Je, TL angetulia angefaa kuwemo ktk timu makinikia?

njeeseka

JF-Expert Member
Oct 19, 2012
1,371
979
Tatizo Jamaa domo tu, lakin kuna wakati ana point, nadhani kipindi hiki cha kuunda First Eleven ya makinikia na Barrick Kocha angeweza kumuingiza ila kwa harakati zake mmh sijui.
Au mnaonaje tushauri awepo nn?

Hebu wataje wengine wanaofaa kuwemo katika hiyo timu.
 
Kwenye Timu ya majadiliano na kuondoa mzizi wa fitina Tundu Antipas Mughwai Lissu na yeye aingizwe humo.

Hoja tunazosikia Bungeni kuhusu kuibiwa madini akaziweke sawa mezani kufikia muafaka kwa faida ya Taifa na watanzania kwa ujimla
 
FaizaFoxy Bi mkubwa huyo jamaa angekuwa tahira kama unavyodai asingefungwa na utawala wa Mkapa kwa kinachowasumbua leo.
Laiti wangelimuelewa tusingekuwa na matatizo haya leo.

Tatizo la nchi hii ni kumfanya Rais kuwa mungumtu asiyekosolewa na ndicho kilichotufikisha hapa leo, Awamu ya tatu wangemsikiliza huyo unaemwita taahira wala tusingehangaika.
 
Ishu sio politicians swala ni uwezo maana hata huyo Prof Kabudi sasa ameingia katika siasa, swala hapa ni uwezo wa ku counter attack timu pinzani. Shauri nani aingie
Issue ni uwezo na Uzalendo...Si lazima Kabudi kuingia anaweza akafuatilia tu...nchi hii ni kubwa na ina wataalamu wabobezi....majaduliano sio kelele za majukwaani....I wonder Wanasiasa wanavyoropoka kwa kusoma abstract za reports.
 
Wafuatao waongezwe katika timu yetu ya makinikia ili wakapambane na wazungu
1.Bashite
2.Gumbo
3.Kessy MB
4.Lusinde MB
5.Faiza

Hii ni timu ya ushindi.
Ha ha haaa wewe mchochezi walah
 
Lakini pia kumuacha kwenye timu yetu ya wataalam hatumkomoi bali tunaikomoa taifa letu.
Najuwa alipowaita uchwara aliwakera to the maximum lakini uzalendo wake hauna shaka.
 
Yule taahira anabwabwaja hovyo. Hana jipya.
wengi wenu huwa mnatimiza wajibu kipindi hiki ni kipindi cha toba kwanini umzushie mwenzio kuwa ni taahira wewe ukiitwa kilaza utapenda?Mbona unaaribu funga yako kwa siasa uchwara ni vyema kipindi hiki ukajiepusha na maneno ya kuudhi
 
Lisu kaumbuka sana yeye alisema tutashitakiwa na tutalipa hela nyingi kwenye macampun ya madin wakati wahusika wenyewe wa madini wamekubali sasa hapo lisu na mtu gan ktk nchi hii?
 
Bi mkubwa huyo jamaa angekuwa tahira kama unavyodai asingefungwa na utawala wa Mkapa kwa kinachowasumbua leo.
Laiti wangelimuelewa tusingekuwa na matatizo haya leo.

Tatizo la nchi hii ni kumfanya Rais kuwa mungumtu asiyekosolewa na ndicho kilichotufikisha hapa leo, Awamu ya tatu wangemsikiliza huyo unaemwita taahira wala tusingehangaika.
Wagumu wa kuelewa wepesi wa kusahau mambo wasamehe hawajui walisemalo
 
Back
Top Bottom