Je Tido alianzisha safari ya kifo cha TBC? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je Tido alianzisha safari ya kifo cha TBC?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by HT, Dec 30, 2011.

 1. HT

  HT JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2011
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 1,899
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Wapenzi wana JF, wote ni mashuhuda wa jinsi RTD kisha TVT na then TBC ilivyonawiri kiteknolojia na hilo halina ubishi. Pongezi kwa waliohusika akiwemo ndugu Tido. Lakini pia tumeona kupotea kwa vipindi vinavyokuwa na sura ya kitaifa na matokeo yake vipindi vingi vimekaa kibiashara na hata ki clouds clouds hivi.
  TBC imepoteza mvuto kama televisheni ya kitaifa.
  Hoja ninayoleta je ni Tido aliyeanzisha safari ya kifo hiki kwa mageuzi yake? Tufanye nini kuirudisha TBC ktk mstari unaoipasa?
   
 2. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #2
  Dec 30, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  ndiyo dawa ya unafiki....ife kabisa
   
 3. M

  Mwanawatu Member

  #3
  Dec 30, 2011
  Joined: Dec 19, 2011
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lugha inayotumiwa na T. Muganyizi kama ingekuwa inaeleweka na wengi, ingetufaa sana katika kuchangia/kuelewa mchango wake. Tafadhali tusaidie katika hili.
   
 4. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #4
  Dec 30, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,902
  Likes Received: 5,364
  Trophy Points: 280
  si tido aliyeamuru matangazo ya tbc yakatwekatwe wakati wa ufunguzi wa kampeni za CDM 2010?
   
 5. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #5
  Dec 30, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,206
  Likes Received: 3,828
  Trophy Points: 280
  Mwambie Mshana afanye kazi ya habari na sio CCM. TBC imekufa, haina la maana tangu tido aondoke. Hopeless-
   
 6. a

  adolay JF-Expert Member

  #6
  Dec 30, 2011
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,595
  Likes Received: 3,071
  Trophy Points: 280
  Ipo kisiasa zaidi na si kitaifa
  Ipo kutekeleza maelekezo ya wanasiasa zaidi kuliko uzalendo na wazalendo
  Ipo kifisadi zaidi na si kitaaluma wala kimaadili
  Ipo kukidhi zaidi matakwa ya watawala na si ya wanyonge watawaliwa
  Haiwakilishi wazalendo kwasababu inatii maelekezo ya viongozi wasio na uzalendo
   
 7. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #7
  Dec 30, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  TBC ni idhaa ya Taifa tukamaanisha kuwa ni ya umma kwa hiyo inatakiwa ifanye mambo yake kiumma na sio kwa ajili ya kikundi cha watu wachache

  tutambue kuwa si wananchi wote wapo ktk vyama kwa hiyo kama ni idhaa ya Taifa ibebe sura ya Taifa

  ndio maana hata Tido yey hakuwa akipendelea pande zozote zile kwani kila mtu alikuwa na haki ktk Idhaa ya Taifa

  lakini kama wasemavyo wengi kuwa imekuwa ni ya chama zaidi kuliko Serikali na watu wake yaani umma
   
 8. m

  mchambakwao Member

  #8
  Dec 30, 2011
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 77
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wakuu,maamuzi ya kisiasa na utalaamu ni vitu tofauti.Mi nilitegemea TBC1 kwa kuwa ni tv ya kitaifa lakini ukiangalia coverage yake ya habari zipo juu juu.Mfano habari ambayo ni ya kitaifa ina nusu saa tu,mbali na kupewa ruzuka za kujiendesha bado tu wanaweka biashara mbele.
   
 9. Mamaya

  Mamaya JF-Expert Member

  #9
  Dec 30, 2011
  Joined: Jul 4, 2011
  Messages: 3,726
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Hakuna siku tbc watasoma taarifa ya habari ikose kasoro hasa matatizo ya kiufundi kwenye kurusha habari. Huwa najiuliza wanakuwa hawajaiandaa au ni nini?
   
 10. HT

  HT JF-Expert Member

  #10
  Dec 30, 2011
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 1,899
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  enough of lawama. Hatuwezi kuendelea na lawama... Tufanye nini sisi kama wenye-nchi????
   
 11. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #11
  Dec 30, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160

  bila tbc KUWA CHOMBO CHA UMMA NA SIO CHOMBO CHA SERIKALI haitafika popote zaidi ya kutetea CCM
  waige mfano wa KBC, SABC,BBC vinamilikiwa na umma hivo utendaji wake unaratibiwa na umma na serikali inakuwa haina maamuzi kuhusu utendaje wake na haiwezi kuwaingilia.kinakuwa chombo huru na isiwe chini ya wizara yoyote au ofisi ya waziri mkuu
  na mtendaji wake anatakiwa achaguliwe na umaa au bunge inaweza chukua nafasi ya kuchagua mtendaji na wajibike kwa bunge
  MSHANA kabanwa na magamba hana sauti bali kutangaza wanayotaka na hii ni hatari ktk tasnia ua uhuru wa habari.
   
 12. k

  kaeso JF-Expert Member

  #12
  Dec 30, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 551
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nadhani Tido aliiweka TBC vizuri na ingeendelea kuwa chini yake nadhani hivi sasa tusingekuwa tunaongea haya.
   
 13. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #13
  Dec 30, 2011
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Watafute na kuajiri mkurugezi mbunifu na waache siasa.
   
 14. g

  goodlucksanga Senior Member

  #14
  Dec 30, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ki clouds clouds hivi.......inamaana kwamba ni WAMEKAA KINAFIKI KINAFIKI TU....!!
   
 15. herrypeter1

  herrypeter1 JF-Expert Member

  #15
  Dec 30, 2011
  Joined: Jan 17, 2009
  Messages: 224
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni tz bana TUANAIPENDA
   
 16. M'Jr

  M'Jr JF-Expert Member

  #16
  Dec 30, 2011
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 3,539
  Likes Received: 152
  Trophy Points: 160
  Mi nafikiri tatizo linaanza kwenye serikali yenyewe, pale inapotaka TBC ijiendeshe kama taasisi. Unajua from what i know kwenye nchi nyingine kuna taasisi ambazo huwa haziachwi kabisa zikaingiliwa na soko huria au zikakaa kibiahsara kasoro hapa kwetu.

  Sasa, kwa hali ilivyo sitashangaa sana kama sasa watakuwa na vipindi vya Lottery tu au utasikia wameanzisha Fiesta 2 ili wapate pesa za kujiendesha. Lakini kuna swali la msingi la kujiuliza, pesa wanazozitafuta kwa nguvu hivyo zinaenda wapi? Ikumbukwe Mishahara ya wafanyakazi wote inatoka Hazina (Tunawalipa sisi kwa kodi zetu), mipango yote ya maendeleo ya inaingizwa katika bajeti ya Wizara ya Habari na Vijana (Kutoka kwenye bajeti kuu)

  Nafikiri ni lazima tuilazimishe ibadilike, maana kama ni ya kwetu si ndio tunatakiwa kuisemea?
   
 17. MJINI CHAI

  MJINI CHAI JF-Expert Member

  #17
  Dec 30, 2011
  Joined: Dec 12, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 587
  Trophy Points: 280
  tido ndiye aliyewafikisha hapo walipo wengi wetu hawajui haya mambo......Alifuta jina RTD na kuwa TBC kwa kile ambacho alisema kwenda na wakati....!!!!!!........Aliitoa RTD serikalini na kuidanya Taasisi......!!!!!! Aliingia mkataba na wachina wa miaka 20 na wachina wafanye matangazo yao na kisha baada ya miaka hiyo 20 watatuachia mitambo...!!!!!!! Alikuwa anajichotea mshahara wa Tshs milioni 12 kwa mwezi lakini alikuwa anachukua Tshs milioni 3 zilizo baki alikuja kulipwa baada ya mkataba wake kwisha.......ameiweka TBC pabaya..........Natamani tuwe kama wachina TIDO ahukumiwe........
   
 18. a

  adolay JF-Expert Member

  #18
  Apr 1, 2012
  Joined: Dec 8, 2011
  Messages: 7,595
  Likes Received: 3,071
  Trophy Points: 280
  Tido ni shujaa tena jasili anayefaham vema kuitendea haki taaluma yake na kwa maana hiyo alidum kwa mafanikio yasio kifani BBC idhaa ya kiswahili.

  Kwa serikali ya maslahi viongozi, isiyojali watu na utu wa raia wake kama tanzania, wakati mhando anairekebesha TBC kuwa chombo cha kitaifa zaidi kwa maslahi ya uma na vizazi vijavyo watawala maslahi waliojaa ubinafsi urafi na wasiomuogopa mungu wakamtoa Dastan Tido Mhando na kuweka kibaraka wao.

  Kwa maana hiyo TBC imepoteza dira kabisa kwa sasa nyuzi 180. Badala ya kusonga mbele wao wanarudi nyuma tena kwa kasi ya ajabu.

  Kwa Tanzania viongozi waadilifu hawadumu bali mbumbumbu na wachumia tumbo hustawi kwa unafiki na porojo, ngojera zisizoisha huku wakiwahujumu viongozi bora wenyemalengo thabiti ya kuindeleza Tanzania.

  Mungu Ibariki Tanzania na uwalaani wote wanowafanya watanzania kuonekana maskini na mazezeta Duniani kote ilhali umetujaria utajiri usioelezeka, Mali asili- wanyapori, aridhi kubwa, madini, bahari na maziwa,misitu minene, na hatimae raia wapole na wapenda amani

  Lakini siku moja amani itageuka jehanamu na viongozi maslahi hakika watalia vilio na kusaga meno
   
 19. T

  Toshack Kibala Member

  #19
  Apr 1, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanaoiharibu TBC ni viongozi waliopo madarakani ambao furaha yao ni kuona habari wanazozitaka wao ndiyo zipewe kipaumbele kuliko zile ambazo wanahisi zitawahalibia mfano wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2010 kipindi cha mchakato majimboni ndiyo kilichomhalibia mzee Mhando.
   
 20. M

  Mmwaminifu JF-Expert Member

  #20
  Apr 1, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 1,096
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  exactly mkuu, kilichopo sasa ni TVT. Wamebakiza kubadili background colour na nembo tu!
   
Loading...