ShalomP
Member
- Jun 14, 2019
- 97
- 154
Leo majira ya jioni ilikuwa mida ya saa moja kasoro, nilikuwa nimetoka zangu mazoezini. Wakati natembea nikamkuta kijana mmoja amemshika binti wa kike msichana kwa makadilio umri chini ya miaka 18 alikuwa anachuma fimbo ili kumuadhibu. Huyo kijana nimpe jina fake la Mike na binti nimpe jina fake la Mary Hawa ni ndugu kaka na dada.
Sasa Mike alimkuta huyu dada ake Mary yupo na rafiki ake wa kiume( boyfriend) nimpe jina fake la Kenny, Sasa Mike akapanic kwa mazingira aliyomkuta dada ake Mary wakiwa na Kenny wanatembea pamoja huku ikionesha kuwa wana mahusiano ya kimapenzi. Hasira zikampanda Mike akamshika dada ake na kumkunja huku akiandaa fimbo ya kumpigia Basi Kenny akawa anamwambia Mike kaka mtu amwachie Mary. Mike akawa anatamka maneno kwa jazba anamwambia Mary hapa ndio Nyumbani, badala kujisomea wewe upo na kimwanaume chako kinakulaghai ambaye ni Kenny Sasa dada Mary Leo lazima nikupe kichapo. Mimi nilikiwa napita sikutaka kuingilia ugomvi usionihusu maana wahenga wanasema ya Ngoswe muachie Ngoswe, mi nikaendelea na safari kabla sijafika mbali nikakuta wanaanza kupigana.
Yaani Mike akawa anampiga dada ake Mary na kumrukia kichwa Kama vile anapigana na mwanaume mwenzake na kusababisha prova na shati alilovaa Mary kuvulika ikabidi Kenny mshikaji wa Mary aanze kupigana na Mike Ili kumnusuru Mary ugomvi ukawa mkubwa, Ikabidi niahirishe safari niingie kusuruhisha ugomvi na kuwaamua kwa kuwa nilikuwa nimetoka zoezi nikaamua ugomvi lakini Mike kaka mtu alikuwa bado ana hasira.
Wananzengo wakawa tayari wamefika nikamsihi Mike haipasi kumdharirisha dada ake kiasi ingempasa akamuadhibu nyumbani. Mary na Kenny wakafanikiwa kukimbia lakini Mike akaapia kwamba dada atakapofika nyumbani atamuadhibu Tena Sasa sijajua kwao kilichoendelea binti mwenyewe inavyoonesha ni mwanafunzi.
Mtazamo wangu ni maombi yangu shule zifunguliwe mapema maana Hawa vipepeo wanafunzi wa kike wamejisahau Sana wanajiachia Sana humu mitaani. Pia Kama ni Kaka umemkuta sehemu dada ako mwanafunzi yupo sehemu sio sahihi chuma fimbo kamuadhibu nyumbani au ikiwezekana mpe elimu ya jinsia Ikiambatana na ushauri nasaha mana Kaka mtu anaweza ukatolewa meno Kuna vijana wamevurugwa kusema Kweli kumchunga mtoto wa kike ni kazi Sana, maana wao wenyewe hawasikii.Wakaka wengi akikuta mtu ambaye yupo na dada ake kamzidi nguvu hasira anakimbilia kumuadhibu dada ambaye kwake anaona ni dhaifu Kama ni vitasa wale wote wa kiume na wakike.
Elimu inahitajika Tena Sana kwa Hawa mabinti wa kike pesa zitusumbue na Hawa Tena tuanze kuwachunga daaah ni heri shule zifunguliwe wakakae mabwenini uko. Wazazi, Walimu na Walezi msijisahau waelimisheni sana hao matineja vipepeo wapeni elimu jinsia ya kuvishinda vishawishi ili wawe na tabia shupavu na wajifunze kusema hapana sio kila kitu ndiyo. Ujumbe wenu vipepeo wote Nukuu "Kila Jambo na wakati wake, Kuna wakati wa kupanda na wakati wa kuvuna, chochote ukipandacho mtu ndicho utakachovuna, ukipanda ngano utavuna ngano na ukipanda magugu utavuna magugu."True story majina nimetumia fake.
matusi, Mambo ya siasa na maneno makali hayaruhusiwi kwenye comment. Changia kwa mtazamo chanya na makini.