Sun is Sun
JF-Expert Member
- Mar 13, 2024
- 1,244
- 1,990
Habari zenu Ndugu zangu?
Kuna jambo huwa linanitatiza sana. Mtu anaweza kuwa na uwezo wa kumsaidia mwenzake anayepitia wakati mgumu, lakini akaamua kukaa kimya kana kwamba tatizo hilo halimhusu.
Mgonjwa anakosa matibabu, mtoto anakosa mahitaji muhimu, kijana anashindwa kusoma kwa kukosa ada, familia inakosa chakula, lakini wengine wanaona na kupita zao.
Cha kushangaza, wakati mwingine tunatumia pesa nyingi kwenye starehe, lakini tunashindwa kutoa hata msaada mdogo unaoweza kubadilisha maisha ya mtu.
Je, tatizo letu ni umaskini, au ni ubinafsi na kupotea kwa utamaduni wa kusaidiana?