Je unaweza kusoma vyuo vya Tanzania bila kudesa?

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,517
21,996
Habari;
(Kudesa;chabo,juche,nondo) kwa wale wasioelewa, ni ile hali ya mwanafunzi kuibia/Kuigilizia katika mtihani,test au assignment; SASA
Naomba kuuliza maswali haya;
a). hivi na ulaya kuna kuigilizia, chabo, desa, juche, nondo,mzigo au kujilipua kama wafanyavyo wanafuzi wa bongo katika mtihani?
b). Je elimu ya bongo ni rafiki kwa wanafunzi kumaliza vyuo pasipo hata siku moja kuibia?
maana nimesikia watu wanasema huwezi maliza chuo bongo bila kula chabo hata siku moja, ukikosa kwenye mtihani/Test basi kwenye Assignment, ukikosa kwenye assignment basi kwenye project n.k Je ni kweli ? Je vipanga na mabest student wa hapa bongo ni sawa sawa na wa ulaya? naomba majibu.
 
Mmmh! Kina aristotle wenyewe walipiga chabo sembuse miye? Kisa cha kusup?! Teh! Nikipata upenyo naibaaaaa!! ajira zenyewe ngumu na cheti nipate zero akati mbele kakaa kipanga!? Teh teh teh teh teh! Hii ndo bongo yani kibongobongo unaiba hadi jina la mwenzio! Teh teh teh teh teh!
 
Ila assigment automatically huwa ni chabo tu! Unachofanya unabadili mpangilio tu na kuongeza au kupunguza vitu. Ila usiombe ukamatwe na chabo kwe mtihani!
 
chabo lazima,yani wewe unajua kias gani mpaka usiangalie wenzako wamefanya nini? hasahasa kwenye assignment lazma watu muangaliziane mmefanana nn na mmetofautiana nini kisha mnaexchange.plagiarism...nayo ni chabo na hii ndo very common kwenye vyuo vyetu,mtu unapewa swali unaliandika lote kwenye search bar ya google bas linakuja na solution yake unaikopi unapata swali lote haha.
 
Ila assigment automatically huwa ni chabo tu! Unachofanya unabadili mpangilio tu na kuongeza au kupunguza vitu. Ila usiombe ukamatwe na chabo kwe mtihani!

We ni mzoefu wa chabo. Kwa miaka 23 niliokaa darasani nijawahi kupiga chabo.
 
Supplementaries za French Kila kukicha pia ilinibidi nitumie Mbinu mbadala kukariri plus Chabo Sana kutoka kwa Mafundi mi nikiwa nimekaa katikati full zoomin Hv unaijua supp au Carry vzr wewe.
 
Bongo chabo kawaida sana ila kwa nchi nilosoma na kozi nillsoma chabo haipo 98%. Kwanza hakuna mtihani hata 1, (sijawah fanya test wala pepa), mwendo ni assignments tu na lazima iingizww kwenye plagiarism checker, ukiwa na 20% sio mbaya but ikikamatama 50% matching na kazi ya mtu mwingine au kitabu unapewa ziro
 
Ndo maana hatuna waandishi mahiri, tuna maprofesor kibao lakini nothing to show off. Vitabu vingi tunavyotumia leo hii huko mashuleni na vyuoni vimetoka ulaya na marekani na vimeandikwa na watu wenye level za kawaida kabisa za elimu. Tatizo la nchi zetu tunaheshimu sana cheti kuliko ubunifu na utendaji kazi wa mtu husika .
 
Back
Top Bottom