa na Mahakama.

Katiba kwa sasa inafuatwa kutegemea hisia za Mkulu pale juu.
 

dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
12,317
2,000
Bunge haliwezi kukataa kupokea ripoti ya CAG ila hawatataka ushirikiano nae.

Mara nyingi pale taarifa ya CAG inapopelekwa bungeni, baada ya kusomwa na kujadiliwa na wabunge, hua wataalam wa CAG wanaitwa mara kwa mara kwenda kuwafafanulia wabunge baadhi ya vitu wasivyo vielewa na mambo kama hayo. Hivyo kwa sasa ripoti ikisomwa bunge litatafta watu wengine wa kuja kuwasaidia kufana nao kazi na sio CAG.

Pure hilarity.
... hivi azimio la Bunge leo ni kutofanya kazi na CAG au na Profesa Mussa Asad? Maana huu nao ni utata mwingine!
 

steveachi

JF-Expert Member
Nov 7, 2011
6,400
2,000
Hii habar nataman iishie humu humu bongo isifike nje ya nchi, wagogo na wasukuma mmejua kutuvua nguo asee. Wakenya watani zetu watatucheka sana. Siku Jaji mkuu akisema bunge ni dhaifu naona wabunge wetu watakataa kushtakiwa kwny mahakama za Tanzania

Sent using Jamii Forums mobile app
Aibu sana aisee,ndivyo watawala wetu wanavyotaka hivyo mkuu,nchi haiishi vituko kabisa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom