Je, unajua kwamba kunguru ni kitoweo?

Je, unajua kwamba kunguru ni kitoweo?

Mimi si ndiyo uliyenijibu!!!, sasa fafanua kwanini uchafu wa nguruwe unapotajwa wewe unakasirika???--- uchafu afanye nguruwe na ashutumiwe yeye wewe unapandwa na ghadhabu, kiwewe na mzuka!!!, Why??
Hata Mimi naongezea.Hakuna mnyama msafi Kama Nguruwe,atakuwa mchafu na kula uchafu kama utaamua kumtunza kimazingira hayo.Nguruwe ni msafi kuliko Wanyama wote.Nimeshuhudia Nguruwe akipigishwa mswaki kila asubuhi na usipomtekelezea siku hiyo ataliga kelele Sana.Nguruwe hali mavi yake na hutenga sehemu ya kujisaidia.Na mwisho,hakuna mnyama mtamu Kama Nguruwe na Ngiri hakuna!
 
Habari za mda huu wakuu,

Hivi karibuni kulikuwa na ubishani Kati yangu na ndugu zangu kuhusu ndege aitwaye Kunguru, wengi tumesikia kwamba ndege huyu hafugiki, hoja ikaja je Kunguru huliwa?. Majibu yakawa wengi Sana Mara ooh kunguru anasumu hata akifa wadudu, inzi hawamgusi Mara anasumu na n.k leo hii nimekuja na fact Kama una addition utaongezea kwenye comment,natanguliza shukrani.

View attachment 1470267

Ukweli Ni kwamba kunguru analiwa, Tambua kwamba Unaweza kula kunguru na usidhurike au kupata magonjwa. Wana ladha sawa na bata bukini,bata mzinga, bata wa kawaida au ndege mwingine wenye nyama nyeusi. Ikiwa wameandaliwa vizuri, wana ladha nzuri, ikiwa sivyo, hauta penda Radha yake,Watu wengine wanadai kuwa hawawezi kuliwa kwa sababu ya tabia yao ya kula karibu kila kitu lakini hiyo sio kweli. Ukiwa uko katika mazingira magumu ya upatikanaji wa chakula, kunguru anapaswa kuwa kwenye menyu yako ikiwa unaweza kuwashika.

Je! Ni sahihi kula kunguru?
Watu wengi wanaamini kuwa kunguru hawapaswi kuliwa kwa sababu hula takataka,mizoga na n.k. Ni Kweli,lakini binadamu tunachagua kwa sababu kunaaina nyingi ya ndege,hivyo kunguru hatakuwa katika orodha ya ndege waliwao, lakini ni sawa kula kama ndege wengine wowote. Ndege wengine pia ni wachafu wanatabia zinazoringana na kunguru,Miaka ya 1930 huko Amerika kunguru alitumika Kama kitoweo,kwasasa Kuna baadhi ya migahawa duniani wanawaandaa kunguru Kama kitoweo Tena maalum .

Je! Kunguru anaradha gani?
Mtazamo mwingine potofu juu ya kunguru ni kwamba wana ladha kama karoti kwa sababu wakati mwingine hula wanyama waliokufa. Hapa si Kweli!!! . kunguru ni ndege mwenye nyama yeusi, Hana Tofauti na ndege wengine wengi. Watu walio Kula huelezewa kuwa na ladha inayopendeza ambayo kwa kweli ni nzuri. Ikiwa wameandaliwa kwa usahihi,ukionja wanaradha kama bata bikini au bata wa kawaida. Ikiwa haijapikwa vizuri, nyama inaweza kuonekana kuwa ngumu.

View attachment 1470268

Jinsi ya kuandaa kunguru!
Kunguru Hana nyama nyingi zaidi ya kifuani,hivyo Haina haja ya kutafutiza nyama nyingine zaidi ya hapo, ukihitaji nyama zaidi maana yake uwinde kunguru wengi zaidi.

View attachment 1470269

Je! Kunguru anaweza kuwindwa kisheria?

Kuna habari inayokinzana huko marekani juu ya uhalali wa kunguru wa uwindaji. Wengine wanasema kwamba walindwa chini ya Sheria ya Mkataba wa Mkataba wa Ndege wa 1918 na wengine wanasema kuwa ni sawa kuwawinda mwaka mzima. Jibu la kweli ni kwamba ni juu ya hali ya mtu binafsi. Baadhi ya majimbo huruhusu kuwindwa wakati wa misimu fulani wakati zingine haziruhusu kamwe na zingine zitakuruhusu uwache kuwinda kila mwaka. hivyo unalazimika uangalie katika eneo lako kuona ni lini (au ikiwa) ni sawa kuwinda kunguru chini ya hali ya kawaida.
Kwa hapa kwetu Tanzania sijajua Kama Sheria ipo ya uwindaji was kunguru!🙂

Je! Kunguru Hubeba Magonjwa Gani?
Kulingana na Miaka hii, ndege wengi wana uwezo wa kubeba magonjwa ambayo yanaweza kuathiri wanadamu.Unapaswa kufahamu uwezekano wa kuwa kunguru anaweza kubeba ugonjwa upo, hii haimaanishi kuwa huwezi kula.

Ndege wanaweza kusababisha magonjwa yafuatayo kwa wanadamu:

Histoplasmosis - Historiaoplasmosis ni ugonjwa wa kupumua na unauwezo wa kuuawa. Inatoka kwa Kuvu ambayo hukua katika matone kavu ya ndege.

Cryptococcosis - Cryptococcosis husababishwa na chachu inayopatikana kwenye njia ya matumbo ya ndege.

E.coli. - E. coli inaweza kusambazwa kupitia unyevu au jasho la ndege,Mara nyingi ugonjwa huu unapatikana kwenye mbolea ya ng'ombe hivyo kuku akienda Kula kwenye mbolea Hubeba vimelea bila kumdhuru na anaweza kuviacha kwenye vyombo vya chakula na maji.

Je! Kunguru huua ndege wengine?
kunguru hula mayai na viota vya ndege wengine. Pia wakati mwingine hula ndege wakubwa wa aina zingine ikiwa wana uwezo wa kuwakamata.

Kunguru anaweza kuishi Miaka mingapi?
Kunguru anaweza kuishi hadi uzee. kunguru kawaida hufa akiwa na zaidi ya miaka 20 ikiwa hawatauwawa kwa njia zingine. kunguru mzee wa porini huoshi Miaka 30,kunguru anayefugwa huishi mpaka Miaka 59!

Hitimisho watu wengi wanatamani kujaribu Kula kunguru labda ni jambo ambalo wengi wetu tungependa. kunguru wanapatikana mahali pote na watakuwa chanzo rahisi cha chakula ikiwa tutaweza kuwala ... kwa bahati nzuri unaweza kula. Hakikisha tu unawapika vizuri Kama ndege wengine.

By rodian

usijaribu kabisa hii kitu, hayo yatokanayo na wanyama pori ni hatari sana. Covid 19 Corona inatosha
 
Watu wanakula mpaka Bundi ndio utajua Mabaharia nuksi
 
Haya, na Fisi naye aliwe kama nguruwe pia, kwa nini hawamli ??, wanabagua Scavengers.
Mkuu inabidi utambue kuwa uchaguzi wa mnyama gani aliwe au asiliwe unaathiriwa zaidi na jamii unayoishi nayo.
Mfano, jamii ya watu wa tanzania hawali fisi si kwa sababu labda nyama ya fisi ni mbaya hapana, ni kwa sababu watangulizi wao walikuta hawali fisi. Mimi kama ningekuta jamii yangu wanakula fisi na mimi ningekula kwa sababu tangu utoto wangu akili yangu ingetambua kuwa fisi ni kitoweo.
Nakula nguruwe kwa sababu nimekuta jamii yangu inakula nguruwe.
 
Haya swali liwe hivi; kwanini watangulizi wako hawakumfanya Fisi awe kitoweo kama nguruwe??
 
Haya swali liwe hivi; kwanini watangulizi wako hawakumfanya Fisi awe kitoweo kama nguruwe??
Mkuu siwezi kujua moja kwa moja ni sababu zipi lakini sababu moja wapo zaweza kuwa ni urahisi katika upatikanaji, imani na mapendeleo binafsi. Kwa mfano dodoma kuna watu wanakula chura, na wengine hawali.
Kuna jamii wanakula nyoka na jamii nyingine hawali. Kuna jamii wanakula popo na kuna jamii hawali. Kwa mifano hiyo michache unaweza kuona si jinsi yule mnyama alivyo ndicho hufanya mtu aamue kama amfanye kitoweo au lah, bali ni mtazamo wa mtu mwenyewe juu ya huyo mnyama.
 
Mkuu, umetaja jamii zinazokula chura, popo nk, na zipo jamii zinakula panya, sasa nataka unionyeshe jamii inayokula Fisi, kama ni suala la upatikanaji mbona kuna jamii zinakula swala, Nyati, Tembo,Pundamilia, Kiboko, Twiga nk, hao wote wanapatiana vipi tushindwe kupata jamii inayokula Fisi ???
 
Mkuu wewe unazifahamu jamii zote ulimwenguni? Nimeshakutajia sababu zinazoweza kuathiri uchaguzi wa mnyama kuwa kitoweo. Kwa hiyo kwa kupitia hizo sababu mtu anaweza kufanya mnyama fulani kuwa kitoweo, awe ni fisi, punda, nzi, chui nk.
 
Mimi nakula nyama ya Swala, Nyati, Twiga, Pundamilia, pongo nk, katika hali ya kawaida kamwe sitakula Nguruwe,Fisi, Tai na Kunguru kwasababu ni Scavengers, kama ni gari basi hao wanyama ni zaidi ya magari ya takataka, Wataalamu wa lishe na chakula (foods and nutrition experts) wanasema; You are what you eat, yaani; Jinsi ulivyo kitabia na kimaumbile "stature" inatokana na vyakula unavyokula, sasa haiwezekani Nguruwe, Fisi na kunguru wale mizoga na takataka halafu wewe ule nyama zao na ubaki salama!!!---- na ndiyo maana hakuna mtu mwenye common sense anayeweza kula nyama ya Fisi au kunguru na Tai.

Watu wengi siku hizi wamekuwa mashoga (ashakum; Mabasha au wasenge) kwasababu ya ulaji wa nguruwe uliokithiri, katika wanyama ukimuondoa nyani na apes wote nguruwe ndiye anaongoza kwa Ushoga hivyo watu wanaopendekea kula sana nguruwe nao wanakuwa na nafasi kubwa ya kuambukizwa ushoga, Ukiona madume ya Simba yanafanya homosexual lazima utakuta maeneo wanayoishi hayo madume kuna nguruwe pori wengi na hao simba hula sana hao nguruwe.

"You are what you eat"
 
Mkuu siwezi kupingana kwa sababu huo ni mtizamo wako, hata hivyo kila mtu anaweza kuishi atakavyo bora tu asivunje sheria za nchi.
Na suala la chakula linabaki kuwa maamuzi binafsi ya mtu.
 
Mkuu siwezi kupingana kwa sababu huo ni mtizamo wako, hata hivyo kila mtu anaweza kuishi atakavyo bora tu asivunje sheria za nchi.
Na suala la chakula linabaki kuwa maamuzi binafsi ya mtu.

Mkuu Stephen, Mimi nakubaliana nawe kwamba mambo ya chakula ni uchaguzi wa mtu binafsi, hayupo mtu awezaye kumlazisha mwenziwe ale nini na asile nini, lakini ni wajibu na jambo jema kutoa nasaha kwa jamii juu ya jambo unaloliona kwalo yafaa nasaha kutolewa ama mtu afuate asifuate hiyo ni juu yake, mimi nimeshika njia ya kutoa nasaha na Mungu atanilipa.

Hata kwenye pakiti ya sigara wameandika; "Cigarette smoking is hazardous to your health"--- kwa maandishi hayo wapo wanaozingatia na wapo wasiojali wanavuta tu.
 
Mungu aliona ya kuwa kila kitu ni chema, ikawa jioni ikawa asubuhi.... mna haki ya kubagua vitoweo kwa kuwa tu mnavyo vingi.
 
Haya swali liwe hivi; kwanini watangulizi wako hawakumfanya Fisi awe kitoweo kama nguruwe??

Ni kwa sababu ‘watangulizi’ walimtumia Fisi kama chombo cha usafiri wa heshima.
 
Kuna jamaa alikula popo akaiponza dunia hadi sasa mambo hayaeleweki.
 
Back
Top Bottom