Je tunao waandishi wa habari Tanzania?

bulunga

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
303
49
Leo nimeshuhudia wanajeshi wakitoa taarifa kwa WAANDISHI wa habri wa vyombo mbalimbali, nilishangaa sana kuona waandishi wakishindwa kuhoji maswali muhimu na ya msingi hasa baada ya kupata majibu ambayo hayakuwa ya kuridisha kutoka kwa wasemaji wa jeshi.

Kuna wakati msemaji wa jeshi alisema kitu kama jokes, ajabu waandishi wetu, majority yao wakawa wana Smile tu kama kwamba hawakuwa kazini na issue hiyo ilikuwa serious na walitakiwa kupewa majibu ya kueleweka.

Nilimuona Joyce Mhavile nilishangaa hakuuliza hata swali moja ingawa kwa mtu kama yeye na wadhifa wake nilitegemea kuuliza swali au maswali ambayo yangeliwalazimisha wanajeshi kutoa majibu ya uhakika.

Mfano msemaji wa jeshi alisema kuwa milipuko haikutokea tena Mbagala kama kwamba ilikuwa ni jambo la mafanikio kwao kwa vile limetokea sehemu tofauti na mazingira tofauti, Waandishi hao hao walishindwa kuhoji kwa nini mambo haya yatokee ikizingatiwa kuwa zama hizi maswala ya SAFETY na ACCIDENT protection, RISK assesment ni vitu muhimu sana sana, msemaji mmoja alisema eti ajali kama hizi ni hutokea na hazina kinga, akatoa mfano nchi kama Ethiopia, Msumbiji etc.

Akasema hata uki search kwenye GOOGLE utaona ajali nyingi tu zimetokea, SO inaonekana kuwa ni kitu ambacho kinatarajiwa kutokea wakati wowote, je ni sahihi kuwa ajali ikitokea sehemu nyingine duniani tusishangae ikitokea hapa, aliendelea kujisifu kuwa sehemu zingine huwa ni SIRI wala wananchi na vyombo vya habari hawaelezwi, nimeshindwa kuelewa hawa waandishi sijui walikwenda hapo kufanya nini ( labda kugombania business card za maafande kama tulivyoona)
 
Kama vyombo vya habari vyenyewe haviko huru unategemea wandishi watakuwa huru mkuu wangu? Wapo huru na vimbelembele kuripoti na kuonyesha matukio yanayotokeanchi nyingine lakini siyo tanzania.

Hatuna vyombo huru vya habari, na rushwa ndiyo imeota mizizi, habari za mafisadi ndiyo zinapewa vichwa vya habari na si vinginevyo. Kwani wapo tayari kuhonga kuliko wengine.

Jambo lingine misha hara wanayolipwa wandishi ni midogo so wapo tayari kujazia kwa kutumia mianya mingine hasa kutoka kwa mafisadi, inabidi wa waabudu mafisadi wapate kuendesha maisha yao kaka.
 
Hatuna vyombo vya habari Tanzania. Ni magenge ya reporters tu wanaoweza kuandika kama vile 'Rais alisema......', 'Waziri Mkuu aliendelea kusisitiza ...', n.k.

Haka kanchi kameoza. Kila kitu feki.
 
Waandishi wa habari wana utaratibu wa kudai posho kama ukiwaita.........Na posho huwa zinatolewa baada ya kikao. Ni nani huyo wa kutia mchanga kwenye kitumbua chake?
 
ni kweli hakuna, unajua ni kwanini magazeti mengi huwa wanaandika habari sawa, hapa kuna makundi mawili moja la kutetea Ufisadi Magazeti yake ni Rai, Mtamzania, HOJA, Dira, ya Kutetea serikali hata kama kuna dosari ni, Uhuru, habari leo Daily News, ya kupambana na mafisadi ni Raia mwema na Mwanahalisi, masilahi binafsi Tanzania Daima, Kulikoni , Gazeti WAZI ambalo HALINA upande ni Mwananchi Pekee.

Vijigazeti vingine ambavyo vina habari za Uchochezi wa kidini ni WAKAti Alnuur, na Zanzibar leo, wanahabari wote huwa wanakutana pale IPS na EMPRESS chini ya miti na kuhulizia habari ya kuandika, anayepata habari mapema huwa anafanya dili ya kuwauzia wenzao, ndio maana hakuna habari za kiuchunguzi kwa kuwa wanakuwa hawana huhakika na kazi zao, hivyo hofu yao ni kuandika habari halafu ikawegeuka.

Anayebishi Kuhusu hili aje Pale kijiweni IPS kwa mashoe shine Jtatu utawaona wako wengi sana wengine hata hawana hadhi ya kuitwa mwandishi. Nchi za watu Mwandishi ni lazima awe na taaluma ya sheria, ili hata aweze kuripoti na kuuliza mashwali habari za kiuchunguzi.
 
ni kweli hakuna, unajua ni kwanini magazeti mengi huwa wanaandika habari sawa, hapa kuna makundi mawili moja la kutetea Ufisadi Magazeti yake ni Rai, Mtamzania, HOJA, Dira, ya Kutetea serikali hata kama kuna dosari ni, Uhuru, habari leo Daily News, ya kupambana na mafisadi ni Raia mwema na Mwanahalisi, masilahi binafsi Tanzania Daima, Kulikoni , Gazeti WAZI ambalo HALINA upande ni Mwananchi Pekee, vijigazeti vingine ambavyo vina habari za Uchochezi wa kidini ni WAKAti Alnuur, na Zanzibar leo, wanahabari wote huwa wanakutana pale IPS na EMPRESS chini ya miti na kuhulizia habari ya kuandika, anayepata habari mapema huwa anafanya dili ya kuwauzia wenzao, ndio maana hakuna habari za kiuchunguzi kwa kuwa wanakuwa hawana huhakika na kazi zao, hivyo hofu yao ni kuandika habari halafu ikawegeuka.

Anayebishi Kuhusu hili aje Pale kijiweni IPS kwa mashoe shine Jtatu utawaona wako wengi sana wengine hata hawana hadhi ya kuitwa mwandishi. Nchi za watu Mwandishi ni lazima awe na taaluma ya sheria, ili hata aweze kuripoti na kuuliza mashwali habari za kiuchunguzi.
Naifanyia kazi kabla sijafika Bongo!
Ahsante member.
 
Upande wa magazeti tunaweza kuwa na waandishi wachache na wanaoweza kuandika wakiwa objective, mfano baadhi ya waandishi wa gazeti la Mwananchi, ukija upande wa waandishi wa elctronic media hasa TV na redio utashangaa, huku kumejaa makasuku waliokaa kimaslahi na utawagundua kwa maswali yao, mfano ' mhe, ww ulikuwa unasemaje kuhusu suala la kuwepo kwa udini hapa nchini'
 
Tunapoelekea inabidi tuweke Qualification halali za uandishi wa habari na ziwe zinahakikiwa hasa. Leo tna waandishi na watangazaji wasiojua maadili wengi tu. Waandishi wa habari wengi wa Tanzania ni wale waliofeli either form 4 au 6.

Wakashindwa kujiunga vyuo vikuu. Wanasoma vicertifcate one year eti mimi mwandishi wa habari. Mimi presenter wa radio or tv. Wengi hawana tofauti na wamachinga.

Ndio maana hata ukipita pale kwenye kijiwe chao cha umbea IPS hawatofautiani na mashoe shiners. Waandishi walioenda shule sawasawa wakiandika utaona tu tofauti.
 
Tuna aandishi uchwara tu wenye njaa na tamaa, Lakini waandishi hasa wengi wameshatangulia mbele ya hakhi.
 
mkuu ni kweli siku hizi hakuna waandishi bali wapo waganga njaa, sababu mtu ameshindwa katika taaluma fulani au kielimu lakini sababu anajua kuelezea kitu kwa maandishi basi anajaribu kui ngia katika fani ya uandishi kwa kusopma kozi fupifupi na kisha akijua kuandika habari na akajaribu siku kupata wenyewe wanasema kigongo basi anajiona yeye tayari kawa mwandishi.

Kwa ufupi tasnia ya habari imeharibika siku hizi watu wanashindwa hata zile hatua tano za uandis uandishi wa habari, wanakurupuka tu na hata hao ambao twaweza sema walikuwa waandishi mahiri siku hizi wamekuwa watu wa posho aka vibahasha hivyo wamepindisha maadili yote ya uandishi.
 
Niambie ni taaluma ipi nchini inafanya kazi kwa ufanisi? tuaona Madaktari wanavyotoa operation na kusahau mikasi tumboni au badala ya kichwa miguu! Wahandisi wanavyoangusha Majengo na barabara dhaifu!

Wanasheria wanavyoshindwa kuelewa mikataba ya Kiingereza na kuingiza nchi katika madeni makubwa! wachumi walivyoshindwa kabisa kuweka mikakati ya kuinua uchumi na tunaendelea kuwa kati ya nchi 10 Masikini duniani!

Maafisa Kilmo hamna kitu! sasa unategemea waandishi watafanya miujiza ipi?! kwanza hakuna specializations, Niambie ni mwandishi gani engineer, Chemist, Political analyst, finances, lawyer?! wenzetu wamefikia hapo! ikitokea Chemicals zimechafua mazingira, kuna waandishi waliobobea katika kemia za mazingira wanaweza kushoot maswali kulingana na uelewa wa field!

Wanaweza amua kujifunza, Ukitaka kujua mambo ya siraha si lazima uwe mwanajeshi au polisi lakini kupitia sources mbalimbali
 
Back
Top Bottom