Je, unajua maana halisi ya Electoral College inayotumika kuchagua Rais Marekani? Jifunze

Mkuu ni sawa lakini mie nilielewa tofauti kidogo na wewe ni kwamba electoral college votes ni zile kura ambazo kila jimbo linapewa kutokana na wawakilishi wake mfano Dar ina majimbo kumi manake ina kura kumi Mwanza labda ina kumi na mbili manake kura kumi na mbili na hii haijali kama Dar ina wengi kuliko,Mwanza na kinachofanyika sio wawakilishi wanapiga kura huwa ni kwamba ukishinda labda Dar basi kumi zote ni zako sio wawakilishi wanapiga kura
Upo sahihi zaidi
 
Calfonia inastahili kulingana na idadi ya watu na nguvu yake kiuchumi.Hillary alishinda kwenye majimbo yenye wajumbe wachache hivyo anakuwa na kura nyingi za watu mmoja mmoja lakini wajumbe wachache ndo maana HC anashindwa.Hata Bush alimpiga All Gore hivyo hivyo hasa baada ya kushinda Florida yenye wajumbe 29.
bush aliiba kura chaguzi zote,kuna watu wanaamua rais awe nani kama walivoamua trump wa republican awe rais
 
Mkuu ni sawa lakini mie nilielewa tofauti kidogo na wewe ni kwamba electoral college votes ni zile kura ambazo kila jimbo linapewa kutokana na wawakilishi wake mfano Dar ina majimbo kumi manake ina kura kumi Mwanza labda ina kumi na mbili manake kura kumi na mbili na hii haijali kama Dar ina wengi kuliko,Mwanza na kinachofanyika sio wawakilishi wanapiga kura huwa ni kwamba ukishinda labda Dar basi kumi zote ni zako sio wawakilishi wanapiga kura
Hapana hata sio hivyo hiyo ni body inayohaguliwa wajumbe na wananchi wamarekani hawachagui raisi moja kwa moja isipokuwa wanachagua hao wajumbe na hiyo bodi inakuwa inaitwa United States Electoral College, ni kama hapo juu jamaa the bold ameelezea vizuri wanapopiga wanakuwa wanachagua "electors" na sio rais.
k
wa mujibu wa wikipedia
"The United States Electoral College is the body that elects the President and Vice President of the United States every four years. Citizens of the United States do not directly elect the president or the vice president; instead they choose "electors", who usually pledge to vote for particular candidates"
Electoral College (United States) - Wikipedia
 
Uchaguzi wa marekani ni wa kihuni sana, iweje kura hazitangazwi? Kwanini hakuna waangalizi wa kimataifa? Marekani inawatu 400m halafu tuambiwe kura 270 tu, hata uchaguzi wa kumchagua lipumba cuf hauko hivyo.
Mkuu kawasaidie TBS kufanya utafiti wa ubora wa Gongo, naona haya ya siasa kwa sasa hayakufai..
 
The bold umeeleza vizuri na kwa kuongezea tu ni kwamba sio kila jimbo lina idadi sawa ya wajumbe bali kuna jinsi walivyopanga wao. Nasikia California ndio ina wajumbe wengi. Hii kitu inaleta utata kwa demokrasia kama zetu na wengine kufikia hatua ya kuona kuwa hakuna haja ya hizi kura za 'popular vote' maana hata mkimchagua mtu hawezi kupita mpaka hizi za wajumbe!
Kupanuana akili zaidi katika hili, mwanzoni nilidhani kwamba ile idadi ya wajumbe wa elector collage wanagawana kwa percentage ya kura za popular vote lakini mkuu kaeleza vizuri.
mimi nadhani zina maana kubwa maana zinapelekea mtu kupata zile electro collage vote
 
Raha ya uchaguzi bongo unakuta wale wazee na miwani yao na sura za kinafiki wamevaa kauda suti zao na makobasi chini huku police wamejipanga kama tuko vitani Nec na Zec mungu anawaona
 
Electoral collage ni kama point tu, kwamba kwa kuwa Dar ina watu wengi, ukishinda unapata point 30, Mwanza point 20, Dodoma point 5 nk. Kwa hiyo unaweza kuwa umepata kura nyingi lakini kwenye majimbo mengi madogo yasiyo na point kubwa. Hii ndio imemtokea Hillary
 
Hapo nimeelewa,je ile ya kutaka kuchaguliwa kwa awamu ya pili,rais aliopo madarakani inakuwaje je, anakuwa na urais wake huku anaomba kura au .........na je rais wa U.S anaruhusiwa kuwa mwenyekiti wa chama chake ...............????
 
Napata shida kufanya tathmini kwamba Hillary Clinton alishinda majority votes kwa tofauti ya kura zaidi ya laki moja, lakini swala la electoral votes yenye idadi ya 270 votes bado sijaelewa vizuri na nina hakika Watanzania wengi hawafahamu zaidi ya kushabikia tu.

Sisi tusioelewa lakini mashabiki wa siasa tunahitaji msaada hapa na tuone application ya hii electoral votes kama ingetokea Tanzania, naambiwa Magufuli angekuwa kama Hillary.

JIBU

Maana Halisi ya Electoral Votes

'Electoral College votes system' ni mfumo mzuri uliowekwa ili kuleta usawa Marekani sababu ni Taifa lilioundwa kwa muungano wa States zipatazo 50. Kuna states kubwa na ndogo kwa maana ya population hivyo ukiruhusu mfumo wa uchaguzi wa 'the highest vote-getter automatically win' kama wa hapa Tanzania basi mgombea anaweza kwenda kupiga campaign kwenye states chache tu zenye wapiga kura wengi na akashinda Uchaguzi e.g Califorina, Texas, Florida, New York na Pennyslavania na akashinda urais wa Marekani.
Hivyo kwa kigezo hicho cha population kila states imepewa idadi maalum ya Electors, mfano state yenye electors wengi ni Califorina ambao ni 55 wakati state yenye electors wachache kabisa ni Alaska. Siku ya uchaguzi wananchi wanaenda kupiga kura na mgombea atakayepata kura nyingi kuliko wote kwenye state husika basi atapata electoral votes zote zilizopo kwenye state hiyo.

Jumla ya electoral college votes kwa Taifa zima ni 538, hivyo mgombea atakayewahi kupata electoral votes 270 automatically kwa hisabati ndogo tu atakuwa ameshinda uchaguzi na kuwa Raisi wa Marekani.

Hivyobasi upo uwezekano mathematically mgombea akawa na popular votes nyingi lakini asishinde uchaguzi. Mfano mwaka 2000 George Bush alipitwa kwenye popular votes na Mr. Al Gore kwa ratio ya 51% kwa 47% lakini alishinda uchaguzi kwa electoral college votes 271 versus 266 alizopata bwana Al Gore.
Vivyo hivyo mwaka huu 2016 Clinton ana popular votes 47.7% dhidi ya Trump 47.5% lakini electoral votes ni 290 kwa 232, na hapo bado tunasubiri confirmation results za state ya Michigan ambapo bado Trump yupo juu kwa maana ya majority votes...hivyo majibu ya Michigan states yenye electoral votes 16 yakiwa confirmed kura za Trump zitaongezea kufikia electoral votes 306. Ili jumla ya 306 na 232 za Clinton ziwe 538.

Ni mfumo mzuri sana ambao nafikiri hata nchi za Afrika inabidi tu-copy and paste.

Regards,
COTANGENT
 
Mi naona huu ni mbovu kuliko, mgombea pia anaweza kutilia umakini kwenye jimbo lenye wajumbe wengi, kwani hauoni majimbo kama manne hivi yameamua rais awe nani, ni mfumo ambao haufai kuigwa kwa afrika haufai kabisa.
 
Ni hivi Mkuu;

Uchaguzi wa marekani una kitu wanaita Electoral Collage, hii ni ile 'mechanism' ya kumtambua/kumchagua mgombea urais ambaye anakuwa ameshinda kwa kuzingatia jimbo kwa jimbo!

Sasa iko vipi?? Wamarekani wanapokuwa wanapiga kura ni kwamba wanakuwa wanapiga kura kuchagua watu wanawaita 'electors'! Hawa electors ndio wanaopiga kwa niaba ya jimbo lao.. Sasa vyama vyote viwili wanakuwa na electors ambao wanachagulia siku ya convention ya kumpitisha mgombea wa chama au wakati wa Primaries.

Kwahiyo wamarekani wanapopiga kura kwenye jimbo tuseme kwa mfano California na ikaonekana Trump ameshinda California kwahiyo ina maana kuwa electors wa republican ndio pekee watakaopiga kura kwa niaba ya California na hii inamaanisha kuwa kura zote (electoral collage) za urais kwa jimbo la California zitaenda kwa Trump.

Na kwa nyongeza tu kwamba majimbo yote ya marekani ukiacha jimbo la Nebraska na Maine wanatumia mfumi wa aliyepata kura nyingi za wananchi anapewa electors/electoral Collage wote (Winner takes all).

Ingawa kuna jambo moja la msingi la kulifahamu ni kwamba hawa electors hawabanwi na katiba kumchagua mtu wa chama chake. Anaweza kumchagua mgombea yeyote but kinachowabana ni kwamba kipindi anachagulia kama elector anatakiwa aweke 'pledge' kuwa atamchagua mgombea wa chama chake.!
Safi mkuu nimepata kituuu
 
Asante mkulu. Hapo nilikuwa sufri kbs
 
Historia ya mfumo huu ni pale blacks au watumwa huru walipo ruhusiwa kupiga kura. walifanya hivi kuzuia watumwa ku influence ushiundi hasa majimbo yaliyo kuwa na watumwa wengi.
sababu nyengine ni pia kuzuia majimbo makubwa kuweka mtu wao kila uchaguzi ...hivyo mfumo wa kura za wananchi ukaachwa.
uchaguzi huu nao umeonesha white supremacy , makabwela na mambwanyeye wa kizungu walijitokeza kwa wingi kumpigia Trump amabye ameahidi kurejesha amerika yao....wamechoka na siasa za democratic party ya kukumbatia waislam , ma black na malatino
 
Ni matokeo ya ushindi ambayo yna athari kubwa kwa chama cha Democrats. Mara tatu sasa uchaguzi huu, uchaguzi wa 2000 Al Gore na mwingine sikumbuki ni mwaka gani ambapo mgombea wa Dems alipata kura nyingi kuliko yule wa Republicans. Juhudi za Democrats kubadili mfumo huu wa Electoral Votes zimegonga ukuta kwa sababu Republicans wana njua itakula kwao. Utakuta vimiji vidogo vidogo kama vijijini vile ambapo wakazi wote ni Wazungu au 99% ni wazungu vimepewa electoral votes nyingi ukilinganisha na miji ambayo ina mchanganyiko wa watu mbali mbali. Huko kwa Wazungu watupu Dems huwa hawashindi hata siku moja hivyo kujinyakulia EV nyingi. Najua hili litazungumzwa sana kufuatia uchaguzi huu baada ya Hillary kupata kura nyingi lakini kushindwa kwenye EV.

Dah MKUU umeleta mada nzuri hata Mimi sijaielewa hii aina ya matokeo ya ushindi.
 
Uchaguzi wa marekani ni wa kihuni sana, iweje kura hazitangazwi? Kwanini hakuna waangalizi wa kimataifa? Marekani inawatu 400m halafu tuambiwe kura 270 tu, hata uchaguzi wa kumchagua lipumba cuf hauko hivyo.
Kweli ushamba mzigo ulifikiri na kule kuna masanduku ya kuibia kura kama kwenu?
 
Ni matokeo ya ushindi ambayo yna athari kubwa kwa chama cha Democrats. Mara tatu sasa uchaguzi huu, uchaguzi wa 2000 Al Gore na mwingine sikumbuki ni mwaka gani ambapo mgombea wa Dems alipata kura nyingi kuliko yule wa Republicans. Juhudi za Democrats kubadili mfumo huu wa Electoral Votes zimegonga ukuta kwa sababu Republicans wana njua itakula kwao. Utakuta vimiji vidogo vidogo kama vijijini vile ambapo wakazi wote ni Wazungu au 99% ni wazungu vimepewa electoral votes nyingi ukilinganisha na miji ambayo ina mchanganyiko wa watu mbali mbali. Huko kwa Wazungu watupu Dems huwa hawashindi hata siku moja hivyo kujinyakulia EV nyingi. Najua hili litazungumzwa sana kufuatia uchaguzi huu baada ya Hillary kupata kura nyingi lakini kushindwa kwenye EV.

hizo zite ni sababu ambazo hazina msingi, democrats na huwa wanashinda uchaguzi mara kibao tu kwa mfumo huu huu, na kusema republicans itakula kwao bila mfumo huu ni uongo, make republicans walishapigiwa kura nyingi zaidi ya dems mara kibao tu
 
0c5fa45f04dc2c7f9e92b3e024d01fc8.jpg
 
Back
Top Bottom