El Jefe
JF-Expert Member
- Sep 13, 2016
- 293
- 364
Electors wanapiga kura (Electoral Votes) baada ya wananchi kupiga kura (Popular Vote) kwenye uchaguzi. Wananchi wakishapiga kura na mshindi akajulikana ndipo wao wanaenda kupiga kura.Ngoja kidogo twende taratibu, sasa kama kila chama kina idadi sawa ya electors kwa jimbo husika inakuaje mgombea mmoja awashinde wengine? kwa nini isiwe draw kila uchaguzi ukifanyika? maana kila elector akimpa kura mgombea wa chama chake maana watakua wamefungana wagombea wote hakutakua na mshindi. Yaani mfano Chadema wanawapiga kura 10, ccm wanawapiga kura 10, na tlp wanawapiga kura 10. Sasa hapo si kila mpiga kura anampigia mgombea wa chama chake kwenye hilo jimbo tunategemea matokeo kila mgombea atapata kura 10. Najua nakuchosha lakini kwa kweli bado sijaelewa.
Usidhani Electors wote wa vyama vyote wanaenda kupiga kura kwenye State husika, hapana, bali Electors wanaopiga kura ni wale ambao chama chao kimeshinda uchaguzi kwenye State husika.
Mara zote lengo la Electors sio kwenda kubadilisha matokeo. Ndio maana Trump ameshatangazwa ni Rais hata kabla ya Electors wa chama chake kumpigia kura. Electors watapiga kura tarehe 19 December 2016 ila wananchi walishapiga kura tarehe 8 November 2016 na kuamua mshindi katika kila State.
Hizo States alizoshinda Trump atapata Electoral Votes zote za Electors wake. Lakini States ambazo Trump ameshindwa hatapata Electoral Votes kwakuwa Electors wake hawaruhusiwi kumpigia kura kwenye States alizoshindwa.
Jaribu kubonyeza link hapa chini, uangalie jinsi wagombea wa Urais wa US mwaka 2016 watakavyopata Electoral Votes za Electors wa vyama vyao.
2016 Election Results: President Live Map by State, Real-Time Voting Updates