Masokotz
JF-Expert Member
- Nov 26, 2018
- 3,471
- 5,481
Leo naona nilite mada Chokonozi;
Wengi tumewahi sikia maneno kama Copyright, Trademark patent na mengine kama hayo. Wengine tunayasoma tu tukifikiri na vibwagizo lakini kuna wengine wanayatumia katika kuhakikisha kwamba wanaweka rekodi sawa na zaidi wanazitumia kufanikiwa katika Biashara.
Kuna watu huwa wantengeneza Logo/Nembo za biashara na kutumia muda kuzipromote mtandaoni lakini hawajui kwamba akitokea mtu akazisjaili anaweza kuwanyang'anya na kuzitumia yeye.
Kuna watu wanachukua vifaa fulani na kuvifanyia maboresho na kisha kuja na kitu kingine tofauti lakini hawasajili ule uunifu wao na kujikuta wakishindwa kufaidi matunda ya ubunifua wao hasa pale wenye mitaji wanapoanza kuutumia kujinufaisha.
Kuna watu ni wabunifu by nature. Yaani wana uwezo ama wa kutengenezavitendea kazi au program za Computer our hata vyombo vinge tofauti kama aina fulani ya majiko na vifaa,lakini kwa kutokujua au kutoupa umuhimu ubunifu au ugunduzi wao wanabaki wakilia njaa kumbe utajiri wao walikuwa wanazunguka nao wakati wote.
TradeMark/ServiceMark,patents na Copyrights zote zinalindwa kwa sheria. Ni kosa mtu kuiga nembo yako ya biashara na ni kosa mtu kutumia ubunifu wako bila kukupa mrahaba. Biashara ya Patent ni moja kati ya biashara ya kipekee sana.Kama wewe ni mtaalamu katika eneo fulani unaweza tu ukawa kazi yako ni kutafiti na kuboresha na kugundua na kisha unatengeza pesa kwa kuwauzia wenye mitaji zile Patents zako.
Kumbuka Patent ikishasajiliwa inakuwa ni bidhaa ambayo unaweza kumuuzia mtu.
Watu wengi sana hawatumii hii fursa ya kutafuta namna ya kugundua njia mpya za kufanya mambo kwa kutafuta suluhu za matatizo yetu ya kila siku.
Wale ambao wnasemaga kwamba kuwa na wazo haitoshi huu ni wakati sasa wa kujifunza JINSI Patent inaweza kubadili maisha yako.
Vitu vya kufayhamu ni kwamba unaweza kufanya Patent ndogo ya maboresho(Utility model protection) au Patent kubwa.Unaweza sajili patent kwa nchi zaidi ya moja(International patent au local patent).
Leo nimeona nilete mjadala huu mdogo ili tujadili uelewa wetu kuhusu sheria za haki miliki na ni kwa namna gani mtu anaweza kutumia Hakimiliki (Patent katika kujitengenezea FURSA.
Karibuni tujadili kwani hii ni mada pana pia.