Je, ungependa kusoma nje (US & Canada) kwa ngazi ya Masters na PhD with 100% funding? Basi hii thread inakuhusu

babuazaboy

Member
Apr 17, 2021
8
4
Hii thread ni kwa ajili ya wana chuo au watu waliomaliza chuo kabisa na wenye ndoto ya kwenda kujiendeleza kimasomo kwa Masters na PhD.

Naandika huu uzi kutokana na my personal experience.

1. Rejea kichwa cha habari, nimeandika 100% FUNDING sijasema 100% SCHOLARSHIP. In short kwa US na Canada scholarships za kusoma MS na PhD ni chache mno na ngumu kupata. Watu wengi wanaondoka kusoma huwa wanapata funding. Je tofauti ya scholarship na funding ni ipi? Scholarship ni free money that you don't have to payback ambayo ni tafauti sana na funding. Funding mara nyingi ni wanaita ASSISTANTSHIP ambapo unapewa kazi ya kufanya na chuo (mfano wa kazi ni grading, teaching, tutoring and researching ). So 100% FUNDING means unalipiwa ada + unalipwa salary kila mwezi kwa kazi unazofanya.

2. Amua unataka kusoma kitu gani (mfano. PhD in Civil engineering) then fanya research by googling unachokata kusoma na upate vyuo wanavotoa hio kozi. Kwenye website ya kila chuo kuna page ya Funding na admission requirements. Soma vizuri hizi page mbili.

3. Itabidi ufanye pepa za GRE Math and English) na pepa ya TOEFL (English tupu). Pia uwe na PDF za transcript yenye GPA nzuri kidogo.

4. Vyuo vingi wanahitaji three or four recommendation letters.

5. Vyuo vingi kwenye during online application watakuuliza if you want to be considered for assistantship. Select YES.

Wenye maswali karibuni.
 
Na je aliyesoma bachelor degree in geography and environmental studies anaweza kupata scholarship au funding akisomea masters?

MÊmENtO HoMO
 
Na je aliyesoma bachelor degree in geography and environmental studies anaweza kupata scholarship au funding akisomea masters?

MÊmENtO HoMO
Ishi ni kufanya research ya uhakika kabla ya kuapply. Unasoma Bachelor ya geograpgt and environmental, je kwa Masters unataka kusomea nini?
 
Ishi ni kufanya research ya uhakika kabla ya kuapply. Unasoma Bachelor ya geograpgt and environmental, je kwa Masters unataka kusomea nini?
mm nimesoma Bsc agronomy, masters nilitaka kusoma Crop science but GPA Nina 3.6, so nahis fursa imenitupa mkono.
 
Umejiuliza kwanini hawatoi nafasi nyingi za Masters degrees na PHD degrees kwenye fani hizi kwetu; Mechanical Engineering, Design Engineering, Process Engineering, Manufacturing Engineering, Plant construction Engineering? Kwanini mara nyingi ni Civil Engineering tuu?
 
Mfano nimegoogle Iowa state university nimepata links hizi hapa


 
Hiinya full funding tamu sana aisee, ahsante sana kwa uzi wako
 
Nilivyoliona jina lako nikakumbuka necta form six , nikamkumbuka Na logboy
 
Habari Kaka naomba unielekeze napenda kusomea MD nje ya nchi
 
Kama ndio kwanza unaanza, wewe ndio una mda mzuri wa kujiandaa ukiwa chuo. Unaweza kujiwekea plan mapema na kujua unataka kufanya/kusoma nini ukishamaliza chuo. Unatarajia kusoma kozi gani?
Nataka kijana wangu, nitakutafuta kaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…