Mimi nimejibu swali la "chanzo cha mtu kuitwa maskini" na si lazima awe fukara, kumbuka umaskini na ufukara ni vitu tofauti, unaweza kuwa na mali lakini huwezi kujisaidia kwa mali yako, kwa hiyo wewe ni maskini na wakuonewa huruma. Ufukara ni kitu kingine, sasa kama mnatalka tuibadili mada haya, na ndio maana nikatowa mfano wa niliouona Saudia. Ufukara ni kitu kingine, mfano mzuri ni Tanzania, tunaitwa nchi maskini, lakini tuna mali za kutosha, kwa nini? ni wakuonewa huruma umaskini wetu, kwa ujinga wetu, lakini si wakukosa mali na rasilmali.