Naomba kuuliza:
Huu mti unaitwaje?
Wauzaji wa miti (wa kibongo bongo) wananiambia kwa kutamka maneno kama vile Akaria, Alcaria, Arcadia .... nimejaribu ku-google Arcadia na Arcaria inatokea miti mingine kabisa.
Richard Mbale
Kuna siku nilikuwa natafuta mti ambao huwa una maua yanayonukia sana pamoja na majani yake pia, unaitwa Cananga odorata au ylang ylang (kwa jina la watu wa Far East).
Sasa nilishangaa nilipoambiwa unaitwa "mlangelange".
Walivyoniambia: Unatafuta "mlangelange"?
Nikawaambia: Nadhani itakuwa huo.
Nilipouangalia nikajua nd'o wenyewe "mlangelange" = ylang ylang
Sehemu nyingine tena nikauliza miti inayonukia kama wanayo.
Nikaambiwa: Kuna "muasumini"
Nilivyokuja kuuangalia nikakuta ni "jasmine"
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.