Je, tujifunze kufikiria tofauti?

OMOYOGWANE

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
3,601
9,063
Kufikiria tofauti ni kitendo cha kuwa na wazo tofauti na lile lililozoeleka siku zote kwa watu wengi.

mfano kama watu wamezoea kupitia mlangoni basi wewe ihangaishe akili yako kubuni njia nyingine ya kutokea! Kwa maoni yangu nadhani kufikiria tofauti ndio chanzo cha mawazo mapya na ubunifu,

Changamoto ya kufikiria tofauti, Jamii inayotuzunguka inaweza kuyachukulia mawazo ya mtu aliyefikiria tofauti kama vile ni ya kiuwendawazimu au ya mtu asiye na akili timamu,

Lakini nawaza hivi inawezekana kutengeneza kitu au kubadilisha mfumo flani bila kufikiria tofauti?

Kwa mfano washindi wa shindano la STORY OF CHANGE wa kwanza yeye alifikiria tofauti na ilivyozoeleka siku zote kwa watu wengi, yeye kaleta wazo kuwe na dira ya maendeleo ya Taifa, mshindi wa pili yeye kafikiria tofauti kwa kuandika makala inayohusu kiti kizito, wa tatu yeye kafikiria tofauti kwa kupendekeza mfumo mpya wa ukusanyaji kodi kwenye masoko makuu,

Ajabu ni kwamba maandiko yao hayakupata comments, votes nyingi wala like za kutosha hii ni kwa sababu walifikiria tofauti na ilivyozoeleka kwa wengi,


Je, kuna haja ya kuihangaisha akili kufikiria tofauti ktk mambo mbalimbali tofauti na ilivyozoeleka kwa wengi?
 
b556b7a8635de356da0adc21fbf7b765.jpg
 
Back
Top Bottom