Je, Taifa litaokolewa na wakina Mama?

Arafat

JF-Expert Member
Nov 17, 2009
2,582
2,000
Ukiangalia kwa makini toka JPM kuingia madarakani na hasa baada ya bahari ya siasa kuwa na mawimbi makali na dhoruba za kuhogofya, wanaume waliokuwa kwenye siasa za kukosoa CCM na kumkosoa JPM wengi walinywea na wengine walirudi CCM.

Kwa upande wa wanaume, mtu pekee aliyebaki moto kama moto alikuwa Tundu Lissu kiasi kwamba, yamkini dawa yake pekee ilionekana ni bora awe eliminated, kutokana na analysis za wasiojulikana.

Pamoja na moto wa Lissu, kundi ambalo lazima tulipe heshima yake ni kundi la wakina Mama, hili kundi halikutetereka sana na dhoruba za siasa za utawala wa JPM. Wadada wamesimama imara na hata katika uchaguzi huu kwa tathimini yangu, naona Wamama ndio nguzo kuu ya ukombozi sasa. Warembo wa Chadema wapo imara zaidi kuliko vijana wengi wa kiume tulio nao katika Taifa letu. Ukiwasoma kwa makini vijana wengi wanaoshabikia CCM ni uoga na hasa uoga wa maisha.

Kwa kizazi cha sasa, hili kundi la Wamama limenishwishi kuwa sio kundi la waoga ukilinganisha na vijana wa kiume wa sasa. Naona ndio kundi litakalo simama imara kutuvusha siku utawala wa mabavu ukitubana mbavu.

Kwaajili hii, naomba mniunganishe na Mdada mmoja wa Chadema ambaye hajaolewa ili awe mentor wangu kunijenga ujasiri.
 

CAPO DELGADO

JF-Expert Member
Aug 31, 2020
1,136
2,000
Mfano halisi ni Mke wa kafulila JESCA KISHOA NA DAVID KAFULILA CCM.

ila kafulila ni muoga jamani
 

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
8,674
2,000
Wadada wamesimama imara na hata katika uchaguzi huu kwa tathimini yangu, naona Wamama ndio nguzo kuu ya ukombozi sasa. Warembo wa Chadema wapo imara zaidi kuliko vijana wengi wa kiume tulio nao katika Taifa letu.
Hata ktk biashara ya manunuzi ya wapinzani wabunge wa kike walionunuliwa ni wachache sana ukilinganisha na wanaume.
 

Keynez

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
1,961
2,000
Nadhani hi tathmini CHADEMA tayari wanaifahamu.

Tukumbuke pia kwa miaka mingi tulikuwa tunaambiwa mtaji wa ushindi wa CCM ulikuwa ni wanawake na kura za vijijini. Leo hii tunaona huko kote CHADEMA wana support kubwa.

Cha ajabu CCM kwa makusudi kabisa kimemtenga mwanamke, kwa sera zao, kwa kauli za majukwaani na kwa vitendo vya wazi vya unyanyasaji. Sijui wanategemea nini kwa kufanya haya?
 

Malcom XX

JF-Expert Member
Sep 12, 2020
448
1,000
Ukiangalia kwa makini toka JPM kuingia madarakani na hasa baada ya bahari ya siasa kuwa na mawimbi makali na dhoruba za kuhogofya, wanaume waliokuwa kwenye siasa za kukosoa CCM na kumkosoa JPM wengi walinywea na wengine walirudi CCM...
Salome makamba
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom