Blue Bahari
JF-Expert Member
- Aug 21, 2016
- 1,232
- 1,146
Mambo vipi wanajamvi!
Nakuja na mada yangu inayohusu kumlipia mahari baba yako pale ambapo hali yake kiuchumi si nzuri. Umeshawahi lifikiria suala hili? Twende pamoja!
Iko hivi, baba na mama yako walioana miaka mingi iliyopita bila ya hata baba yako kumalizia mahari ukweni. Ahadi ya baba mzazi kwa wakwe ni kuja kumalizia taratibu huku wakiwa wanaendelea kuishi na mkewe (mama mzazi).
Wakwe wanamkubalia baba kuishi na mkewe kwa kuwa tayari amekwishalipa sehemu ya mahari. Kwahiyo, wakwe wanaamini kwamba baba angelimalizia mahari siku zijazo kwa kuwa tu uchumi ni mgumu kwake. Maisha yanaanza kati ya baba na mama; unazaliwa wewe na wadogo zako kadhaa lakini mahari bado haijakamilishwa.
Mnakuzwa na kulelewa kiugumu ugumu hivyo huku mahari bado hajikamilishwa. Watoto mnakuwa wakubwa na kuanza shule, kisha kumaliza shule kwa ngazi ya msingi, sekondari, na pengine vyuo huku baba bado mahari hajakamilisha.
Watoto mnaanza kujitegemea kimaisha na pengine Mungu amewajalia hali nzuri kiasi ya maisha bora, lakini baba mzazi bado hajakamilisha mahari. Kumbuka kwamba, ninyi watoto tangu kuzaliwa na kukua kwenu, hamkuwahi kuambiwa na wazazi wenu suala la ukamilishaji wa mahari; yaani si baba wala mama mzazi ambaye amewahi kuwatamkia kwamba "Baba yenu hajakamilisha mahari".
Baada ya ninyi watoto kuanza kujitegemea, na Mungu kuwainua kiuchumi kwa kiasi chake, siku moja baba na mama wanakorofishana na hatimaye mama mzazi anaamua kurudi kwao (ukweni kwa baba mzazi). Ndugu wa mama wanamjia juu baba kwa unyama wa kipigo aliyomfanyia mama. Baba anaomba msamaha na kuomba/kuhitaji mkewe arudi nyumbani ili maisha yaendelee.
Ndipo ndugu wa mama wanafungua faili la madai na kukuta baba hakumaliza mahari ya mkewe; ndugu wanatoa sharti kwamba ili mkewe arudi, lazima kwanza mahari ikamilishwe, la sivyo mkewe hawezi kurudi na ataendelea kuishi ukweni kwa muda wote mpaka pale mahari itakapokamilishwa.
Baada ya baba kupewa sharti hilo, hali inakuwa ngumu kwake kutimiza takwa hilo kwa muda wa haraka. Mkewe anamuhitaji, kaomba msamaha wa kadhia ya kipigo alichompa mkewe, mkewe na ndugu zake wanaupokea msamaha, lakini, changamoto ni mahari bado hajakamilisha.
Sasa je, afanyeje ili kumkomboa mkewe? Pesa ya haraka hana, hata kama atadunduliza kwa muda wa miezi sita hawezi kufikia kiwango cha mahari alichobakiza. Hii ni kwasababu kazi anayofanya baba ni yenye kipato duni sana. Ndipo wazo linamjia baba kwamba msaada pekee wa kumkomboa mkewe ni kutoka kwa watoto.
Baba anakuja kwako kukueleza tukio zima la kukorofishana na mama yako, na pia sharti alilopewa la kumkomboa mkewe. Kisha baba anakuomba msaada wa pesa iliyobakia ya mahari ili akalipe kwaajili ya kumkomboa mkewe. Wewe binafsi unatahamaki kusikia baba hakuwahi kumaliza mahari, ndipo siku hiyo unajulishwa ili umsaidie kiasi hicho cha pesa akamalizie.
Wewe kama mtoto uwezo kiuchumi siyo mbaya sana, hali ya kiuchumi inakuruhusu kumsaidia kiasi cha mahari kilichobaki. Swali ni je, utakuwa tayari kumsaidia baba yako kiasi hicho cha mahari kilichobaki ili akamkomboe mama yako na kisha maisha yaendelee?
Karibu kwa mjadala.