Je, unadhani Rais Samia kwenda kusemea Marekani kuwa kufanya Kazi na Hayati Rais Magufuli ilikuwa Ngumu analenga nini kati ya yafuatayo?

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
1. Anamshtakia Hayati Rais Magufuli kwa Wamarekani?

2. Anataka Kujitofautisha nae ili Wamarekani wampe sana Misaada?

3. Anawaomba Msamaha Kidiplamasia ili Wamarekani wampende?

4. Anathibitisha kuwa Waafrika wote tuna PhD's za Unafiki na Uzandiki tukiwa mbele ya Wazungu?

5. Anawaambia kama ameshindwa kutoa Siri hiyo Kwetu Watanzania na kaenda kuitolea huko Marekani hivyo hata wakihitaji Siri zingine za Kuichukua moja kwa moja Tanzania and we are kuwapa tu?

6. Amewawashia Taa ya Kijani Wamarekani kuwa kwa sasa Tanzania iko chini ya Bibi Mstaarabu na siyo Mkorofi Mwerevu aliyeondoka na Israeli, hivyo wanaweza kuja kuendelea kufanya Tanzania ni Shamba lao la Bibi kama zamani?

7. Anawataarifu rasmi kuwa sasa Tanzania ( Bara na Visiwani ) ni yao hivyo Washindwe tu wenyewe.
 
Kila Ijumaa Kuu, Wakristu tunapoazimisha kifo cha Bwana, hukumbushwa kisa cha Yuda Iskariote.

Yuda anatufundisha na kutukumbusha daima kuwa usaliti hutoka kwa watu wetu wa karibu.

Samia kama msaidizi namba moja wa Hayati Magufuli amedhihirisha dhana hii.

Adui yako hawezi kukusaliti kamwe, ila mtu wako wa karibu.

Tuwe na Jumamosi Kuu njema.
 
Wala mm sioni tatizo yeye kusema hivyo na anapaswa kusema zaidi.
Tatizo langu kwake ni kuchanganya mambo akiwa na watu wa huko. Hasa aliposema Harris Ni mgombea wa kwanza wa umakamu wa uraisi Marekani. Kitu ambacho sio kweli. Tatizo lipo hapo na atafanya wamdharau
 
Na wasi wasi na siri alizokua anazitoa kigogo alikua anazipata direct toka juu.

Back
Top Bottom