Je, Tutsi ni moja ya makabila ya Tanzania?

Je, Tutsi ni moja ya makabila ya Tanzania?

kama unasema ni madaktari, walimu, na wengine wana nyadhifa kubwa kuliko hizo.....huoni kuwa wanatumikia taifa la Tanzania na wenye kufaidika ni watanzania? haya mambo usiumize kichwa sana cha msingi jua tu raia wa Tz kwani walizaliwa huku(kwa waliozaliwa) na endapo kuna waliongia kinyemela toa taarifa haraka kwa maofisa wa idara ya uhamiaji.
 
Mbona kuna wahaya wengi tu Kigali na hakuna anayewafuatilia...
Kifupi ni kwamba Wanyarwanda wanaangalia unaifanyia nini Rwanda na sio Rwanda inakufanyia nini...
Watanzania tujifunze kufanya kazi...
Wote ni waafrika
 
Hakuna kabila linaloitwa tutsi, tutsi ni ethinic group na sio kabila
 
Hapana, hapo umekosea, tena sana tu, huwezi kufananisha Rwanda na Tanzania au Rwanda na Kongo, kwa maana Tanzania kuna lugha nyingi kwa mfano lugha ya kindengereko siyo sawa na lugha ya Kimasai lkn Wanyarwanda wote wanaongea lugha moja kwa kifupi hakuna lugha ya kitusi wala ya kihutu wote wote wanaongea lugha moja tu iitwayo Kinyarwanda, na wana utamaduni mmoja tu!
Lakini unajua kwamba socio-economic activities ndio hasa zinazofanya utofauti wa makabila? Lugha ni sehemu ndogo sana ya utambulisho wa kabila.
 
Back
Top Bottom