Je, Unamwona Yesu Kama Nani Kwako?

Je, Unamwona Yesu Kama Nani Kwako?

Namwona kama nabii na mitume wengine wa kabla na baada yake, si mwana wa Mungu na wala si Mungu kama yeye mwenyewe asemavyo.
Siyo kitu cha kushangaza kwa wewe kutojua Yesu ni nani. Hata wakati akiwa Duniani, Yesu aliwajaribu mitume wake kutaka kujua kama hekima na akili ya kibinadamu ingewafanya wamfahamu YEYE ni nani. Wote walishindwa kujua YEYE ni nani. Ni mtume Petro pekee ndiye aliweza kujibu kuwa Yesu ni nani, na Yesu mwenyewe akamwambia Petro kuwa hakumjua kwa sababu ya akili yake bali Baba wa Mbinguni ndiye aliyemfunulia. Hivyo wewe kutomjua Yesu ni nani, si jambo la ajabu. Halikadhalika, wale wanaomjua kwa uhakika Yesu ni nani, siyo kwa sababu ya werevu wao. Uhakika wa hayo unayapata katika mafungu haya:

​

MAthayo 16: 14-18​

Basi Yesu alipofika katika wilaya ya Kaisaria, aliwauliza wanafunzi wake, “Watu husema mimi ni nani?” Wakamjibu, “Baadhi husema ni Yohana Mbatizaji, wengine husema ni Eliya; na wengine husema kwamba ni Yeremia au mmojawapo wa manabii.” ;Akawauliza, “Na ninyi je, mnasema mimi ni nani? 16;Simoni Petro akamjibu, “Wewe ndiye Kristo, Mwana wa Mungu aliye hai.”Na Yesu akamwambia, “Umebarikiwa, Simoni mwana wa Yona, kwa maana si mwanadamu aliyekufunulia hili, bali ni Baba yangu aliye mbinguni. 18;“Nami nakuambia, wewe ni Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu ambalo hata nguvu za kuzimu haziwezi kulishinda.

1Wakorinto12:14
Wala hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu.

Hivyo, omba Roho Mtakatifu, Roho wa Bwana ili umjue Yesu Kristo ni nani.

Tazama vitabu vyote, kuanzia Agano la kale mpaka Agano Jipya, hakuna hata sehemu moja ambapo Yesu alitajwa kama nabii, ila kuna maandiko mengi ya manabii, yenye unabii juu ya Yesu Kristo. Manabii wakubwa kama Isaya na Yohana mbatizaji, walitoa unabii juu ya Yesu:

Isaya 9:6​

Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto wa kiume; Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake, Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani.
 
Back
Top Bottom