Je, unakumbuka ulivyokuwa ukifikiria ulipokuwa mtoto?

Mimi nilifikiri ngongoti sio binadamu,halafu nilifikiri kuwa kwenye filamu mtu akifa inakuwa kweli.
 

Zamani enzi za RTD kabla ya taarifa ya habari zilipigwa ngoma za Mzee Moris Nyunyusa basi mie nilidhani kuwa Mzee yule yuko ndani ya redio yetu aina ya Memory Q. Siku moja nilisafiri na wazazi wangu kwenda Lindi, siku moja tukiwa na mwenyeji wetu kabla ya taarifa ya habari, nilisikia zile ngoma. Nilishangaa sana kuwa Moris Nyunyusa amefikaje kule Lindi tena kwenye redio nyingine isiyo ya kwetu!
 


Mkuu umenichekesha..ila umenikumbusha miaka ya karibuni tu kuna mtu alikuwa Dsm aliwasha bluetooth kwenye cm yake akampigia cm rafiki yake alikuwa Mbeya kwamba amrushie wimbo
 
mi nlidhani mlio wa honi za gari unatoka kwenye taa"headlight" za gari,afu ili gari iende spid unanyonga zaidi usukani
 
Jamani sina mbavu hapa. Mimi nakumbuka nikiwa Class One nilikuwa nafikiri mwalimu wangu wa kike hana kovu lolote sehemu ya mwili kwahiyo kila siku namchunguza akifundisha nikaona ni msafi na hivyo nika conclude that walimu hawana scars.
 
nilikuwa nadhani majambazi ni jamii ya watu,nikawa natamani siku moja wavamie kwetu afu mi nikamate kitoto chao ndo nipambane nacho
 
Mimi nilikua najua kwamba ukipiga picha mbele ya ukuta, picha yako inatokea ukutani wakati huohuo.
 
Mimi nilikua najua kwamba mtu anayeendesha gari kubwa ana nguvu sana kuliko anayeendesha gari ndogo
 
nikiwa darasa la tano[watoto wa siku hizi tofauti kabisa dah] nakumbuka nilifuatwa shule niende nyumbani kumsalimia broo ambae alikuwa anatoka uk baaada ya kukaa miaka minne; ilikuwa patashika kwani kwanza nilijua jamaa keshageuka kuwa mzungu halafu hajui tena kiswahili wala lugha ya nyumbani!!ukizingatia nilikuwa sijui zaidi ya zis,zat ,no na yes! Nilipata wakati mgumu mno kurudi home siku hiyo..:......
 
Mkuu usihangaike reference ya mbali sana, im a case study. Nimenunua simu ya memory card mwaka juzi nikampigia simu rafiki yangu aliyeko Tanga anitumie wimbo wa machozi kwa bluetooth mie nipo Ludewa.
Mkuu umenichekesha..ila umenikumbusha miaka ya karibuni tu kuna mtu alikuwa Dsm aliwasha bluetooth kwenye cm yake akampigia cm rafiki yake alikuwa Mbeya kwamba amrushie wimbo
 
Mkuu usihangaike reference ya mbali sana, im a case study. Nimenunua simu ya memory card mwaka juzi nikampigia simu rafiki yangu aliyeko Tanga anitumie wimbo wa machozi kwa bluetooth mie nipo Ludewa. Nikikumbuka nashindwa kujishangaa!!!
Mkuu umenichekesha..ila umenikumbusha miaka ya karibuni tu kuna mtu alikuwa Dsm aliwasha bluetooth kwenye cm yake akampigia cm rafiki yake alikuwa Mbeya kwamba amrushie wimbo
 

Mkuu, umenikumbusha Yolanda! Akina Lulu hawajui hii kitu.
 
Mie utotoni nilikuwa nadhania samaki hulimwa kama mazao(nafaka) basi kila nikimaliza kula nilikuwa nakusanya mifupa nakwenda kuotesha shambani cha ajabu ilikuwa haichepui ndipo bibi akaja kunitoa tongotongo!
 
Mimi nilikua najua kwamba ukipiga picha mbele ya ukuta, picha yako inatokea ukutani wakati huohuo.
Khaaa !? Aiseeh ! Mie huwezi amini, niliishusha saa kubwa ya ukutani ile ya kizamani, nikaifumua yote nijue kulikoni. Aaaah ! Kimbembe ikawa kurudishia kama ilivyokuwa, aaaah........................wapi ! Nikaikusanya nikaitupia juu ya dari ! Nyumbani iliaminika imeibiwa !
 
kila mmoja wenu alijuwa kuwa watoto wananunuliwa.
Na kama hukupatwa hapo basi mlikuwa mnajuwa kuwa watoto wanazaliwa kutokea kwenye matumbo ya mama zao ambayo yanakuwa yanachanwa.
Kuna mtoto alimuona mama yake mdogo ni mjamzito, kisha akaenda kujifungua. Aliporudi na mtoto, ndipo yule mtoto akadai ufafanuzi watoto wanapatikanaje !? Akajibiwa kuwa wananunuliwa Hospitali. Mtoto akaendelea kuliza: Je inakuwaje kwa Ng'ombe ? Hupata wapi pesa !? Kisha akasema Yeye ameshuhudia Ng'ombe wa Babu alipompitishia mtoto wake ! Watu wazima wakatoa mimacho kodo kwa uongo wao !
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…