Baada ya Rais Samia kufungua soko la nyama falme za Kiarabu. Je, wanaopuuza zoezi la uwekaji hereni mifugo ni wasaliti wa Rais aliyewateua?

Jabali la Siasa

JF-Expert Member
Jul 10, 2020
2,530
2,141
Nawasalimu kwa Jina la JMT,

Tanzania kuna mambo ya kubishaniwa ila sio uhodari,Umakini na Uchapakazi wa Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan.

Mtakumbuka hivi majuzi Rais Samia alifanya ziara katika nchi za falme ya kiarabu (UAE) akihangaika kuifungua Tanzania ili kuwaletea Watanzania anawaongoza mendeleo endelevu.

Moja ya jambo kubwa la mafanikio ya ziara hiyo ni kufanikiwa kuzishawishi tena nchi hizo za kiarabu kununua ngo'mbe mbuzi na kondoo toka Tanzania.

Mtakumbuka, ni karibu nusu karne nzima waarabu waligoma kula nyama toka Tanzania wakihitaji wauziwe viumbe hao wakiwa hai ili kwa imani yao wao wenyewe wawapeleke "Kibra " yaani wawachinje wao.

Tanzania wakati wote imeshindwa kutimiza takwa la mifugo yake kuwa na utambuzi,unaotambulika kitaifa na kimataifa, yaani kuwa na hereni zenye "Bar code " kama ilivyo kwa wenzetu Uganda.

Tanzania kwa sasa inakadiriwa kuwa na mifugo inayofikia milioni 50,kama kadirio la chini na iko nafasi ya pili baada ya Ethiopia Africa.

Endapo Tanzania itafanikiwa kusajili walau 70% tu ya mifugo yake basi mifugo hii itachangia kwenye pato la Taifa kwa zaidi ya 20%, karibu sawa na sekta ya madini.

Kama kunajambo Rais Samia atapiga bao marais wote waliomtangulia basi ni hili la 'Livestock identification ' kwani bei ya ngo'mbe itapaa juu mno, wafugaji wanakwenda kuwa billioners.

Mfugo wenye " Id " anakuwa tayari ni "International based " anaweza kuuzwa kokote duniani, tofauti na ilivyo sasa wanaishia tu pale Pungu au kale kamnada kakwampalange.

Fankly, Sijawahi kmpongeza Ndg yangu Mhe Mashimba Ndaki waziri wa Mifugo na Uvuvi kwenye hili wacha niseme ameupiga mwingi kwelikweli,na anastahili heshima sana pamoja na team yake yote.

Kinachonisikitisha zaidi ni kuona baadhi ya wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi kutolipa uzito unaostahili zoezi hili litakalo maliza migogoro ya muda mwingi kati ya wakulima na wafugaji na kuwaacha wafugaji wakiwa matajiri wa kutupwa.

Napendekeza uwekaji wa hereni uwe ndio kipimo cha utendaji wa viongozi hao.

Kazi na iendelee,#Samia5Tena


IMG_20220702_093355_3.jpg

Huyu ni ng'ombe mwenye hereni huko Mbarali Mbeya,

Wacha nimpongezi Mhe RC wa Mbeya, Mhe DC wa Mbarali na Mhe Mkurugenzi wa Mbarali kwa kumsaidia vema kazi Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan,
 
Binafsi nasikitika sana, hilo soko huwa lipo miaka mingi sana, lakini je? hawa wabongo wanaweza kuingia kwenye hii biashara au iko monopolized na watu kadhaa matycoon wanaofanya umafia na kuhakikisha wengine hawatoboi.

Inawezekana viongozi baadhi wanajitahidi kufungua njia kwa watanzania wengi kunufaika lakini wanasahau kwenye ground mambo hawajaweka sawa ili watanzania wasipate vikwazo.
 
mifumo kwenye ground sio rafiki wa watanzania wakawaida na wachini kuweza kupenya na kufanya hii biashara.

tumeruhusu mpaka matajiri kutoka hukohuko UAE kuja hapa na kuwekeza kwenye hiyo biashara kwa niaba ya wenzao waliopo huko, matokeo yake ni kulalia bei na kunyanyasa wazawa aka wafanyabiashara wa ndani.
 
mifumo kwenye ground sio rafiki wa watanzania wakawaida na wachini kuweza kupenya na kufanya hii biashara.

tumeruhusu mpaka matajiri kutoka hukohuko UAE kuja hapa na kuwekeza kwenye hiyo biashara kwa niaba ya wenzao waliopo huko, matokeo yake ni kulalia bei na kunyanyasa wazawa aka wafanyabiashara wa ndani.
Shida ni hao watu wa chini wengi hawafahamu mambo mengi
 
Shida ni hao watu wa chini wengi hawafahamu mambo mengi

Hatupaswi kuendelea kuamini hawafahamu chochote, mamlaka zinajukumu la kuwafanya wafahamu chochote ili waweze kujiajiri na kuajiri wengine.

Tunapolalamikia tatizo la ajira kwa watu wetu ni pamoja na kuwapa mbinu na urahisi wa mitaji ili waweze kujiajiri na kuajiri wengine, balozi zetu zinapaswa kuweka nguvu sana kuhakikisha vijana na watu wote huku Tanzania wanajua hizo fursa na namna ya kupenya ikiwa pamoja na kuwasimamia wasipigwe. Huku nyumbani serikali ihakikishe milango iko wazi.
 
hatupaswi kuendelea kuamini hawafahamu chochote, mamlaka zinajukumu la kuwafanya wafahamu chochote ili waweze kujiajiri na kuajiri wengine.

tunapolalamikia tatizo la ajira kwa watu wetu ni pamoja na kuwapa mbinu na urahisi wa mitaji ili waweze kujiajiri na kuajiri wengine, balozi zetu zinapaswa kuweka nguvu sana kuhakikisha vijana na watu wote huku Tanzania wanajua hizo fursa na namna ya kupenya ikiwa pamoja na kuwasimamia wasipigwe. Huku nyumbani serikali ihakikishe milango iko wazi.
Kuna kitu unacho aise, nimekuelewa
 
Kwanza mtoa mada ni mjinga asiejua falme za kiarabu . kwa ufupi ukiwa falme za kiarabu kuna mifungo kama mbuzi kondoo na ngombe kuku ni wengi sana inategemea na weww unataka mbuzi au kondoo kutoka nchi gani, mbuzi huko au kondoo ni rahisi kuliko tanzania nimeishi huko miaka 30 ninaijua vizuri.

Kila nchi duniani inaleta mifugo na matunda wanashindana. falme za kiarabu haitaji saana tanzania kwa mifugo yake na matunda yake wale wana kilakitu mungu kawajaalia kuna matunda huko yapo tanzania hakuna wale wanaishi pepo ya ulimwenguni.
 
kwanza mtoa mada ni mjinga asiejua falme za kiarabu . kwa ufupi ukiwa falme za kiarabu kuna mifungo kama mbuzi kondoo na ngombe kuku ni wengi sana inategemea na weww unataka mbuzi au kondoo kutoka nchi gani, mbuzi huko au kondoo ni rahisi kuliko tanzania nimeishi huko miaka 30 ninaijua vizuri. kila nchi duniani inaleta mifugo na matunda wanashindana. falme za kiarabu haitaji saana tanzania kwa mifugo yake na matunda yake wale wana kilakitu mungu kawajaalia kuna matunda huko yapo tanzania hakuna wale wanaishi pepo ya ulimwenguni
Kwahiyo Rais Muongo?
 
Back
Top Bottom