Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 5,527
- 7,121
Naongea na wewe uliyeachana na mwenzi wako wa kwanza na kuoa au kuolewa tena. Nakujulisha kuwa huyo mke/mume uliye naye sasa sio wako mbele za Mungu — unazini.
Katika dunia ya sasa ambapo talaka na ndoa ya pili au ya tatu zinaonekana kama jambo la kawaida, ni muhimu sana kwa watu wanaotamani kwenda mbinguni kufahamu msimamo wa Mungu juu ya ndoa, talaka, na kuoa au kuolewa tena baada ya talaka.
1. Ndoa ni agano la milele, sio mkataba wa muda
Biblia inafundisha kuwa ndoa ni muungano wa kiroho na kimwili uliowekwa na Mungu mwenyewe.
Katika Mwanzo 2:24 tunaambiwa:
“Kwa hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.”
Muungano huu wa “mwili mmoja” si wa muda, ni wa kudumu mpaka kifo kitakapowatenganisha. Hili linasisitizwa tena na Yesu Kristo katika Mathayo 19:6
"Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe..”
Kwa hiyo, talaka haibatilishi kile Mungu alichokiunganisha. Ingawa mwanadamu anaweza kutoa talaka, mbele za Mungu bado mme na mke wa kwanza wanahesabika kuwa wameunganishwa.
2. Talaka haitoi ruhusa ya kuoa au kuolewa tena
Yesu mwenyewe alizungumzia jambo hili kwa uwazi sana. Katika Luka 16:18 anasema:
"Kila amwachaye mkewe na kumwoa mke mwingine anazini; naye amwoaye yeye aliyeachwa na mumewe anazini.”
Hapa tunaona wazi kuwa kuoa au kuolewa tena baada ya talaka ni uzinzi. Kwa lugha nyingine, kama ulimwacha mume au mke wako wa kwanza, ukaoa au kuolewa tena, basi huyo uliye naye sasa sio wako. Mbele za Mungu unahesabika unaishi katika uzinzi.
3. Talaka iliruhusiwa kwa sababu ya ugumu wa mioyo — sio mpango wa Mungu
Yesu alipoulizwa kuhusu talaka, alisema katika Mathayo 19:8:
“... Musa aliwaruhusu kuwaacha wake zenu kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu. Lakini tangu mwanzo haikuwa hivyo.”
4. Hatari ya kuishi katika uzinzi
Wale wanaoishi na wake au waume wa ndoa ya pili, wanaishi katika hali ya dhambi — yaani uzinzi wa kudumu. Na Biblia inasema wazi katika 1 Wakorintho 6:9-10:
"Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti.”
Hili ni onyo kali. Kama unaendelea kuishi na mke au mume asiye wako bila kutubu na kurekebisha, una hatari ya kupoteza uzima wa milele.
5. Suluhisho: Tubu na umrudie mme au mke wako wa kwanza
Suluhisho sio kuhalalisha mahusiano uliyo nayo sasa. Suluhisho ni kutubu kwa dhati, kujitenga na hali ya uzinzi, na kumrudia mwenzi wako wa kwanza. Kama huwezi kumrudia huyo wa kwanza, ukae hivyo hivyo peke yako.
Katika 1 Wakorintho 7:10-11, Paulo anaandika:
“Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe; lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe.”
Biblia haiungi mkono ndoa ya pili baada ya talaka, bali inashauri ama kubaki bila kuolewa/kuoa au kumrudia mwenzi wa kwanza.