Je, Supermarket na migodi huwa wanapenda kuagiza hadi mchicha nje ya nchi?

CHASHA FARMING

JF-Expert Member
Jun 4, 2011
7,791
8,934
Leo nimeona Sijui ni Waziri au nani anadai ni marufuku kuagiza Michicha nje. Kwamba Migodi wanaagiza michiche nje.

Kipindi cha nyuma napo ilikuwaga mijadala kwamba Super Market wanaagiza kila kitu nje. Wanaagiza hadi nyanya nje. Wanaagiza sijui viazi nje.

UKWELI NILIO WAHI KUUPATA.

Mwaka juzi nazani 2016 niliwahi kuonana physical na Meneja manunuzi wa Super Market ya NAKUMAT kabla hawajafunga biashara Tanzania. Nilikaa naye Offisini Arusha saaa nzima tulionge na sana nilitaka kujua Ununuaji wa vitu kama matunda na mboga.

MAJIBU YAKE.
Alicho niambia ni kwamba wao tena wana pata hasara sana kuagiza nje ya nchi na si kwamba wana penda bali inawabidi. Inawabidi kuagiza kulinda Brands yao. Wanapo agiza nje profit Margin huwa ni ndogo kwa sababu mzigo huja kwa ndege tena ya Abilia.

Sababu alizo niambia kwa product za Kitanzania

1. Quality ilikiwa ni tatizo na hapa ndo tatizo kuu lilipo.

2. Quantity- Hapa alidai Mtu anapewa Oda vizuri atasupply wiki za mwanzo baadae utashangaa analeta nusu ya kinacho hitajika na anakuja na sababu kibao hadi misiba mara alivamiwa na wezi mara sijui nini.

3. Inconsistent- Hapa ni Quality ila ni pale Bidhaaa inapo kuja ina quality tofauti,kuku wanaletwa wengine wana rangi Orange wengine rangi nyeupe, Mtu analeta viazi saizi tofauti tofauti.

4. Packaging- Hapa alidai sio changamoto sana kwa sababu walikuw Wanaweza ku repack kwa kutumia package zao endapo supply alikuwa na shida ya Packaging.

5. Supplier kuingia mitini bila kutoa taarifa- Yaani ana supply akisha lipwa anaweza asionekane tena na hajatoa sababu za kwa nini ameacha. Au siku ya kuleta mzigo kama ni asubuhi walipatana hataonekana matokeo yake analeta mchana. Hii inawaumiza sana.

Kwenye Quality hapo ndo kulikuwa na changamoto kubwa sana kwa sababu aliongelea hadi madawa zile Chemical.

Baada ya NAKUMATI nilikuja kuongea pia na Meneja wa Super Market ya Fool Lover. nae aliniambia yuko tiyari muda wowote ule kuchukua mzigo. Hapa nilifanya nao biashara na kweli quantity ikaja ikanishinda yale yale nilio elezwa na NAKUMAT.

Nimewahi pia kuongea na Shorpez wale nao ni hivyo hivyo.


Watu tuwekekeze kwenye Quality Jamani nenda Super Market hizo angalia Quality ya vitu wanavyo leta kutoka Nje hasa South africa angalia Packaging zao.

Super Market wako kifaida wao hawana shida na Product wanacho angalia ni Quality tu na Uwezo wa ku supply.

So tuache visingizio na lawama kwa hizi Super Market na Migodi.

Hivi wanataka migodi wanunue michicha ambayo hujui Source yake? Hujui inalimwa wapi na nani na inatunzwa vipi?

Nani anaue jua Tikitiki anazo kula zimetoka shamba gani? Je unajua Tango unazo kula zimelimwa na nani?
 
Uzi mzuri sana, nimejifunza vingi.

Hapo kwenye kujua tikiti limelimwa na nani au limelimwa shamba lipi wakulima wadogo wanafanyaje ili kuvuka hiki kikwazo.?
 
Kuna rafiki yangu alikuwa ana-supply mayai yenye kiini cha njano wakati huo Shoprite. Kuna siku aliona bidhaa flani ninayo na ambayo ilikuwa inauzwa na ndugu yangu. Aliipenda sana akaomba afanye biashara naye, kusema kweli kama kuna swali alikuwa anauliza zaidi ya mara tatu kwa siku ni kuhusu 'uchakachuaji' na uaminifu wa huyo Ndugu yangu.

Na alikuwa wazi, kwamba hiyo bidhaa (ni ya kilimo) ikigundulika imechakachuliwa maana yake tumeua biashara yake na Shoprite.

Kama kumbukumbu zangu zipo vizuri Arusha kuna wazalishaji wa mbogamboga na wana mikataba na wauzaji wanaouza nje ya Nchi (Ulaya). Njombe na Rungwe parachichi zinasafirishwa soko la Ulaya tena in tones. Naamini wapo wanaoweza kufanya hivyo pengine kuna tatizo zaidi ya hilo
 
Nimeiona hiyo taarifa jana star tv, waziri alitakiwa aulize ni kwanini wanaagiza kutoka nje. Narudia tena na tena kumuuzia chakula mzungu si lelemama
 
Back
Top Bottom