Je, ulianza ujenzi ukiwa katika hali gani kiuchumi/ kipato?

Sina familia Niko peke yangu

Umeona hapo tu kwenye andiko langu.?

Anyway, hapo unaweza kupunguza hiyo bili ya kula kazini ni kubwa... ila itategemea na eneo la kazi na mkumbo wa wenzako ofsini.

Ukimaliza kujenga nyumba ya mama, fanya mwendo huo huo 300k kila mwezi iende kwenye ujenzi wako.... ukijibana msosi inaweza kufika 400k.

Ukifanikiwa kuzingatia hilo kwa nidhamu, miaka mitano inatosha kuwa sehemu nzuri kimaisha.
 
Laki7 sio mshahara mzuri ni average mno. Ila kwa hesabu hizo unajitahidi mno. Hapo kazi ni kusave mpk upate hela ya kiwanja cha kueleweka ndio kimbembe ila kujenga utajenga tu na itaisha. Zichange karata vizuri.
 
Habari za Muda Wana JF

Kama Kichwa Kinavojieleza, kumekuwa na mjadala hususani kwa Vijana kuhusu suala la ujenzi, hali inayopelekea wengine kutafuta Pesa kwa njia zisizofaa hususani waajiriwa

Wengi wanatamani kufikia maisha fulani kwa haraka baada tu ya kuajiriwa. Utakuta kijana kaajiriwa si muda mrefu lakini anatamani awe na Usafiri na kumiliki nyumba kipindi hicho hicho. Kitu ambacho kinakuwa kigumu bila kujua walivyonavyo wamestruggle for some years

Je, wewe ulianza ujenzi ukiwa katika hali gani ya kipato mfano mshahara ulikua sh ngap na uliwezaje kuugawanya na kupeleka kiasi kadhaa kwenye ujenzi na kingine kwenye majukumu ya binafsi na kifamilia pia? Karibuni, naamini mchango wako unaeza kuwa msaada mkubwa kwa wengine?
kujenga sio kazi rahisi hasa kama wewe ni muajiliwa wa serikali kwa kuwa kipato ni limited sana inabidi ule nyasi kweli kweli kwa miaka mingi na udharirike sana mtaani.
Nimekuwa kwenye ujenzi kwa miaka sita sasa, nilianza kujenga 2014 kwa chumba na ukumbi, mpaka 2019 nimefanikisha kumaliza kupaua nyumba yote yenye chumba nne, kumbi mbili na jiko la ndani. Sio kazi nyepesi huwezi kula wala kuvaa vzr through out ujenzi, hta hapo bado finishing.. Ila kwa. Mfano mm nimefanikiwa kujenga nyumba mbili kwa wakati mmoja.. In short nimekuwa ni mzee wa top up every year.. Ila nashukuru nipo kwangu na familia.
Ila maisha magumu sana na watu wa ukoo utagombana nao kwa kuwa no msaada unaopeleka huko.
 
Nilianza ujenzi mwezi wa kwanza tu wa ajira nikiwa na mshahara wa laki 2 na nusu, kilicho nisaidia nilikua nakaa kwenye nyumba ya ofisi na msosi ulikua wa ofisi

Kadri siku zilivyosonga na mshahara ukawa unaongezeka na per diem zikaanza hatimae nikamaliza, sasahivi nipo kwangu na kazi ilishaisha.
 
Kujenga kunafaida kama unajua unataka kuishi miaka mingi duniani, lakini kama unajua tunaishi maramoja na sisi ni tunapita hapa duniani, basi hakuna sababu ya kuharibu hayo mamilioni kujenge njiani kwasababu sote tunapita...
 
Umekwisha
 
Naombeni ushauri Jamani napokea 740k take home Nina mwaka mmoja kazini mpaka Sasa nimepanga nimefanikiwa kununua vitu vya ndani tu TV, godoro ,kitanda na n.k na vile vile nilikua nimeanza ujenzi kumjengea bi.mkubwa nyumba yake nimeshapaua

Sasa napata hamasa Sana kuona mwaka unaisha Sina hata kiwanja na akiba yoyote benki naombeni ushauri nataka nipumzike kumalizia nyumba ya mama. Nijikusanye nitafute kiwanja nianze kujenga yakwangu siko comfortable kwenye nyumba za kupanga

Matumizi yangu baada ya kupata mshahara;: Niko dar!

1. Usafiri kwa mwezi 50,000
2. Kula kazini mwezi mzima: 150,000
3. Nyumbani: jioni na weekend: 100,000
4. Kwaajiri ya ujenzi wa nyumbani natuma Laki3 kila mwezi

Kodi kwa Mwezi laki 1 nalipa kwa miezi 6

Napokea hela nzuri kibongobongo! Hata hata inavyoisha sijui!

Naombeni ushauri
Hama unapokaa kapange chumba cha 40,000,save 60 hiyo kwa mwezi kwaajili ya kiwanja.

Tuanzie hapo
 
Naombeni ushauri Jamani napokea 740k take home Nina mwaka mmoja kazini mpaka Sasa nimepanga nimefanikiwa kununua vitu vya ndani tu TV, godoro ,kitanda na n.k na vile vile nilikua nimeanza ujenzi kumjengea bi.mkubwa nyumba yake nimeshapaua

Sasa napata hamasa Sana kuona mwaka unaisha Sina hata kiwanja na akiba yoyote benki naombeni ushauri nataka nipumzike kumalizia nyumba ya mama. Nijikusanye nitafute kiwanja nianze kujenga yakwangu siko comfortable kwenye nyumba za kupanga

Matumizi yangu baada ya kupata mshahara;: Niko dar!

1. Usafiri kwa mwezi 50,000
2. Kula kazini mwezi mzima: 150,000
3. Nyumbani: jioni na weekend: 100,000
4. Kwaajiri ya ujenzi wa nyumbani natuma Laki3 kila mwezi

Kodi kwa Mwezi laki 1 nalipa kwa miezi 6

Napokea hela nzuri kibongobongo! Hata hata inavyoisha sijui!

Naombeni ushauri
Mimi nilinunua kiwanja changu Kwanza ndo nikaanza kujenga nyumba ya wazazi imeshaisha Bado tiles chache wanauwezo wa kukaa.
Kisha nikahama mkoa ambako kuna kiwanja dar. ikabidi ninunue nilikohamia mbeya nikaanza kuwekeza hela kwa watu wa vifaa vya ujenzi WANAOAMINIKA kidogo kidogo kuanzia misumari,cement na nondo baada ya miezi 5 nikaanza ujenzi .sababu nilikua na vifaa vyote ikobaki ikawa Ni kumlipa fundi tu.baada ya miezi 7 nikahamia bila hata Finishing ila panavumilika.
Ushauri wangu mipango ndo dira hakuna hela ndogo
 
Kama unaixh pekee ako jarbu kuminimize matumiz yako hyo pesa unayotumia kiuchumi ni kubwa xana, ukiachana na tabia za kutaka sifa kwamba unaixh vizur xana na malengo yako yanafel bhax utaona mafanikio makubwa. tazama hama nyumba ukapate nyumba ya bei ndogo,chakula punguza hyo laki kwa mlo wa jioni pekee tena kwa kujipikia mwenyewe ni hela kubwa xana kiuchumi, ukiixh hvyo ni uhakika utajenga within xhort period baada ya hapo unakula bata kama kawa maana si ni wa mavumbi na vumbini tutarudi
 
Back
Top Bottom