Je, ungekuwa wewe ungefanyeje?

kichwa kikubwa

JF-Expert Member
Sep 24, 2013
2,275
1,698
Mambo zenu.
Haya sasa toa maoni yako hapa.
Wewe ni mwanachuo wa chuo x. Unafahamiana na binti mmoja wa chuo hicho hicho (chuo x), kwa bahati nzuri wote mnajikuta mko program moja (tuchukulie B.arts with education). Mara unajikuta umependezwa na huyo binti ktk mahusiano, unadhamiria kuja kumtokea. Na kweli unatimiza ndoto yako ya kumfunulia lililo moyoni mwako na si tu mahusiano ya kuishia njiani......... Lakini yeye binafsi (binti) anachomoa kwamba anamtu wake, Basi fresh.
Lakini kadri Siku zinavyozidi kwenda unagundua binti anajaribu kujiweka karibu kwako kwa kila mbwembwe baada ya kuona umempotezea (kisa kakutosa); na wewe bila hajizi unakuwa unajaribu kuendelea kumchombeza kuonyesha kwamba hujakata tamaa kwake, lakini unakuta bado anaendelea kukutosa. Na cha ajabu ukimsusa kabisa basi yeye ndiyo atazidisha mbwembwe za kutaka uendelee kumsumbua kumtongoza tongoza, alafu na yeye aendelee kukutosa.
Wewe unaona kama ni utoto vile, mnaingia mwaka wa pili (toka mwaka wa kwanza ulivyorusha mistari) unachukua maamuzi magumu ya kukata mawasiliano naye kabisa hata kwa mbwembwe zipi...... Baada ya yeye binti kugundua sasa ndo umemsusa jumla na huku akiendelea kukumbuka maneno kuntu uliyokuwa unampa kipindi unamfukuzia, mnapofika mwaka wa tatu semester ya mwisho anakufuata yeye mwenyewe na kukufunulia kisa cha kukusumbua, anakwambia;
"Samahani kaka, niliguswa na maneno yako kipindi kile unanitongoza, lakini nilishindwa kukumbia ukweli ulio dhahiri. Ni kwamba kipindi kile nilikuwa nachukuliwa/ natembea na lecture wa kozi flani hivi, sasa niliogopa kukubalia moja kwa moja kwa kuwa niliogopa kukusababishia matatizo wewe binafsi na Mimi pia (huyo lecture alikuwa ananisaidia sana, hata kwenye masuala ya kitaaluma). Na ndiyo maana nilikuwa nakusumbua makusudi ili mwisho wa siku nakuja kukubalia wewe baada ya kuachana naye. Na nakuhakikishia saizi nimeachana (lecture) naye, niko huru; ambapo hakutakuwa na tatizo lolote lile kwako na kwangu".
Sasa je; baada ya binti kukueleza ukweli:
A. Utakubaliana naye kwamba wewe (mwanaume) sasa kwa Raha zako ni ruksa kujinafasi kwa kuwa ameachana na lecture?
B. Utamuacha kama alivyo kwa kuwa huna imani naye kama kweli ameachana na lecture?
C. Utamshukuru kwa akili yake aliyoitumia kukunusuru wewe na kisha kumtaka muwe kama kaka na Dada?
D. Utamlaumu kwa kutokuwa muwazi toka mara ya kwanza?
E. Au uta...........?

Toa maoni yako, ungefanyeje?
 
nenda straight to the point.. NAKUPENDA au SIKUPENDI basi hayo ndio majibu sio eti ooh subiria mara nna mtu wangu mara imepanda imeshukA..inaboa
Haraka haraka haina baraka, na tukikubali haraka mnatuita malaya,
 
Mimi ningejibu C,kwa wanaume walio wengi hata km ulikuwa na mtu wako huwa hawapendi kumjua.pili wakimjua kunavitu anapunguza kwa huyo dada au mchumba km uaminifu,imani na anaweza hata kumuacha
 
Mkuu ogopa sana Mwanamke anayekuambia nilikuwa na mtu X ila nimeachana naye ila sasa tulisongeshe... Mbele ya safari hashindwi kutoka na mwingine kisha akaja kukuambi nilimpa kimoja tu.. Sina mpango naye.. Bora anauekaa kimy na kuyamaliza mambo yake kimya kimya
 
Mimi ningejibu C,kwa wanaume walio wengi hata km ulikuwa na mtu wako huwa hawapendi kumjua.pili wakimjua kunavitu anapunguza kwa huyo dada au mchumba km uaminifu,imani na anaweza hata kumuacha
Vip, lakini anasema amekwisha Achana na lecture sasa yuko huru/free.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom