jchofachogenda
JF-Expert Member
- Jan 8, 2012
- 537
- 123
Mimi nilifikiri ngongoti sio binadamu,halafu nilifikiri kuwa kwenye filamu mtu akifa inakuwa kweli.
Nakumbuka nilipokuwa mtoto kila nilipokwenda stesheni (Tbr) nilikuta injini za tren zipo on muda wote, pia mabehewa yakisukumwa kwenda mbele na nyuma. Hapo nilidhani kwamba injini ya treni ikizimwa basi haiwaki tena, na mabehewa yakikaa muda mrefu bila kupelekwa mbele na kurudishwa nyuma (shanting) hupata kutu na kusababisha injini kushindwa kuyavuta. Je wewe unakumbuka nini ulipokuwa mtoto?
mwlimu wa sayansi alifundisha matumizi ya darubini.
akasema moja ya hayo ni kuangalia kitu kilichombali,
kukivuta na kukiona kwa ukaribu kama vile kiko karibu zaidi.
Mimi nikadhani ni umbali wowote. kaka yangu flani akatoka nairobi,
akawa anapiga story kua darubini yake imeharibika. me nikajua bro hua anatuangalia
tokea nairobi hadi hom (moshi).
hiyo hata mimi,afu slow motion ya kwnye muvie nilihangaika sana kujifunzami nilikuwa najuwa akina madege na watu wote waliopo kwenye gazeti la sani wapo kweli Hahaaaaaa
aisee huu ni ukweli kabisaaaa...!
Mkuu umenichekesha..ila umenikumbusha miaka ya karibuni tu kuna mtu alikuwa Dsm aliwasha bluetooth kwenye cm yake akampigia cm rafiki yake alikuwa Mbeya kwamba amrushie wimbo
Mkuu umenichekesha..ila umenikumbusha miaka ya karibuni tu kuna mtu alikuwa Dsm aliwasha bluetooth kwenye cm yake akampigia cm rafiki yake alikuwa Mbeya kwamba amrushie wimbo
kumi hili nilisahau kulinukuu mwanzo mm wakati niko totoo nilikuwa najua ukipaka pafyumu na ukibana makwapa harufu haisikiki kwa wengine ila ukiachia mikono au ukokaa kawaida ndo harufu inaruka kwa wengine basi bana,
sikui ya siku nakumbuka ilikuwa usiku nishaoga nimevaa night dress mama akanituma rum kwake nikalete kalamu na gazeti coz mum alikuwa anapenda kujaza puzzle games kwene magazeti sasa kwa ufinyu wangu wa akili nikaona pafyum kwene dressing table wajua ilikuwa pafyum gani bana ilikuwa yolanda kopo la bati la rangi ya pinki we acha nikapuliza makwapa yote halafu nikabana makwapa kwanguvu nikapeleka gazeti na kalamu kwa mama huku mikono imebana kwapani kwanguvu ili asisikie harufu nikashangaa akaniambia nani kakwambia upake pafyum yangu weee nilitahayari nikaomba msamaha haraka kabla cjashushiwa kofi coz mum alikuwa mkali balaa lol nikaondoka ila nikajiuliza alijuaje wakati nilibana makwapa sana jibu ckupata now najiona very fun
mi nilikuwa najuwa akina madege na watu wote waliopo kwenye gazeti la sani wapo kweli Hahaaaaaa
Khaaa !? Aiseeh ! Mie huwezi amini, niliishusha saa kubwa ya ukutani ile ya kizamani, nikaifumua yote nijue kulikoni. Aaaah ! Kimbembe ikawa kurudishia kama ilivyokuwa, aaaah........................wapi ! Nikaikusanya nikaitupia juu ya dari ! Nyumbani iliaminika imeibiwa !Mimi nilikua najua kwamba ukipiga picha mbele ya ukuta, picha yako inatokea ukutani wakati huohuo.
Kuna mtoto alimuona mama yake mdogo ni mjamzito, kisha akaenda kujifungua. Aliporudi na mtoto, ndipo yule mtoto akadai ufafanuzi watoto wanapatikanaje !? Akajibiwa kuwa wananunuliwa Hospitali. Mtoto akaendelea kuliza: Je inakuwaje kwa Ng'ombe ? Hupata wapi pesa !? Kisha akasema Yeye ameshuhudia Ng'ombe wa Babu alipompitishia mtoto wake ! Watu wazima wakatoa mimacho kodo kwa uongo wao !kila mmoja wenu alijuwa kuwa watoto wananunuliwa.
Na kama hukupatwa hapo basi mlikuwa mnajuwa kuwa watoto wanazaliwa kutokea kwenye matumbo ya mama zao ambayo yanakuwa yanachanwa.