Je unajua kwamba baada ya Miaka 1-1.5 kuku huanza kupunguza utagaji?

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,789
8,915
Kuku anapo timiza mwaka mmoja tangu aanze kutaga, Utagaji huanza kushuka taratibu mpaka kufikia mwisho, na hapa kwa mfugaji alioko siriasi atakuwa na batch za kuku wa kuleplace kila baada ya Miezi 3, Yaani kila Baada ya Miezi 3 unatakiwa uwe tiyari na Batch ya kuku watakao chukua nafasi ya watakao choka kutaga.

8.31chicken-laying-an-egg.jpg

Kushindwa kufanya hivyo kuna maanisha kuna kipindi itafika production itashuka mpaka 0 na hutakiwi kusubili kuku waliopo wazeeke au uwatoe ndo uingize vifaranga wapya, kufanya hivyo maana yake ni kwamba utapoteza wateja wako wote ulio kuwa nao.

NANI ANAFANYA HIVYO?
 
asante kwa kutukumbusha ni kitu muhimu kuweza kulishika soko. Nina swali, kuna mtu anajua wapi chanjo ya Mareks inapatikana?
 
Za siku mamy! Mareks waweza pata pale pamba house, sikumbuki ghorofa ya ngapi ila ukifika pale waweza ulizia office zinazoshughulika na dawa za mifugo.
 
Mim huwa nachukua Nairobi Kenya kwa kweli sijui kwa Bongo na kwa sabababu Marek ni ghari sana mnaweza organise hata watatu mkachukua kwa sababu ile chanjo ni kwa vifaranga 1000 na kama unatotolesha chini ya vifaranga 300 basi si razima kuwapa Marek, na marek haina hatari kama olivyo kider.
Na kuna OTC 5 jaribu kuuliza huko inaweza tumika badala ya Chanjo ya Marek.
 
Ila ukitaka mashine ya kuchoma automatic unaweza pata Nairobi, mimi hiwa natumia mashine wakati wa kuchoma Mareks
 
Za siku mamy! Mareks waweza pata pale pamba house, sikumbuki ghorofa ya ngapi ila ukifika pale waweza ulizia office zinazoshughulika na dawa za mifugo.

asante sana dear tunapambana soon tutakuwa na mayai. Ktk kuulizia soko la mayai ya kutotolesha nimekutana na kuku wa jirani analalamika akitotoa kwa watu mayai kuku wanaugua wanapooza na kufa ndo nikatafuta ugonjwa. Nitapitia hapo pamba house niulizie
 
Mim huwa nachukua Nairobi Kenya kwa kweli sijui kwa Bongo na kwa sabababu Marek ni ghari sana mnaweza organise hata watatu mkachukua kwa sababu ile chanjo ni kwa vifaranga 1000 na kama unatotolesha chini ya vifaranga 300 basi si razima kuwapa Marek, na marek haina hatari kama olivyo kider.
Na kuna OTC 5 jaribu kuuliza huko inaweza tumika badala ya Chanjo ya Marek.

nashukuru sana Chasha kwa maelezo kumbe nikitumia OTC plus pia ni vizuri pia basi nitawaelekeza. Binafsi huwa natumia otc sasa hawa wengine anataka afuge kienyeji bila chanjo wala nini. All the best, siku nikipanga kuja Arusha nitakutafuta nijifunze vingi uko Nairobi bado kidogo.
 
Ni OTC 5 Sio otc plus, karibu sana utanikuta
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom