Je, Uhuru, Haki na Maendeleo vipo CHADEMA?

Amani Msumari

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2016
Posts
1,833
Reaction score
978
Wakuu, kuelekea Uchaguzi Mkuu wa tarehe 28.10.2020, hebu tutafakari pamoja hii kauli mbiu ya CHADEMA: Uhuru, Haki na Maendeleo.

Uzi huu hautalenga kuichambua kaulimbiu hiyo bali utalenga kwenye kuangalia kama kweli kauli mbiu hiyo imekuwa ikitekelezwa kwa vitendo kwenye chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania.

Uhuru na Haki

Wakati bunge la Ndugai linakaribia kuvunjwa, viongozi wakuu wa CHADEMA waliwataka wabunge wao kuacha vikao vya bajeti na kwenda kijikarantini. Huenda hili lilikuwa jambo jema lakini halikupaswa kulazimishwa hasa katika kipindi ambacho wananchi waliwahitaji sana wabunge wao wawatetee kwenye bajeti. Wakati wabunge hao ambao walishavuta posho wakijikarantini, wananchi wao walikuwa barabarani wakitafuta riziki zao za kila siku.

Baadhi ya wabunge waligomea amri hiyo. Sote ni mashahidi kilichowakuta akina Lijualikali, Silinde na wenzao.

Wabunge wa CHADEMA hukatwa shilingi milioni moja kila mwezi kutoka kwenye mishahara yao. Je, makato hayo ni makato ya hiyari ambayo yanatawaliwa na misingi ya haki na Uhuru?

Maendeleo

CHADEMA kama chama kikuu cha upinzani kilipaswa kuonesha kwa vitendo kuwa ndio mbadala wa CCM. Pamoja na ruzuku, michango na miradi, ofisi ya makao makuu ya chama hicho haiakisi dhana ya maendeleo. Wengi wa wabunge wake hawaoneshi ubunifu kwenye majimvo yao ili tuone kwa vitendo kuwa hawa ni watu wa maendeleo.

Je, kaulimbiu yao sio ghiliba kwa wananchi?

Povu, utopolo na ugoro: RUKSAAA

Amani Msumari
Tanga
 
Vingekuwepo Mbowe angepora bilion 8?
 
Uhuru na haki na maendeleo kwao vipo navitawezekana kutokea nakutekelezwa kwa vitendo.Nimiongoni mwamambo ambayo,hayahitaji muujiza kuyatekeleza.Na yayana gharama ,hats ikiwepo ni kwa ajili ya kubadili mifumo michache,kufiki lengo kamili.
 
Sasa unauliza swali halafu unajibu mwenyewe!Sisi tufanyeje?
Kama hayo uliyoeleza ndio kigezo cha kuonesha hakuna haki wala uhuru CDM basi kumbe Chadema wako vizuri kwenye eneo hilo!

Nways,tunachokitaka wananchi ni uhuru na haki zetu za kushiriki kikamilifu katika shughuli zote halali ziwe za kijamii,kiuchumi au kisiasa!Mambo kama ya kina Nusrat Henje,Mawazo,Saanane na kilichompata Lissu lazima yadhibitiwe na chama kitakachounda serikali!

Wananchi wasiwe targeted kwa sababu ya itikadi zao,yaani ukishamjua huyu ni mpinzani na anakukera basi ndio unakuwa mwanzo wa kumsumbua na kumtafutia kesi!Tunahitaji usawa mbele ya mahakama na vyombo vya dola!

Swali langu kwako:Kwanini hoja ya uhuru na haki imepata mashiko sana kipindi hiki?Kwanini watu wanaiunga mkono hoja hii?
Panapofuka moshi basi kuna moto!
 
Hayo niliyoyaandika hujayaona? Yatolee maelezo
 
Kama mmeshindwa kwenye chama kipi kitatufanya tuamini kuwa mkipewa nchi mtatekeleza? Hoja ya haki ba uhuru imeshika Kasi zaidi kwa mafisadi, wakwepa kodi na wavunja sheria wengine. Mimi Kama mwananchi wa kawaida sioni shida yoyote
 
Sasa unauliza swali halafu unajibu mwenyewe!Sisi tufanyeje?
Kama hayo uliyoeleza ndio kigezo cha kuonesha hakuna haki wala uhuru CDM basi kumbe Chadema wako vizuri kwenye eneo hilo!

Nways,tunachokitaka wananchi ni uhuru na haki zetu za kushiriki kikamilifu katika shughuli zote halali ziwe za kijamii,kiuchumi au kisiasa!Mambo kama ya kina Nusrat Henje,Mawazo,Saanane na kilichompata Lissu lazima yadhibitiwe na chama kitakachounda serikali!

Wananchi wasiwe targeted kwa sababu ya itikadi zao,yaani ukishamjua huyu ni mpinzani na anakukera basi ndio unakuwa mwanzo wa kumsumbua na kumtafutia kesi!Tunahitaji usawa mbele ya mahakama na vyombo vya dola!

Swali langu kwako:Kwanini hoja ya uhuru na haki imepata mashiko sana kipindi hiki?Kwanini watu wanaiunga mkono hoja hii?
Panapofuka moshi basi kuna moto!
Kamuulize zitto atakupa majibu kilichompata.
 
Kiukweli hamna ili ni bora tubadili tu, ili tupumue!
 
😂😃 wanataka kuibadilisha nchi nzima wakat wameshindwa kuibadilisha hata ofisi za makao makuu
 
Back
Top Bottom