Je uamuzi huu wa DC wa Mvomero ni sahihi?

sinafungu

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
1,527
865
Nimeshangazwa na hatua aliyoichukua DC wa Wilaya ya Mvomelo Bi Betty Mkwasa.

Nadhani hata katiba ya Nchi inamzuia kufanya hicho alichofanya,kwamba; AMECHIMBA MTARO KUTENGANISHA WAKULIMA NA WAFUGAJI ILI KUSIWEPO MAINGILIANO , nawauliza wadau hili jambo ndio muarubaini wa magomvi kati ya wakulima na wafugaji?
 
nimeshangazwa na hatua aliyoichukua DC wa Wilaya ya Mvomelo Bi Betty Mkwasa. nadhani hata katiba ya Nchi inamzuia kufanya hicho alichofanya,kwamba; AMECHIMBA MTARO KUTENGANISHA WAKULIMA NA WAFUGAJI ILI KUSIWEPO MAINGILIANO , nawauliza wadau hili jambo ndio muarubaini wa magomvi kati ya wakulima na wafugaji....?
kweli ni kama kujenga ukuta kati ya ujerumani magh/mash!
ila alitakiwa kufanya nn?
 
Nimeshangazwa na hatua aliyoichukua DC wa Wilaya ya Mvomelo Bi Betty Mkwasa.

Nadhani hata katiba ya Nchi inamzuia kufanya hicho alichofanya,kwamba; AMECHIMBA MTARO KUTENGANISHA WAKULIMA NA WAFUGAJI ILI KUSIWEPO MAINGILIANO , nawauliza wadau hili jambo ndio muarubaini wa magomvi kati ya wakulima na wafugaji?
Hiyo ndio dawa kwani ng'ombe huwa hawezi kuvuka mtaro,
 
Safi sana mama yetu umeonyesha mfano mzuri, mkuu wa mkoa aliyekuwepo dr..... alishindwa kabisa kuwa mbunifu sasa anabembeleza ajira
 
Nimeshangazwa na hatua aliyoichukua DC wa Wilaya ya Mvomelo Bi Betty Mkwasa.

Nadhani hata katiba ya Nchi inamzuia kufanya hicho alichofanya,kwamba; AMECHIMBA MTARO KUTENGANISHA WAKULIMA NA WAFUGAJI ILI KUSIWEPO MAINGILIANO , nawauliza wadau hili jambo ndio muarubaini wa magomvi kati ya wakulima na wafugaji?
Ni sawa amefanya vizuri, tena yy ni mbunifu saana
 
Dah,sijui kama ni njia sahihi maana njia nzuri ni mazungumzo mezani sio kuwekeana mipaka ndani ya wilaya moja.
 
Kwa jinsi nilivyosikia kwenye taarifa ya habari huo ni uamuzi Wa mahakama na sio DC
 
Dah,sijui kama ni njia sahihi maana njia nzuri ni mazungumzo mezani sio kuwekeana mipaka ndani ya wilaya moja.
Mazungumzo ni mazuri kwa watu wazima. Lakini wachungaji mara nyingi huwaachia watoto wadogo wachunge mifugo na hii inapelekea mifugo kuingizwa mashambani kwasababu hawakuhusishwa kwenye hayo mazungumzo! Dawa ni hiyo ya mfereji ingawa baadhi ya wakulima wanadai hawakuhushishwa na zoezi zima.
 
Nimeshangazwa na hatua aliyoichukua DC wa Wilaya ya Mvomelo Bi Betty Mkwasa.

Nadhani hata katiba ya Nchi inamzuia kufanya hicho alichofanya,kwamba; AMECHIMBA MTARO KUTENGANISHA WAKULIMA NA WAFUGAJI ILI KUSIWEPO MAINGILIANO , nawauliza wadau hili jambo ndio muarubaini wa magomvi kati ya wakulima na wafugaji?
mtaro huo haujachimbwa kwa amri ya Mkwasa umechimbwa kwa amri ya Mahakama hivyo mahakama imeona ni sululisho la mgogoro huo.
 
Huu ni usuluhisho wa mda.
Dawa ni wafugaji kuweka senyenge maeneo yao yote na kuachana na open ranching.
Ng'ombe wakionekana nje ya senyenge utakuwa uchokozi na wataifishwe. Mfereji una haribu mazingira na si salama.
Pia uta saidia kwa maeneo madogo na nighari kwa vijiji vikubwa
 
Ulitaka afanye nini? Watu wanauana na mifugo inauawa,wewe unadhani kipi kingefanyika?
 
Wala hilo siyo suluhisho! Hivi mnafikri kama kule kwa wakulima kuna malisho mazuri, mfugaji atashindwa kuvusha mifugo yake? Ngoja niwashirikishe uzoefu wa kule kwetu ambako ni karibu na game reserves, wakati wa kiangazi vijijini huwa tunaishiwa malisho lakini kwenye GRs unakuta nyasi zinalaliana. Sasa kilichokuwa kinafanyika tulibadilisha mida ya kuchunga ikawa kuanzia saa 12 jioni tunakuwa tunazuga kuchunga jirani jirani na GR, mpaka inafika saa 2 usiku unakuwa umeingia kwenye GR mpaka inafika saa 10 usiku ng'ombe wanahema tu maana wameshiba ile mbaya unarudi zako home kulala asubuhi unawapeleka tu kwenye maji. Sasa kutokana na huo uzoefu mfugaji hashindwi kufukia mtaro kwa upana wa mita moja na kupitisha mifugo yake hata kama itakuwa usiku!

Suluhisho la migogoro hii ya wakulima na wafugaji ni kwa wanasiasa kukaa mbali na hii migogoro wawaachie wataalam wa usuluhishi wa migogoro wafanye kazi yao! Kwa hili la Betty linaweza kuchochea uhasama baina ya wakulima na wafugaji na wakaishi kama MWARABU na Myahudi! Hapo naomba nikiri kabisa kwamba ubunifu ni zeero (kwa sauti ya Magufuli). Tufike mahali tuwe wawazi katika hili la wakulima na wafugaji ya kwamba wakorofi ni wakulima, maana wao wakitaka kupanua mashamba yao ardhi inayoangaliwa ni ya mfugaji, wao wanaona kama wafugaji hawajui kuitumia ardhi! Serikali ifike mahali iwatungie sheria kali kama sharia hawa wakulima ya kwamba hakuna mkulima atakayeruhusiwa kupanua shamba lake na kila mkulima alime kitaalam kabisa (afuate kanuni za kilimo bora). Sasa hivi unakuta kakulima kajinga kanalima ekari 50 kanavuna magunia 40 ya mahindi, kumbe mavuno hayo kangeyapata kwa kulima ekari 3.tu tena huenda kangevuna magunia 45.badala ya 40. Kwa kufanya hivyo ekari 47 zingebaki kwa ajili ya mfugaji!! Basi badala ya ekari 3 kape ekari zingine za ziada 7 ili kalime na mazao mengine, hivyo ekari 40 zingebaki kwa ajili ya mfugaji!!

Sikubaliani na suluhisho la kuwatenga watu kwa misingi ya ukulima na ufugaji! Wote tunategemeana!!
 
Nimeshangazwa na hatua aliyoichukua DC wa Wilaya ya Mvomelo Bi Betty Mkwasa.

Nadhani hata katiba ya Nchi inamzuia kufanya hicho alichofanya,kwamba; AMECHIMBA MTARO KUTENGANISHA WAKULIMA NA WAFUGAJI ILI KUSIWEPO MAINGILIANO , nawauliza wadau hili jambo ndio muarubaini wa magomvi kati ya wakulima na wafugaji?

Mkuu umesema umeshangazwa na DC Mvomero kuchimba huo mtaro na kwamba haikubaliki kikatiba (kifungu hujataja lakini), sawa tumepokea mshangao wako. Nilitegemea baada ya kumaliza kushangaa ungetoa mapendekezo yako ili DC na watendaji wa Mvomero wayasikie, lakini naona umeishia kulalamika.

Nimebahatika kufika Mvomero na hata eneo husika nimefika na ukweli ni kwamba migogoro hii imesababisha hasara kubwa na vifo vya wananchi kwa zaidi ya miaka mitano sasa na hakuna ufumbuzi wa kudumu uliopatikana. Kwa kuwa mzizi wa tatizo hili ni kugombea matumizi ya ardhi kati ya wafugaji na wakulima basi huyu DC na timu yake (kumbuka pia maamuzi haya yalifikiwa hivi majuzi baada ya watu na mifugo kuuwawa kikatili, na Waziri Mwigulu akatembelea eneo husika) kukutana na wananchi wa maeneo hayo na kuafikiana kwamba eneo lipi liwe ni la kilimo tu, na lipi liwe ni la kuchungia mifugo. Baada ya maafikiano hayo ikatafutwa namna ya kuhakikisha mifugo (ambayo ndiyo inayotembea, na wafugaji ni wajeuri kwa sababu wanatoa sana rushwa) haivuki na kuingia eneo la mashamba. Kwa maoni yangu mkuu huyu wa Wilaya na timu yake wamekuja na suluhisho sasa kama lifanya kazi au la hilo ni jambo lingine.
 
Mie nampongeza sana huyu Mdada,maana pale wanaume wenyewe wamehsindwa kuwa na njia mbadala.

Hiyo ni hatua nzuri kwa Mwanzo,asikudanganyeni mtu aisee wafugaji watemi saana,wafuga kizamani halafu wabishi kweli kuandaa malisho ya mifugo yao.

Unapokuwa huna njia ya kudum basi tumia hata ya muda,issue hapa sio ubaguzi issue ni kuzuia maafa ya hawa viumbe ambao wao wenyewe wanabaguana.
Ukitaka kuwa muungwana saana kwenye tension kama hizo ndio maana wakuu wa mikoa kibaoo ngoma iliwashinda.
Bora ulaumiwe kuokoa maisha ya wengi
 
Back
Top Bottom