Kwa pamoja tutashinda.. Si mara ya kwanza watawala kutaka kutufunga midomo, kitu wasichoelewa ni kuwa katika ulimwegu huu wa sasa huwezi kuwafunga watu wote na kwa muda wote midomo.
Walianza na wapinzani, wakaja kwenye Bungelive, wakaenda kwenye vyombo vya habari, wakayafungia magazeti sasa wanataka kuchukua hata hiki kitu kidogo tulichobaki nacho? (yaani mtu kutoa mawazo yake bila kumuogopa mtu yeyote).
Kuwaacha watawala wafanye watalao kana kwamba sisi ni watoto wadogo nini kosa ambalo halitakiwa kufanywa na kizazi hiki ni lazima watanzania bila kujali itikadi zetu tuchore mstari, tuwambie watawala mpaka hapa basi, tumewachangua kwa ajili ya kutuongoza si kwa ajili ya kutupangia cha kusema.
Na kwa hili tutafanikiwa ikiwa sotekwa pamoja tutashikamana na kupigania haki yetu.