Mkuu
begi la pesa kwa upande wa Copyright yaani hakimiliki coverage yake kwa sehemu kubwa huwa ni universal pasipo kujalisha ulifanya 'designation' kwa nchi zote ama lah! Na ndio maana ukiandika kitabu hapa nchini ama ukitunga na kuba wimbo hapa nchini na ukasajili pale COSOTA basi iwapo kuna mtu Marekani akaunakili na kuuimba unaweza kumshtaki.
Kwa upande mwingine; patent, utility model, na intellectual nyingine tofauti na Copyright huhitaji kusajili ama kifanya designation kwa kila nchi ambayo unataka kulinda huo ubunifu wako. Mfano umeunda mashine na teknolojia mpya ya kitengeneza jembe basi utapaswa kusajili na kufanya compliance kwa nchi zile ambazo utataka ubunifu huo usiingiliwe. Kwa nchi yetu utasajili BRELA, kwa nchi nyinginezo za hapa Africa utasajili ARIPO na kwa upande wa nchi nyinginezo nje ya Africa basi utasajili kupitia WIPO.
Kila la kher