Je, unasumbuliwa na Kisukari na unapenda kujitibu mwenyewe kwa lishe? Majibu haya hapa...

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Salama wadau, nimekutana sehemu na hili andiko la ndugu yetu, nadhani linaweza kusaidia jamii, wale wenye Kisukari na ambao hawana kwa lengo la kujilinda

--------------------

JE UNASUMBULIWA NA KISUKARI NA UNAPENDA KUJITIBU MWENYEWE KWA LISHE?

Katika miaka ya karibu kumekuwa na ongezeko kubwa sana la wagonjwa wa kisukari na wengi wao wamepoteza maisha yao au kulipa gharama kubwa za matibabu na kuishi maisha ya unyonge na ya kujijutia na kulaumu “kwa nini mimi”.

Hayo yametokea wakati kuna tiba-lishe ambayo mtu yeyote akitumia na kuizingatia, ugonjwa huo utakuwa si kitu cha kutisha na wengi watarudia maisha yao ya kawaida.

Lishe hiyo ni vyakula ambavyo ni vya kawaida na vinapatikana kwa urahisi kikubwa ni kuwa na nidhamu ya kuvitumia kila siku. Kama wewe au ndugu, rafiki au mzazi wako wako anasumbuliwa na kisukari au unapenda kisukari kisikupate basi kila siku asubuhi hakikisha unaanza kwa kula kwa pamoja (kachumbari) ya:

1. Karoti ndogo moja au nusu kama ni kubwa;s
2. Tango dogo;
3. Kitunguu-maji kimoja;
4. Hoho moja;
5. Nyanya moja; na
6. Limau pamoja na maganda na mbegu zake.

Waweza kusaga kwa njia ya blender na kunywa asubuhi kama kinywaji cha kwanza. Ukila au kunywa subiri hadi dakika 45 au saa nzima kabla ya kula chakula kingine. Zingatia kupunguza vyakula vya wanga kama ugali na wali katika mlo wako. Wengi ambao wanatumia lishe hii wamepata nafuu kwa haraka na wanasikitika kwa kuchelewa kuipata elimu hii na gharama kubwa sana walizoingia kujitibu na wengine kupoteza sehemu za viungo vyao.

NB: Kwa kuwa vyakula kama nyanya, hoho, na tango vinapuliziwa dawa ni vema kuvisafisha vizuri kwa maji-tiririka na kama inawezekana nunua na jipatie nyanya, tango, na hoho ambazo zinalimwa kwa kilimo-hai yaani kilimo ambacho hakitumii dawa za kuua wadudu.

Aidha waweze kupata elimu ya lishe bora kutoka kwa Dr. Boaz Mkumbo ambaye ameandika kitabu cha “Sayansi ya Mapishi”

BURE”. NAWATAKIA LISHE NJEMA.
 
Hapo kwenye limao pamoja na maganda yake na mbegu zake fafanua kidogo mkuu manake maganda ya limao ya ya nje ni machungu sana
 
Imekaa vizuri, sio gharama kubwa inawezekana kwa kila mtu.
Thanks
 
Back
Top Bottom