Safari ya Mwisho ya Mwanahabari Nguli wa Siasa, Marin Hassan Marine, Alianzisha Jambo TZ na Ameacha Alama ya TBC Aridhio

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,437
113,445
Wanabodi,
IMG-20240401-WA0160.jpg

Wale wenye nafasi, unganeni nami kupitia TBC Live kuangazia Safari ya Mwisho ya Mwanahabari Nguli wa Siasa nchini Tanzania, Mtangazaji wa TBC, Marin Hassan Marine, aliyefariki jana asubuhi kwenye hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam.

Marin Hassan Marine ndiye aliyeanzisha kipindi cha Jambo TZ, Safari ya Dodoma, Nyumba ya Jirani na ameacha alama kubwa kabisa ya kipindi kipya cha TBC Aridhio.

Kwa hapa Dar es Salaam, Mwili wa Marin uliswaliwa Msikiti Maamur hapo jana, na kusafirishwa kwa ndege ya rais kupelekwa Zanzibar, Leo asubuhi mwili wa Marin umemaliza kuswaliwa katika msikiti wa Amaan na sasa ni safari ya kuelekea makaburi ya Mwanakwerekwe Uguja ambako ndiko kutafanyika maziko.

Baada ya msiba, TBC imetumiwa salaam mbalimbali za rambirambi zikiwemo kutoka kwa Rais wa JMT, Dr. John Pombe Magufuli ambaye ametoa ndege yake kuupeleka mwili wa Marin Zanzibar.

Kwa mujibu wa Yusuf Omar Chunda, Marin alianzia uandishi wa habari, katika gazeti la Al Noor, ndipo akaonyesha kupenda zaidi utangazaji, hivyo Chunda akamuombea ajira TVZ, akakubaliwa ndipo akajiunga na TVZ.

Saa hizi ndio maziko yanafanyika. Kwenye maziko hayo serikali inaongozwa na Waziri wa Habari, Dr. Harison Mwakyembe, Waziri Aboud wa Zanzibar na Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dr. Ayoub Rioba.

Wengi wamemwelezea Marin kama alikuwa mtangazaji ambaye sio wa kawaida. Alikuwa ni Mwanzisha njia. Waziri Mwakyembe amemzungumzia kama mtangazaji nguli aliyeimudu barabara.

Nikiwa TVT nilipostiwa Zanzibar hivyo nilifanya kazi na Marin akiwa TVZ na baadaye alipokuja kujoin TBC 2005 mimi tayari nilikuwa nimeisha ondoka, ila tukafanya nae mahojiano mbalimbali ndani ya Jambo Tanzania.
Maziko yamemalizika sasa ni dua ya mwisho.
MC ni Farouk Karim, amemkaribisha Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dr. Ayoub Rioba anazungumza
Dr. Rioba amemsifu sana Marin na kuahidi kumuenzi kwa kuzihifadhi kazi zake. Sasa anazungumza Waziri Mohammed Thabit Kombo.
Waziri Kombo anamzungumzia Marin alicheza nae, kama mtoto waliokuwa nae.
Marin alichaguliwa miongoni mwa vijana 13 kwenda kusomeshwa utangazaji nchi ya nje.
Waziri Kombo anasema, Marin ni kama samaki wa bwawani, akikua mkubwa sana, bwawa linakuwa dogo, hivyo akahamia bahari kubwa ya TBC kuendelea na kazi.
Kati ya watangazaji 13, ni watatu tuu ndio walirejea nchini. Huu ni uzalendo wa hali ya juu kwa taifa lake.
Waziri Kombo kamaliza, sasa ni zamu ya Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Dr. Harrison Mwakyembe

Kifo cha Marine ni pigo kubwa kwenye tasnia ya Utangazaji, Mwakyembe anaeleza. Mwakyembe amemshukru rais Magufuli kutoa ndege yake kumfuata mke wa Marehemu Dodoma, kisha ndege hiyo kuupeleka mwili wake Zanzibar, mwili huo uliandamana na Mkewe na mwanae, na viongozi wa serikali
Sasa anazungumza msemaji wa familia, Famia imeshukuru wote, kuanzia rais wa JMT, VP, Waziri Mkuu, Rais wa Zanzibar, Mawaziri wa Tanzania na Zanzibar, Uongozi na wafanyakazi wa TBC, wanahabari na Watanzania kwa jumla.
Sasa anazungumza mwakilishi wa Chama cha Mapinduzi CCM
Sasa anazungumza Mwakilishi wa Chadema, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu,
Salum Mwalimu anasema baada ya Marine kuanzisha Jambo Tanzania, hivyo awatia changamoto Channel Ten ndio wakaanzisha Barugumu
Salum Mwalim anaendelea kumwagia sifa Marin, kuwa thamani ya maisha ya binadamu sio umeishi umri gani, bali umeacha nini hapa duniani, Marin ametoa mchango mkubwa kwenye tasnia ya habari. Ameacha kitu, ameacha alama
Salaam mbalimbali za wasifu wa Marin zinaendelea kuelezwa. Moja ya sifa za ziada za Marin alikuwa ni mcha Mungu, ni mtu wa swala 5.

Mwisho wa matangazo ya Live ya TBC.
Watangazaji ni Khalid Gangana, na Mbozi Katala
Nimefanya RTD miaka 5, watangazaji huwa wanakufa, ila sikuwahi kusikia wakiwa coved live.
Nimefanya TBC miaka 5, watangazaji wanakufa lakini sikuwahi kuona mazishi ya mtangazaji yakiwa coved live.
Msiba wa Marin umeshtua sana kwasababu juzi tarehe 31 amesimamia TBC Ardhio, kesho yake akiwa kazini, jioni akazidiwa ghafla akakimbizwa Lugalo hospital. akalazwa jana asubuhi kachomoka!, it was a shock!.
Tulimpenda Marin Hassan Marin, Mungu amempenda zaidi.
RIP Marin Hassan Marin
Paskali

Paskali
 
PM kauli yako ya kusema umestaafu JF ndio inayokutesa....hata kama umestaafu uandishi wa habari haaminishi hauwezi kukataa kukaa kwenye majukwaa na kuwasikiliza na kutoa maoni yako kwenye tasnia iliyochukua sehemu kubwa ya maisha yako.....JF hapa panaitwa utakuja tu...
 
Wanabodi,
Wale wenye nafasi, unganeni nami kupitia TBC Live kuangazia Safari ya Mwisho ya Mwanahabari Nguli wa Siasa nchini Tanzania, Mtangazaji wa TBC, Marin Hassan Marine, aliyefariki jana asubuhi kwenye hospitali ya Lugalo jijini Dar es Salaam.

Marin Hassan Marine ndiye aliyeanzisha kipindi cha Jambo TZ, Safari ya Dodoma, Nyumba ya Jirani na ameacha alama kubwa kabisa ya kipindi kipya cha TBC Aridhio.

Kwa hapa Dar es Salaam, Mwili wa Marin uliswaliwa Msikiti Maamur hapo jana, na kusafirishwa kwa ndege ya rais kupelekwa Zanzibar, Leo asubuhi mwili wa Marin umemaliza kuswaliwa katika msikiti wa Amaan na sasa ni safari ya kuelekea makaburi ya Mwanakwerekwe Uguja ambako ndiko kutafanyika maziko.

Andamana nami.

Paskali
Pascal si ulituaga jana wewe?
Au ilikuwa April fool?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom