Je synnovate ni mali ya ccm ??. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Je synnovate ni mali ya ccm ??.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by politiki, Sep 22, 2010.

 1. p

  politiki JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2010
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  Kitendo cha wana synnovate kuja juu kwa hasira nyingi za kufikia kutaka kushitaki vyombo vya habari vilivyoripoti habari zilizotolewa na mbowe kwenye mkutano wa hadhara kinatia shaka sana kama synnovate ni taasisi huru kama inavyodai. sababu ya kuoji ili ni kuwa kulikuwa hakuna sababu yeyote kwa synnovate kupaniki kiasi hiki na kuja juu kutishia kushitaki vyombo vya habari vilivyoripoti kauli ya mbowe. wasiwasi wangu ni kuwa synnovate wameshakula pesa za CCM km ambavyo wamekuwa wakifanya miaka ya nyuma kwa ajili ya kuwafumba watu macho sasa walioliwa pesa zao CCM wanakuja juu na ndio maana tunashuudia synnovate kupaniki namna hii. Taasisi yeyote ambayo aipokei pesa kutoka CCM ilikuwa haina sababu za kupaniki hovyo namna hii. Taasisi inayojieshimu itakanusha habari na kuonyesha ukweli huko wapi ili watu waamue pumba ni zipi na mchele ni upi?? na siyo kupaniki namna hii na kuanza kuvitisha vyombo vya habari hii inaonyesha wazi kuwa taasisi hii huenda ikawa inatumiwa CCM na siyo huru km inavyodai na hasa ukizingatia matamko ya nyuma ya ajabu ajabu kuwa watanzania wanachukia utendaji wa serikali na mawaziri wake lakini wananchi wanampenda sana kikwete inaonyesha wazi kuwa wana bwana wanaemtumikia na si Taasisi huru km ambavyo wangependa tuamini.
   
 2. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,939
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  Wanajua wataambiwa wamekiuka sheria za usajili wa kampuni na kuombwa kurudi Kenya!
   
 3. Emma Lukosi

  Emma Lukosi Verified User

  #3
  Sep 22, 2010
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Mtu akikuita chizi then ukapanik na kuanza kumrushia mawe, watu hawatoshangaa kwani uthibitisho umeshauonyesha, kuwa wewe ni chizi hatari tena wa kuogopwa. Kama CCM ikishinda* synovate wangekua na hali ngumu sana mwakani.
   
 4. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #4
  Sep 22, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Kuna Mdau kaniambia hiyo Synnovate ni Mradi wa Prof. Mkandala wa UDSM, na si mnajua yupo pale kwa uteuzi wa JK so lazima amfanyie kazi bosi wake
   
 5. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2010
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Na REDET ni ya nani? Mie nilidhani ni REDET tu ndo ya Mkandala?
   
 6. M

  Msavila JF-Expert Member

  #6
  Sep 22, 2010
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 404
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Taasisi nyingi za kutafuta maoni katu hazifanyi kazi bila kulipwa na yule anayezitaka. Sasa usambazaji wa matokeo si wa Synnovate bali mlipaji. Kinachowasumbua Synnovate ni kuwa matokeo yameonwa na wasiotakiwa kuona. Kama utafiti umelipiwa na CCM na matokeo hayawapendelei, basi CCM au yeyote atatumia ripoti hiyo kurekebisha mapungufu. Na Mpinzani wa wake akiyapata atakandamiza kishenzi maana keshamkaba koo. Nakumbuka Ngombale Mwiru alipojibu kuhusu usawa katika vyombo vya habari vya Taifa. Alisema " Mnapogombana mieleka huwezi kumpa mpinzani wako kisu". Ripoti hiyo ni kisu kwa wapinzani wa CCM na wtakitumia ikibidi kumtegua kwenye mieleka hiyo!! Ukweli pengine, kwa wengine, ndio unaonekana sasa. He who pays the piper chooses the tune. Synovate is a business entity and will work for anyone who can pay them no matter what. They have to survive in this jungle.
   
 7. Emma Lukosi

  Emma Lukosi Verified User

  #7
  Sep 22, 2010
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  so true
   
 8. V

  Vaticano Member

  #8
  Sep 22, 2010
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 75
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata mkilazimisha na kutoa polls za kizushi, hiyo haitawasaidia. Kura hazipigwi kwenye vyombo vya habari na kwenye poll result.
   
 9. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #9
  Sep 22, 2010
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  Kifupi MBOWE kawashika pabaya!! Hawana ujanja mwaka huu kilichobakia wana anzisha BIFU na GAZETI la MWANANCHI, baada ya kuona WANASHINDWA KULINUNUA.

  Kama wanazweza watoe matokeo tuone nini kilichomo wakisema vile walivyozoea ya 88% CCM watu wata washangaa, yani kichobakia labda wapoze waseme 50/50 hata hivyo watanzania hawawezi kuwakubali.
   
Loading...