Je, technology ya V.A.R inaweza kutumika kwenye udanganyifu?

SAYVILLE

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
5,135
7,903
Nimefuatilia kwa karibu matumizi ya V.A.R katika mashindano ya CAF na kusema ukweli huwa sina imani na jinsi zinavyotumika hasa pale timu mojawapo ni ya Afrika Kaskazini.

Kwa mfano najiulizaga kwa nini siyo kila replay ya V.A.R huwa inaonyeshwa? Nimeona matukio mengi ambayo mpira unasimama ili refa afanye review ila replay haionyeshwi. Mwarabu akijiangusha ndani ya box, refa akireview akasema siyo penati, replay haitaonyeshwa maana inaweza kusababisha apewe kadi kwa udanganyifu. Nakumbuka pia mechi ya kwanza ya Simba na Wydad, kuna foul alifanyiwa Baleke kwa kusukumwa akiwa anaelekea kufunga ila replay ilionyesha upande mmoja tu ambao haukuwa na msaada kuonyesha kama foul kweli ilitendeka.

Kuna ile video technology inayotumika kwenye chambuzi ambapo unaweza kusogeza mchezaji kutoka aliposimama, je wale wataalamu wa V.A.R hawawezi kutumika kumsogeza mchezaji aonekane yupo au hayupo offside maana kuna nyakati wanaonyesha tu picha mgando halafu wanachora mstari?

Jana katika mechi ya Wydad na Mamelodi, nilishangaa baada ya goli la kwanza la Mamelodi, kipa wa Wydad alimuonyesha refa ishara ya handball, ila ukireview lile goli hakukuwa na dalili zozote za handball kufanyika kwa sababu kwanza mipira yote ya mwisho ilikuwa inatambaa chini, nikakumbuka waarabu hata ukiwafunga kihalali, huwa wanajaribu kuweka mazingira kuonyesha wameonewa au umependelewa wakati kawaida wao ndiyo michezo yao hiyo.
 
🤔🤔🤔🤔🤔🤔

Scars njoo huku
 
Back
Top Bottom