Je umehakiki usajili na namba yako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je umehakiki usajili na namba yako

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Oct 27, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Oct 27, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  UMEHAKIKI USAJILI WA NAMBA YAKO

  Ilikuwa siku na wiki sasa ni miezi toka zoezi la kusajili namba za simu kwa wateja wa mitandao yote ya simu nchini kwa kweli watu wengi sana wamesajili namba zao za simu bila kuuliza au kujiuliza itakuwaje huko mbeleni baada ya zoezi zima kufikia kikomo chake na kuanza utaratibu mpya wa manunuzi ya line za simu kuanzia disemba 1 .

  Pamoja na usajili kwenda vizuri sana inabidi sasa kila aliyesajili namba yake awe anawasiliana na kampuni hizi mara kwa mara kujua kama taarifa zake alizosajili wakati huo ni sahihi na hazijabadilika kitu au kuongezewa kingine chochote ambacho yeye hakuweka .

  Kwa sababu katika usajili kuna wengine huwa wanachukuwa tu vitambulisho vya kazi ambavyo havijathibitishwa kama kweli kampuni hizo zipo au kweli mtu huyo anafanya kazi kampuni hiyo au anasoma shule au chuo hicho je kampuni hizi zinahakikisha vipi kufuatilia kujua aina hii ya udanganyifu .

  Je mtu akihama kampuni au shule hata makazi anatakiwa kwenda katika mtandao wake wa simu kutoa taarifa hizi au jambo hili sio lazima sana kinachoangaliwa ni ule usajili wa kwanza tu ?

  Pia kuna wengine wamejisajili lakini hawakuwa wao wamewatuma ndugu zao kwenda na vitambulisho vyao kuwasaidia kusajili jambo hili pia lina utata kidogo kwa sababu kuna wengine wanaweza kutumia taarifa za mwingine bila huyo kujua au kutumia taarifa za mtu ambaye ni mfu hili jambo linawezekana kabisa .

  Na je kampuni hizi zinashirikiana vipi na vyombo vingine kuhakikisha taarifa zinazotolewa na mtu Fulani ni sahihi ? je huwa wanafuatilia kwa wenye viti wa mitaa Fulani kuhakiki kama mfano mtu ametumia kitambulisho chake cha kupigia kura ? au hii ni siri yao wenyewe ?

  Lingine ni kufumuka kwa wizi wa simu huko mbeleni ambapo simu hizo na line zitakuwa zinatumika kwa ajili ya kufanyia uhalifu au hujuma zingine mbali mbali , je kampuni hizi za mawasiliano zimejiandaaje pamoja na vyombo vya sheria .

  Unaweza kudondosha simu yako ndani ya daladala la kwenda sehemu Fulani wakati wa jioni , mtu akaokota simu hiyo akaenda kutumia kwa shuguli zake zingine , fikiria kama uko mbali na kituo cha polisi utatoaje taarifa mapema zaidi kabla ya tukio hilo kutokea ?

  Na unapoenda kituo cha polisi hao askari watathibitishaje kwamba ni simu yako kweli pamoja na line hiyo ? inabidi kuwasiliana na kampuni yako ya simu mfano kama usiku itakuwa tabu kidogo huwezi kwenda kwenye kampuni yako usiku itabidi ongoje kesho labda askari watapewa uwezo wa kuwasiliana na kampuni za simu waweze kuzuia line hiyo isitumike hata hivyo itabidi uende na uthibisho wa usajili wako kwa njia ya maandishi .

  Mwisho ningependelea uanzishwe utaratibu wa kuwa namba za siri kwa kila mteja ambapo kama inatokea tatizo Fulani linalohusu simu yake basi aweze kuthibitisha kutumia namba za siri na hizi namba ziwe zinabadilika mara kwa mara .

  Usikose kutembelea www.askmaro.blogspot.com Upate mambo moto moto
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Lets not build castles in Air!
  Lets be patient dudes, all questions are going to be answered with time!
  After all no any system on Earth that starts with 100% efficiency!

  Otherwise, BIG-UP to you for a kinda ALERT!
   
Loading...