Je, umwinyi ulikuwa ni cheo?

Braza Kede

JF-Expert Member
Nov 1, 2012
1,711
3,360
Wakuu kuuliza si ujinga.

Siku za nyuma niliwahi kusikia kuna watu wanaitwa mamwinyi.

Hawa walitajwa kupatikana zaidi ukanda wa pwani.

Naomba kufahamu kama umwinyi ilikuwa ni cheo yaani mtawala wa eneo au ni jina tu la rika fulani au ni jina la heshima au nini hasa?

Na je hawa tunaowatambua kwa jina hilo leo hii je walitoka familia hizo za mamwinyi au ilikuwa ni jina tu kama yalivyo majina mengine?
 
Umwinyi ulikuwa ni mfumo wa ukabaila na utawala katika jamii za Pwani mwa Afrika Mashariki. Ukabaila ndio ulikuwa mfumo wa kwanza wa kiuchumi wenye unyonyaji.
 
Wakuu kuuliza si ujinga.

Siku za nyuma niliwahi kusikia kuna watu wanaitwa mamwinyi.

Hawa walitajwa kupatikana zaidi ukanda wa pwani.

Naomba kufahamu kama umwinyi ilikuwa ni cheo yaani mtawala wa eneo au ni jina tu la rika fulani au ni jina la heshima au nini hasa?

Na je hawa tunaowatambua kwa jina hilo leo hii je walitoka familia hizo za mamwinyi au ilikuwa ni jina tu kama yalivyo majina mengine?
Mwinyi ni boss, mtawala au ni mkuu kwa tafsiri nyingine..
Mamwinyi walikuwepo ukanda wa pwani kuanzia mzizima bagamoyo hadi kwa wabondei kote huko watawala waliitwa mamwinyi..
Mwinymkuu, mwinyijuma, mwinyi, na n.k
 
Back
Top Bottom