Je unakumbuka vibano na adhabu za shuleni??

Je unakumbuka vibano na adhabu za shuleni??

MaxShimba

Platinum Member
Joined
Apr 11, 2008
Posts
36,008
Reaction score
4,093
222424_397748996962544_1054002765_n.jpg


Comment kwa kutaja shule, adhabu na mwalimu ambaye hutokaa usahau viboko vyake!
 
Hahhaaaaa Gambian Boys, Mr. Madiga huyo bhana, saa hizi kawa mkurugenzi sijui wa Wilaya gani huko
 
Mr Kaima alikuwa Ashira Girls!!Huyu alikuwa mkali balaa,katutembeza sana kwa magoti!!!
 
'sundi' buhangija hiyo!!!ila leo kawa kama mbwa koko mpoleeeee!
 
mr. Thomas a.k.a uncle Tom..... Huyu ticha alikua wa hisabati, sasa sera yake ilikuwa maswali 50 ya hesabu usikose zaidi ya maswali 3. vinginevyo zikizidi kila swali utakalokosa anakuramba bakora 3,,, ilikuwa Kilakala primary school.
 
Mr Kiguru ( R I P ) Mwembetogwa, mzee wa wababa ntapiga wapi sasa huyu hana nyama.
 
Mgonapasipapumuno huyu alikuwa balaa njosi sec.
 
Mwanangu mbuzimzee usinikumbushe kasheshe niliyopata skuli. Hata hivyo vilitupika tukaiva na kuwa na manufaa.
 
Mwl luyeye a.k.a mzee poa wa s/m mzakwe.....kengele ya namba asubuhi anagonga mwenyewe kudadadeki
 
Mr. Shija - TBR Girls, hata sijui alikuwa anafundisha somo gani maana nilikua A-Level alikua anafundisha O-Level nadhani ni masomo ya ufundi maana ofisi zake zilikuwa karakana. Huyu O-Level walikuuwa wanamwita "chimpanzee" kutokana na umbo lake na mwendo. Ikiwa zamu yake wiki nzima mnakuwa kama mko kwenye wasiwasi wa vita! Alikuwa hajali kuingia mabweni ya wasichana kutimua watu waende prep usiku na kuwahi mchaka mchaka asubuhi. Muwe mnavaa au mmelala ye hajali anachojali ni muda tu!

Alikuwa na uwezo wa kuchapa form I mpaka VI mtu wa 1 na wa mwisho wakatapa maumivu sawa.
Kuna siku alinichapa kwa kutosafisha eneo tulilopangiwa Form V, fimbo iliuma mpaka nikahisi kupata kichaa! Nilijikuta nampigia makelele "UMENICHAPA HIVI? NA SIFAGIII! NASEMA SIFAGIIIII! Wenzangu hawakuamini maana sikufagia kweli na aliamua kuniacha.
 
Mrs Kitine, Shule ya msingi Mapinduzi staili ya "shika masikio" ile unachuchumaa then unapitisha mikono yako through ur legs hehe

Mr Uhuchu, The Highlands Sec School ilikuwa inaitwa "under the table" hata muwe ishirini mtaingia 2 ukitokezea tu kiboko hehe gud ol times
 
........Mgaya simply ulikuwa child abuser, RIP where you're. I can't describe more!
 
Mwalimu Mtolela, Kisutu Pri. School RIP na kama uko hai, die soon.

Sekondari hakuna mwanaume aliyethubutu kugusa masa..ri yangu.
 
Back
Top Bottom