Je utajuaje kama 'mpenzi' wako anafungulia nnje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je utajuaje kama 'mpenzi' wako anafungulia nnje?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Pape, Nov 15, 2009.

 1. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #1
  Nov 15, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Je utajuaje kama 'mpenzi' wako anafungulia nnje?
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Nov 15, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  utajua tu...
  1.atakuwa akitoka anajiremba kupita kawaida yake..
  2,usipo ingiza timu hakuulizi.
  3.kichen party zitaongezeka..
  4.ukimuudhi hakasiriki sana kama zamani.
  5.akirudi anaenda bafuni moja kwa moja.
  6.hakuchungi sana kama zamani.
  7.akipokea simu anatoka nje kwenda kuongea.

  yapo mengi.hayo ni machache..
   
 3. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #3
  Nov 15, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  thanks The Boss
   
 4. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #4
  Nov 15, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,386
  Likes Received: 5,670
  Trophy Points: 280
  Love is a Feeling, Marriage is a Covenant and a Relationship is Work!
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Nov 15, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,386
  Likes Received: 5,670
  Trophy Points: 280
  Mchumba asiye mwaminifu huwa mwenye ndoa asiyemwaminifu!

  [​IMG]Swali:
  Habari za kazi kaka naomba nisaidie naangamia kwa kuwa na mawazo yasiyo na msingi na kuumiza afya yangu, kweli nateseka mno.
  Mimi ni binti mwenye umri wa miaka 29, nilikuwa na relation ya kwanza ambayo ilidumu kwa miaka mitatu lakini kikubwa kilichotufanya tusaparete ni dini yeye muislam mie mkristu.
  But baada ya muda kupita nikapata mvulana mwingine kwa kweli nilifurahi toka siku ya kwanza kwa kuwa wote ni wakristu na nilimuona kwamba anampenda Mungu kwa matendo yake lakini kadri tulivyoendelea na relation nikagundua ana affair na wasichana wengine.

  Niligundua kupitia simu yake ya mkononi, nikamwambia na nikampa masharti kama ananipenda anipeleke kwao kunitambulisha na akafanya hivyo, haijapita mwezi bado anaendelea na hao wasichana wengine tena akiwa anakuja kwangu anawambia wasitume msg wala kupiga simu, lakini pia nimegundua ana relation mpya kaanzisha tena kwa mwanamke mwingine yani kichwa kinaniumwa!

  Maswali
  Je, Ni kweli mwanaume wa hivi anarekebishika kweli?
  Je, kwa nini anakuwa na wasichana tofauti tofauti?
  Na nikajaribu kupeleleza kwao nikaambiwa ni mimi peke yangu nilipelekwa kutambulishwa.
  Je, kweli anafaa kuwa mume?
  Maana sihitaji kuwa nabadilisha wanaume kila siku nahitaji kupata ushauri wa kuwa kama anabadilishika bora nitulie nae kuliko kufuata mwingine na kila siku kuwa na wanaume tofautitofauti.
  Kweli nampenda kwasababu familia yao ipo katika misingi ya dini imara.

  Nimeelemewa na mawazo.

  Ni mimi dada Yamenikuta.

  MAJIBU YA SWALI LAKO

  Pole sana dada Yamenikuta!

  Kama mmoja ya watu ambao hupokea maswali mengi yanayohusiana na ndoa na uchumba au mahusiano kwa ujumla, ukweli kumekuwa na mijadala mingi sana kuhusiana na suala la wanandoa kuoa wrong partner, na kinachoshangaza zaidi ni kwamba wengi wa hawa ambao wameoana na wanaume/wanawake wasiofaa wanakiri kwamba walikuwa wanajua na kufahamu fika kwamba wachumba zao walikuwa na tatizo hata kabla ya kuoana, kwa kuwa walikuwa wamependa (fall in love) au pendana kwa muda mrefu au muda wa kuoa ulikuwa umefika waliamua kwa hiari zao kuendelea na mahusiano wakitegemea kwamba siku moja watabadilika.

  Je, tunaweza kujifunza kitu gani kutoka kwa hawa watu?
  Hivyo basi dada Yamenikuta, ni jambo la busara na hekima kubwa kuwa makini na maamuzi unayofanya hasa baada ya kukutana na mwanaume ambaye ameshindwa kutembea katika ahadi kamili za msingi wa mahusiano yenu na kutegemea kuwa na ndoa yenye baraka.

  Usikubali kuoana naye kwa sababu eti unampenda sana na umekuwa naye kwa muda mrefu katika mahusiano kabla ya kuoana.
  Urefu wa mnahusiano kabla ya kuoana (uchumba) au wewe kumpenda na kujioana huwezi kuishi bila yeye hauna uhusiano wowote na afya ya ndoa yako baadae kama huyo mchumba wako ameshindwa kuwa mwaminifu kabla ya kuoana.
  Tabia alizonazo kabla ya kuoana haziwezi kubadilika ghafla baada ya kuoana.
  Mwanaume asiyemwaminifu kabla ya kuoana hatakuwa mwaminifu baada ya kuoana pia.
  Ndoa huwa haibadilishi mtu kiburi chake, hasira zake, umalaya wake, wizi wake, tabia zake chafu sana sana ndoa hufunua hizi tabia na kuziweka mezani uzione.

  Usijidanganye mwenyewe na kujipa moyo, utaangukia pua!

  Kile unachoona sasa ndicho utakachopata ukioana naye.

  Si kweli kwamba huyo mwanaume anampenda Mungu kwa matendo kama ulivyosema na sijajua ulitumie vigezo gani kwani kutembea na wanawake wengine ni uthibitisho kwamba dini yake ni ovyo.

  Pia yeye kukupeleka kwa wazazi wake (baada ya wewe kumlazimisha kama uthibitisho kwamba anakupenda) kukutambulisha si jambo kubwa sana ambalo linaweza kumfanya mwanaume mhuni asiwe mhuni bali ni taratibu tu za kuwaambia wazazi kwamba huyu ni mtarajiwa (siyo mke) hii ina maana hata kesho anaweza kuamka na kumtambulisha mwingine.

  Pia wazazi wake kuwa wanadini wazuri haina maana mtoto wao naye atakuwa na dini nzuri na kukuhakikishia maisha safi ya ndoa, hata hivyo dini nzuri kwa maana ipi ? kwenda kanisani au kuona wagonjwa au jinsi wanavyoishi?

  Ni kweli kama wewe upo makini na dini yako uamuzi wa kuchangua mume ambaye dini zinafanana ni wa busara sana unaweza kusoma hapa

  Sasa tuje kujibu maswali yako.
  Mwanaume wa aina hiyo huwa harekebiki na Mungu anakupenda sana kwamba amekuondoa kwenye shimo ambalo ungeingia kutoka ingekuwa kazi ya ziada, hivyo furahi na amini kwamba Mungu anaweza yote na shukuru kwa kukuonesha kwamba huyo mwanaume hafai.

  Ni ngumu sana kukubali kwamba mwanaume huyo hafai kwani inaonesha ulimkabithi moyo wako wote hata bila kuchunguza vizuri ni wapi moyo wako unaweka.

  Suala la kwa nini anakuwa na wasichana wengi naamini yeye ndiye anajua hata hivyo inaonesha kwamba hata kama anakupenda ana tabia mbaya ya uhuni kiasi kwamba hawezi kuwa na wewe tu bila hao wanawake wengine.

  Na je anafaa kuwa mume, ukweli ni kwama hafai na kimbia na mwogope (kama njaa) kwa maelezo zaidi kuhusu kujua anafaa au hafai au ni yeye au si yeye wa kuoana naye soma hapa

  Usijifariji kwamba eti afadhari ubaki naye yeye ili usionekane unabadilisha wanaume, ukweli huyo hafai na pia kama wewe umezoea kuwa na mwanaume na kumpa mwili wako ni kweli hisia zako zitakuwa zimeumia zaidi, wakati mwingine ukipata mchumba hakikisha humpi mwili wako kwanza hadi ndoa
   
 6. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #6
  Nov 15, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  asante mkuu
   
 7. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #7
  Nov 16, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...utapoamua kumchunguza, au uthibitika na dalili za UKIMWI. Ukisalimika, siku utayogundua DNA tofauti na yako...
   
 8. Papizo

  Papizo JF-Expert Member

  #8
  Nov 16, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 4,611
  Likes Received: 392
  Trophy Points: 180


  Thanks mtaalam nadhani umekamilisha!!
   
 9. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #9
  Nov 16, 2009
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  thx
   
 10. P

  Paullih Member

  #10
  Nov 16, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 85
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  The Boss,

  Hayo yote ni dalili tosha ya kuwa tunda linamegwa. Je, kama mimi ndo ninayechelewa kurudi kazini sikuzote kwa sababu ya majukumu, si ndo ntakuwa sijui kabisa kama mwenzangu anamegwa? mana sitamwona anapowahi kwenda kouga, simu hana haja ya kujificha, na labda mtakuwa nimejichokea na mzigo hivo hata mchezo simaindish sana... du, kazi kwelikweli.
   
 11. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #11
  Nov 16, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  the boss ya kweli hayo jamani ??
   
 12. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #12
  Nov 16, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Mzee ishakukmba NINI mbona kama mzoefu vile
   
 13. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #13
  Nov 16, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,392
  Likes Received: 672
  Trophy Points: 280
  Swahiba haya yote umejulia wapi?Au yalishakuathiri?
   
 14. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #14
  Nov 16, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,386
  Likes Received: 5,670
  Trophy Points: 280
  utajua tu...
  1.atakuwa akitoka anajiremba kupita kawaida yake..
  2,usipo ingiza timu hakuulizi.
  3.kichen party zitaongezeka..
  4.ukimuudhi hakasiriki sana kama zamani.
  5.akirudi anaenda bafuni moja kwa moja.
  6.hakuchungi sana kama zamani.
  7.akipokea simu anatoka nje kwenda kuongea.

  yapo mengi.hayo ni machache..

  HIYO RED INABID AKIPITA MBELE YAKO SWAIBA KUELEKEA BAFUNI AKITOKA UNAPIGA ASTKAFFULILLAH....HAPO AAAAHHH VINGINEVO NA WEWE UNAKUWA NA LILE....
   
 15. Juma Contena

  Juma Contena JF-Expert Member

  #15
  Nov 16, 2009
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 1,195
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  We mama mia umetoka kuzusha jukwaa la siasa sasa umekimbilia huku mada yako kule aindeleze nani?
   
 16. V2d

  V2d JF-Expert Member

  #16
  Aug 5, 2011
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 212
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Matendo yake lazima utagundua 2
   
 17. Mtalingolo

  Mtalingolo JF-Expert Member

  #17
  Aug 5, 2011
  Joined: Aug 4, 2011
  Messages: 2,188
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mmh napata somo hapa maana mapenzi hayana muamana kweli.
   
 18. M

  Mwanaweja JF-Expert Member

  #18
  Aug 9, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 3,576
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  mkuu hapo wala hakuna ubishi ni dalili tosha kabisa maana wengine wanadanganyika sana
   
 19. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #19
  Aug 9, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  8. Kuchati na simu muda mwingi ukiikagua utakuta msg zote zinapokelewa na kuwa deleted on the sport
  9. Kuweka simu mbali nawe... hatoruhusu umpokelee simu yake hata akienda WR atakuwa nayo.
   
Loading...