Je Ulikueko enzi zetu?

Aventus

JF-Expert Member
Mar 8, 2013
2,011
2,165
ULKUWEPO ENZ HZO
1.Kupakwa jivii kwenye kidonda.
2.kung'olewa jino kwa uzi
3.ubwabwa kupikwa j2 tuuu
4.kidonda kuwekwa unga wa vidonge vya rangi mbili
5.kupamba sebule kwa kadi,pamba na toilet pepa kipindi cha shuguli au sikukuu
6.kunyolewa na mkasi
7.kufunga pesa kwenye leso au pindo la kanga
8.kurewind kanda kwa peni au penseli
9.Nchi nzima kuangalia komando john(anodi la jeni),double impact(van dame mapacha),Rambo na bruce lee
10.watoto wa mtaa mzima kufahamiana kwa kucheza kombolela na kidali poo
11.kuunguzana na tunda ya ubuyu baada ya kuisugua chini
12.kukata ndala iwe kifutio
13.kunyolewa msalaba skuli kama nywele ndefu
14.kuweka viboxbox mgongoni mwa shati la shule
15.kuweka shati la shule blue ili liwe maridadi
16.ubitozi ni kusimamisha kola ya shati
17.ukiandika barua kwa umpendae lazima alama ya kopa na mshale katikati na lazima upulizie kapafyum ya "YU"
18.ukigombana na mtu basi subiria siku ya kufunga shule chamoto
19. Kumpigia demu misele kwao na kutumia kisingizio cha kuomba maji ya kunywa
20. Kwenda kunyosha nguo kwa jirani
21. Kujipendekeza kwa rafiki yako ili ukienda kwao asikutimue kuangalia video
22. Kuacha kuhudhuria tuition ili pesa ukaweke bili sinema
23. Kununua daftari na kulikata katikati then hicho kimini kujaza jina la movie unayoiona then kucompare na wenzio at the end of the year nani katazama movie nyingi
24. Kuvaa tafu-buti na losso kwa wadada kama bonge la ujanja
25. Mjanja kuvaa jeans zenye machata ya chui magotini
26. Kuweka kioo chini ya dawati anapokaa msichana na kumchungulia then kujifanya unaweza kubashiri kavaa chupi rangi ipi
27. Kukaa asseble na lens kwenye jua kali na kuitumia kuwachoma wenzio
28. kunyoa panki na kimemba
ONGEZA
 
mkiwa mnacheza kibaba baba na kimama mama ukiambiwa leo unakuwa mtoto hutaki yaani uko radhi mchezo usichezeke ilimradi uchukue character ya kuwa baba....
 
Back
Top Bottom