JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 625
- 938
Nini Chanzo Cha Pneumonia
Pneumonia husababishwa na bacteria, virusi, fangasi na vyanzo vingine. Hapa chini tutaona baadhi ya vyanzo hivi kwa undani zaidi:
Bacterial Pneumonia
Wagonjwa wengi wa pneumonia hushambuliwa na bacteria aitwaye Streptococcus pneumoniae. Watu wanaougua kwa muda mrefu ugonjwa wa obstructive pulmonary disease (COPD) au wale wanaotumia pombe kwa wingi hupata pneumonia kutokana na bacteria waitwao Klebsiella pneumoniae na Hemophilus influenzae. Baadhi ya wagonjwa wengine hupata ugonjwa huu kutokana na bacteria aitwaye Mycoplasma pneumoniae.
Maji yasiyo salama yakinywewa au kutumika ndani ya viyoyozi husababisha pneumonia kutokana na bacteria aitwaye bacterium Legionella pneumoniae.
ZIFUATAZO NI AINA ZA NIMONIA
Kuna aina ya pneumonia, pneumocystis carinii pneumonia, ambayo hushambulia mapafu yote mawili inayotokana na mwili kuwa na upungufu wa kinga unaotokana na magonjwa ya kansa au UKIMWI au kutibiwa rheumatoid arthritis na baadhi ya dawa.
Viral Pneumonia
Hii ni pneumonia inayotokana na virusi na ambayo haisikii tiba za antibiotics. Baadhi ya virusi wa aini hii ni Adenoviruses, rhinovirus, influenza virus (flu), respiratory syncytial virus (RSV), na parainfluenza virus.
Fungal Pneumonia
Aina hii ya pneumonia husababishwa na fangasi wa aina za histoplasmosis, coccidiomycosis, blastomycosis, aspergillosis, na cryptococcosis.
Nosocomial Pneumonia
Viumbe wadogo walioishi kwenye mazingira ya antibiotics kwa muda mrefu hujijengea uwezo wa kuhimili dawa hizo na pindi wakiingia katika mapafu husababisha nosocomial pneumonia. Bacteria wa aina hii hupatikana kwenye majumba ya kuuguzia wagonjwa na katika hospitali